Sunday, 17 May 2015

NAHITAJI JIBU LAKO


Zimepita siku nyingi,mori nanze kuandika,
Nilivyoweka ni vingi,hadi kusoma mwachoka,
Hadithi za mitomingi,na visa hadi mwacheka,
Mashairi na hadithi,kipi mimi nakiweza.
Kama sina niwezacho,semeni mie niache, 
Sije kuwa kichekesho,kila siku mi nikeshe,
Leo kwenu iwe mwisho,riwaye nikaziache,
Mashairi na hadithi, kipi mimi nakiweza.

Kama naweza kimoja,semeni nisijichoshe,
Mori nisiwe kioja,siku zote nisikeshe,
Nilishike langu moja,roho zenu nizikoshe,
Mashairi na hadithi,kipi mimi nakiweza.

Mashairi nayapenda,niyasome ya wenzangu,
Nazo hadithi napenda,nifanyaje ndugu zangu,
Napenda mkiniponda,nijue kipi fani yangu,
Mashairi na hadithi,kipi mimi nakiweza.

Msomeni kaka nyemo,ama omari maguza,
Tuseme tulikuwemo,ila hatukuongoza,
Wao wamenipa somo,maarifa kuongeza,
Mashairi na hadithi,kipi mimi nakiweza.

Kama vyo naviweza,ndugu mniambieni,
Ukiweza nipongeza,niambie hapa chini,
Muda nisijepoteza,kuwaza niweke nin
i,
Mashairi na hadithi kipi mimi nakiweza?

0 comments:

Post a Comment