Sunday, 24 May 2015

SHAIRI;HII SIKU MWAKA JANA


Haikuwa ijumaa,japo tarehe ni kumi,
Sikuwa nimezubaa,kama nazuru Mikumi,
Ilikuwa ni furaha,amani tele moyoni,
Siku hii mwaka jana,ilikuwa safi sana.

Mapema nawasha simu,ninapokea salamu,
Natafakari salamu,naganda kama sanamu,
Wa ukweli na muhimu,kanitumia salamu,
Siku hii mwaka jana,ilikuwa siku safi.

Tabibu wa moyo wangu, wengi mnamfahamu,
Natamani awe kwangu,ngoja ashike elimu,
Namweka moyoni mwangu,nafasi hii adimu,
Siku hii mwaka jana, ilikuwa siku bora.

Alimpigia mama,mama alozaa chema,
Nitampenda daima,hata leo ninasema,
Mama aloleta chema,ni’pe nini huyu mama,
Siku hii mwaka jana ,ilikuwa siku njema.

Yupo wapi huyu wangu,simuni hapatikani,
Nimepata na machungu,mwenzangu haonekani,
Mpenzi urudi kwangu,nifurahi duniani,
Leo ya mwaka jana,tofauti kubwa sana.

0 comments:

Post a Comment