Tuesday, 29 July 2014

DAFU HUJA NIMALIZA

DAFU HUJA NIMALIZA
Kila kiwona mnazi,akili huja dafuni,
Hata kama si mkwezi,na kuzubaa sokoni,
Makuti na siyabezi,akili ipo dafuni,
Dafu huteka akili,kila kiona mnazi.

Sitaki kusema wongo,kiona nasisimka,
Tachanganywa ubongo,dafu kutaka zidaka,
Naweza kutoa hongo,japo dafu kuzishika,
Makuti na hilo shina,wala sina hamu navyo.

Zimejipanga vyema,nikizona nazubaa, 
Macho ntatoa pima,kisa dafu kushangaa,
Hapo ipo yangu homa,dafu siji zikataa,
Mie dafu ndiyo nazi,vingine ni kama kero.

Zile dafu za kijani,siwezi kuzikinai,
Zikipambwa natamani,nikipewa sizubai,
Naweza kuswekwa ndani,na tuhuma sikatai,
Madafu yale mapacha,kwangu naona dhahabu.

Raha yawe mwake ndani,bila kutoa maganda,
Usiyatoe nazini,damu yaweza niganda,
Nitachelewa na kazini,na kugombana na konda,
Mie homa yangu dafu,sijui wewe ni nini.

Alo macho haambiwi,kujua nini nasema,
Wala hatumsumbuwi,asije mbele kusema,
Jama dafu hazijui,arudi shule kusoma,
Dafu changa huchanganya,waweza maliza ada....****

0 comments:

Post a Comment