Sunday, 27 July 2014

MASIKINI SABRINA SEHEMU YA KWANZA


RIWAYA;MASIKINI SABRINA
MTUNZI;Moringe John Mhagama
SEHEMU YA KWANZA
Mara tuu baada ya kushinda kwa kura nyingi na kushika rasmi urais wa nchi ya Malawi Mheshimiwa Jonathan Mkandawile ambaye kabla ya hapo alikuwa mtangazaji katika kituo kimoja cha redio mjini Lilongwe,kitu cha kwanza ni kutekeleza ahadi yake ya kupambana na madawa ya kulevya ambayo yalionekana kuichafua nchi yake kimataifa.Kila raia kutoka Malawi aliyefanikiwa kuingia nchi nyingine alikutana na ukaguzi wa hali ya juu kutokana na kupoteza imani juu yao.Lilikuwa ni jambo lililotia faraja kwa raia na hata nchi jirani kuwa walau kiini cha biashara hiyo haramu kimeanzisha mapambano hayo ambayo yalikuwa yakigusa viongozi na wafanyabiashara wakubwa barani Afrika na Asia.
Lakini jambo moja lililofanyika katika kijiji kimoja kilichopo
mpakani mwa nchi hiyo na Tanzania lilibadili matumaini ya watu wote huku asasi nyingi za kiraia zilikilaani jambo hilo.
Kuuawa kikatili kwa mtoto mlemavu na kikosi cha kupambana na biashara hiyo haramu .
Kila gazeti la nchini Tanzania lilipambwa na picha na habari kumuhusu mtoto Sabrina ambaye Mwandishi wa mashairi na hadithi ndugu Moringe john ambaye alikuwa ni binamu yake alikuwa akimwandika sana katika kazi zake kama njia mojawapo ya kumpa heshima ndugu yake huyo ambaye kutokana na kuishi naye kwa muda mrefu alikuwa ni zaidi ya ndugu yake.
Tahariri nazo zilimhusu huku nyingi zikishutumu kitendo hicho cha kumuua mtoto huyo mlemavu ambaye ilidaiwa alikamatwa na madawa ya kulevya yakivushwa mpakani.
''Mtoto kilema asiye na uwezo wa kufanya chochote zaidi ya kuona atawezaje kufanya biashara hiyo?
''Je mtu akishikwa na madawa huuawa?ni sheria ya wapi?na kama alibambikwa? ni baadhi yamaswali yalioulizwa na watanzania wengi huku wanasiasa wakilaani kitendo hicho na wengine wakimtaka Rais wa Jamuhuri wa muungano wa Tanzania kutoa tamko juu ya jambo hilo.
''Rais utuambie msimamo wa nchi yetu''
''Mheshimiwa kwa hili usikae kimya'' yalisomeka mabango mengi yaliyokuwa yakilaani kitendo kile kilichofanywa na askari wa Malawi.
Rais alitakiwa kutoa msimamo kutokana na jambo lile ambalo liliendelea kuwa mada ya kila mazungumzo na sababu ya maandamano yaliyohusisha wafanyabiashara ,wanavyuo na hata wananchi wa kawaida nchini hasa karibu na sehmu yalipotokea mauaji yale.
Lakini wakati hayo yakiendelea nchini upande wa pili ambako ndiko walioshutumiwa habari ilikuwa nyingine kabisa kwani vyombo vya habari viliongelea taarifa ile tofauti kabisa hali iliyofanya kusitishwa kwa mazishi ya mtoto yule aliyeuawa ilio kupisha uchunguzi mwingine juu ya kifo kile.
''kiongozi wa dini amponza mlemavu''
''Dunia imekwisha kiongozi wa dini asababisha kifo kisa madawa''
Na maneno mengine mengi ya shutuma juu ya kiongozi wa dini ambaye hakuna aliyemjua wala kuzisikia habari zake nchini Malawi.
Uhasama na shutuma zilianza kupunguzwa na taarifa hiyo na kuwafanya watu waanze kulitazama jambo hilo kwa jicho la tatu.
Habari zilizidi kukanganya na kuchanganya wananchi ambao  hawakuujua ukweli juu ya jambo lile lililokuwa likiendelea nchini mwao.
