Sunday, 10 August 2014

PUMZIKA KWA AMANI MDOGO WETU IBRAHIM


UBEPARI UMERUDI
Si siasa jamani,ni kweli yametokea,
Imeniuma jamani,jambo niloshuhudia,
Kama mambo ya zamani,yale tuliyosikia,
Ubepari umerudi,ubepari wa mweusi.

Mtu anafuga mbwa,si dhambi ninatambua,
Anapendwa huyo mbwa,hata akija kuua,
Kila siku anaomba,mbuzi wanateketea,
Ubepari umerudi,ubepari wa mweusi.

Wengine kwenye mashamba,amani hawaioni,
Mbuzi wetu kwenye nyumba,nje hakuna amani,
Kweli mbwa kama simba,basi mweke mbugani,
Ubepari umerudi,ubepari wa mweusi.

Juzi mwana ameua,kaua mwana mdogo,
Eti watoa fidia ,waona ni jambo dogo,
Ni mzaha waongea,kubwa walipa kisogo,
Ubepari umerudi ,ubepari wa mweusi.

Ashangaza huyu bwana,anavyofanya mzaha,
Baba kamkosa mwana,ni kweli si mzaha,
Polisi tumewaona,nanyi mwafanya mzaha,
Ubepari umerudi,ubepari wa mweusi.

Vyovyote itavyosemwa,uzembe unachangia,
Sio kamwa mwatukanwa,ukweli twawaambia,
Leo mmevumiliwa,kesho msije kimbia,
Ubepari umerudi,ubepari wa mweusi.

Pole kwenu wanafunzi,mlomzoea Ibu,
Pia kwa wake wazazi,mungu atatoa jibu,
Pia kwenu viongozi,mnaiona aibu,
Uepari umerudi ubepari wa mweusi.

PUMZIKA KWA AMANI MDOGO WETU IBRAHIM

UBEPARI UMERUDI
Si siasa jamani,ni kweli yametokea,
Imeniuma jamani,jambo niloshuhudia,
Kama mambo ya zamani,yale tuliyosikia,
Ubepari umerudi,ubepari wa mweusi.


Mtu anafuga mbwa,si dhambi ninatambua,
Anapendwa huyo mbwa,hata akija kuua,
Kila siku anaomba,mbuzi wanateketea,
Ubepari umerudi,ubepari wa mweusi.

Wengine kwenye mashamba,amani hawaioni,
Mbuzi wetu kwenye nyumba,nje hakuna amani,
Kweli mbwa kama simba,basi mweke mbugani,
Ubepari umerudi,ubepari wa mweusi.

Juzi mwana ameua,kaua mwana mdogo,
Eti watoa fidia ,waona ni jambo dogo,
Ni mzaha waongea,kubwa walipa kisogo,
Ubepari umerudi ,ubepari wa mweusi.

Ashangaza huyu bwana,anavyofanya mzaha,
Baba kamkosa mwana,ni kweli si mzaha,
Polisi tumewaona,nanyi mwafanya mzaha,
Ubepari umerudi,ubepari wa mweusi.

Vyovyote itavyosemwa,uzembe unachangia,
Sio kamwa mwatukanwa,ukweli twawaambia,
Leo mmevumiliwa,kesho msije kimbia,
Ubepari umerudi,ubepari wa mweusi.

Pole kwenu wanafunzi,mlomzoea Ibu,
Pia kwa wake wazazi,mungu atatoa jibu,
Pia kwenu viongozi,mnaiona aibu,
Uepari umerudi ubepari wa mweusi.

PUMZIKA KWA AMANI MDOGO WETU IBRAHIM

0 comments:

Post a Comment