Monday, 18 May 2015

SHAIRI;PENDO


Pendo ni kitu chema, wengi tunakitamani,
Mpate aliye mwema,ambaye hukuthamini,
Ni kama pendo la mama,vile anakuthamini,
Penzi lake mwenye pendo,’taona mana ya pendo.


Magonjwa na ulemavu,hayo hayana nafasi,
Hutopata maumivu,wala kuwa mbinafsi,
Pia huchangiwa na wivu,wivu ule wa kiasi,
Penzi lake mwenye pendo,'taona mana ya pendo.

Tamwona yeye mzuri,kuliko mtu yeyote,
Kila kitu kwenu shwari,hakuna shida yoyote,
Mengine huna habari, kila saa muwe wote,
Penzi lake mwenye pendo,’tapata mana ya pendo.

Pendo lake huyo wako,liwe kwako siku zote,
Akupende peke yako,na atuheshimu sote,
Iwe raha kuwa wako,ajivune kwote kwote,
Penzi lake mwenye pendo,'tajua mana ya penzi.

Mwisho napenda kusema,penzi halina kipimo,
Eti wenda kupima,kama upimavyo kimo,
Matendo yake yatasema,ndani yake kilichomo,
Penzi lake mwenye pendo,'tajua mana ya penzi.

0 comments:

Post a Comment