Akiwa na mawazo lukuki,mpelelezi aliyeheshimika na idara yake ncini Malawi bwana Paul Mazanda alijibwaga kochini kabla ya kufungua chupa ya maji na kuanza kuyanywa.Mawazo yalipita kichwani mwake harakaharaka tangu siku ya kwanza alipoitwa na shuleni alikokuwa akisoma sekondari na kuingizwa kwenye kazi hiyo hadi wakati ule ambapo alikuwa akiona ni mwisho wake wa kuishi.Hakuwa na tumaini la maisha tena,lakini aliona ni kifo cha haki kwani alifanya hivyo kuliokoa taifa lake baada ya miaka mingi ya aibu na fedhea duniani.Kifo hakikumtisha, kwani aliamini kila aliyezaliwa angekufa pia alikikwepa mara nyingi kazini kabla ya kukikaribia kwa wakati ule,majibu ya daktari yaliyoandikwa kwenye karatasi iliyokuwa mezani pake na maelezo aliyopewa na daktari muda mfupi uliopita yalipunguza matumaini ya kuendelea kuishi tena.
''Kwa sasa ugonjwa huu hauna tiba duniani kwote ,labda nchini China walikuwa na dawa za kuupooza tuu makali yake''Sauti ya daktari  iliyojaa tumaini lisilo na maana ilisikika na kumfanya aliyeambiwa maneno  hayo abaki kimya bila kuongea kitu chochote.
Sauti ya daktari bigwa wa magojwa ya damu ilijirudia akilini.
Mazanda alipata ugojwa hatari ulioingia nchini Tanzania ambako nako ilisemekana uliingizwa na wahamiaji haramu kutoka Somalia.
Ugonjwa ulioshambulia seli nyeupe za damu kabla ya kusababisha mauti ndani ya masaa tisa tangu kuonekana kwa dalili zake ulimpata Paul Mazanda.Kitu kilichompa faraja ni kule kuupata ugonjwa ule akiwa kazini akilitumikia taifa lake,kwani alifanikiwa kuukata moja mirija ya uingizaji wa madawa ya kulevya yaliyokuwa yameichafua Malawi kimataifa.Aliamini kabisa mtu aliyemwambukiza ugonjwa ule alikuwa ni Mwanamke mmoja aliyekytana naye nchini Tanzania na kujifanya amevutiwa naye lakini lengo likiwa ni kupata taarifa za kipelelezi alizokuwa akizihitaji.
Huku akijua kuwa kulikuwa na hatari ya kupata magonjwa ya zinaa alijikuta anasukumwa na uzalendo kulifanya jambo lile kwa manufaa ya taifa lake.
Wakati anawaza hayo mara simu yake iliita na alishtuka baada ya kuona namba iliyopiga.
Ilikuwa ni simu kutoka ikulu na aliifahamu kutokana na idadi ya tarakimu na alizipokea simu kama hizo mara chache sana kunapotokea jambo la msingi na lililogusa maslahi ya taifa na kumtaka kulipeleleza.
Kama alivyotegemea ilikuwa ni simu kutoka ikulu safari ile ilikuwa ni ya Rais wa nchi ile aliyemtaka afike ikulu mara moja.
Alitoka nje haraka na kuingia garini kisha kuliondoa kwa kasi hali iliyowafanya watu kushika vichwa vyao baada ya kuliona gari lile jinsi lilivyoendeshwa kwa fujo.Simu ile ilimweka kwenye hali ya kawaida huku mawazo juu ya ugojwa aliokuwanao yakipotea kwa muda.
''Pita anakusubiri ndani''ni kauli aliyoisikia kila alipokutana na wafanyakazi wa ikulu na kumfanya aamini wito wake ulijulikana kabla.
''Mmefanya nini sasa?,hatuaminiki tena ''Paul alisikia sauti ya amiri jeshi mkuu ambaye ni rais akizungumza kwa ghadhabu mara tu alipoingia alipoelekezwa kwenda hali iliyompa woga kabla hata ya kukaa aliona nguvu zilimwisha na kuanguka kama mzigo
Je, nini kiliendelea?
TUKUTANE JUMAPILI JIONI

0 comments:

Post a Comment