Tuesday, 19 May 2015

SHAIRI;HIZI NI KAULI ZAKE


Nitakufa masikini,sijui nilifanyalo,
Na anajuta kwa nini,hakujua asemalo,
Anipende nina nini,na wala sina viwalo,
Yeye kaniona lofa,anajuta kunipenda.Alonaye ndiye bora,anajuta kuwa nami,
Nitazipata bakora,na kuvisaka vichomi,
Hata niwe Haji Gora,shairi langu hasomi,
Yeye kaniona lofa,anajuta kunipenda.

Siwezi kumchukia,ingawa ninaumia,
Wapi nitakimbilia,na mimi nikatulia,
Nashindwa kuvumilia,na bado namlilia,
Yeye kaniona lofa,anajuta kunipenda.

Siri zangu azijua,adai kunifichia,
Ila nikimzingua,nitajuta kumjua,
Moyo wangu waugua,mama anihurumia,
Yeye kaniona lofa,anajuta kunipenda.

Nitafute hadhi yangu,yeye matawi ya juu,
Japo alinita wangu,ukweli wake ni huu,
Sitokuja mwita changu,hata avunjike guu,
Yeye kaniona lofa,anajuta kunipenda.

Mama yangu akipiga,asema hana tatizo,
Shida mie nikipiga,nimeusaka mzozo,
Eti sijui kuoga,nanuka kama uozo,
Yeye kaniona lofa,anajuta kunipenda.

Bado mie nampenda,ila hivyo ameenda,
Sijui wapi kwa kwenda,ambako watanipenda,
Mori nazidi kukonda,hayupo wakunipenda,
Yeye kaniona lofa ,anajuta kunipenda

0 comments:

Post a Comment