Friday, 22 May 2015

TULIA EWE NAFSI


Hisia za hii nafsi,zanifanya nigutuke,
Eti nijipe nafasi,wan'onao wasicheke
Nafsi yangu yanighasi,nami bingwa niibuke,
Nafsi yangu utulie,hili jambo siyo jema.


Kazi hii naifanya,nisuuze yangu nafsi,
Nafsi usije nifanya,mie kufwata mikosi,
Hilo jambo kulifanya, ni kujitia nuksi,
Nafsi yangu utulie,jambo hili siyo jema.

Kazi yangu kufundisha,na kujifanya mzazi,
Nafsi yangu yanichosha,pia si yangu malezi,
Yule mtoto wa ngosha,nisimfanye mzazi,
Nafsi yangu utulie,hili jambo siyo jema.

Eti nimfwate Wema,awe mama wa nyumbani,
Jema bado anasoma,kuna myaka thelathini,
Nini atawaza mama,alomleta shuleni,
Nafsi yangu utulie,hili siyo jambo jema.

Nafsi kweli wanitesa,kucha namwaza Wema,
Hivi hujui ni kosa,Wema bado anasoma,
Eti nikatoe posa,akimaliza kusoma,
Wema wangu nakupenda,jitunze nitakufwata.

0 comments:

Post a Comment