Tuesday, 29 July 2014

NATAMANI NIWE KULE


.
NA MIE NINA TAMAA
Natamani niwe pale,walipofika wenzangu,
Niandike kama yule,niandike kwa uchungu,
Nami nizitoe shule,kama walivyo wenzangu,
Natamani niwe nyemo,ama alivyo Matimba.

Kila ninapoandika,nawawaza hawa watu,
Manjonjo ninayaweka,wayapende wengi watu,
Akili nije zishika,kama vile dada Atu,
Junior ananifunza,siku nimkaribie.


Shalua ananishika,dawa yao usiseme,
Nawaza nije andika,uwanjani mnisome,
Karlos kaka andika,uwanjani tusihame,
Natamani niwe kule,walipofika wenzangu★★★★


0 comments:

Post a Comment