Tuesday, 19 January 2016

RIWAYA:MAMA YANGU MUUAJI


MTUNZI:MORINGE MHAGAMA
MWANZO
Kila mtu aliyefika pale nyumbani anionekana kunishangaa kwa mwonekano niliokuwanao,sikuonekana kabisa kushughulika na msiba ambao mimi ndiye mfiwa pekee wa moja kwa moja niliyekuwepo pale.Hakukuwa na ndugu mwingine aliyekuwepo  zaidi ya marafiki wa marehemu mama yangu ambaye katika  maisha yangu yote niliyoishi naye sikuwahi kuwaona ndugu  zake wengine hadi masaa machache kabla ya kifo chake ambapo aliniambia ukweli si tuu ulimuumiza yeye bali hata mimi uliniumiza sana na kufanya niamini kuwa mama yangu alikuwa muuaji kitendo ambacho sina hakika kama Mungu alimsamehe kwani hata kifo chake kilikuwa cha kujiua.


‘’Yule kijana kama hajafiwa yaani hana habari kabisa’’ilisikika sauti ya mama mmoja ambaye alionekana kuumizwa na tabia niliyooneshwa.
‘’Huwezi jua mama ni mama anaweza kuwa anaumia kwa  ndani’’Alijibiwa na mama mwingine wakati huo idadi ya watu ikizidi kuongezeka kwani marehemu mama yangu kabla ya kifo chake alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa na marafiki wengi nadhani kutokana na tabia yake ya kucheka na kila mtu aliyokuwa nayo .
‘’Hapana huyu kijana amezidi haiwezekani mtu umefiwa na  mama yako mzazi halafu masaa yote unacheza na simu yako tuu’’Alidakia mama mwingine ambaye kabla ya kifo cha mama alikuwa akija mara kwa mara pale nyumbani.
‘’Labda anawasiliana na ndugu zake awape taaarifa za  msiba’’Ilisikika sauti nyingine kwani kitendo changu cha kuonekana nimevaa 'earphones' kiliwapa uhuru wa kuongea  kwa sauti ya juu wakiamini sikusikia chachote ambacho walikiongea.
‘’Ana ndugu huyooo? mama yake hawajui si wa upande wa  baba si wa upande wa mama’’Yule mama aliyeanzisha  majadiliano aliongea akionekana kuijua historia yetu huku  maneno yake yakinifanya niondoke mahali pale na kuingia chumbani kwangu huku nikikumbuka yale aliyoniambia mama yangu nikijaribu kuyapima kama yalikuwa na ukweli wowote.
Nilikumbuka kauli ya mama kuwa aliamua kujiua kutokana na mambo kumwelemea na hatari iliyokuwa mbele yake kukosa njia ya kujiokoa.Sikutaka kabisa kuamini kama aliyoyaongea yalikuwa ya ukweli au kulikuwa na jambo lingine lililojificha hadi kumpelekea mama yangu ndugu yangu wa pekee niliyemfahamu hapa duniani.
Nakumbuka tofauti na siku nyingine mama yangu alirudi mapema siku ile akiwa kwenye hali tofauti na niliyomzoea siku zote kwani alikuwa na tabia ya kuingia pale nyumbani kwa matani na vichekesho vya hapa na pale kila alipofika.
Siku ile baada ya kutupa kibegi chake kochini alikaa chini na kuniomba nimpe chai jambo ambalo nililifanya kwa haraka kwani haikuwa kawaida kwake kuwa vile hivyo hali iliyonifanya niamini kuwa huenda alikuwa anaumwa.
‘’Mwanangu usiogope haya ni maisha ya kawaida unaonekana kumwogopa mama yako usimwogope leo ameamua kuwa mkali kama baba yako’’Aliongea mama yangu akikoroga
sukari kwenye chai aliyoimimina huku akijilazimisha kutabasamu tabasamu ambalo lilishindwa kuishi usoni pake hata kwa sekunde kumi na kicheko chake kikiishia kooni na kuniongezea hofu na si kunitia tumaini tena.
‘’Hapana mama utakuwa unaumwa au kuna watu wamekuvuruga huko kazini kwako ‘’Niliongea kwa masikitiko makubwa kwani mara nyingi ilikuwa kawaida kunieleza jambo lililomkera huko kazini kwake.
‘’Hapana mwanangu nataka nikuambie kitu kimoja muhimu sana ‘’Sauti yenye mikwaruzo ilisikika na kunifanya nimsikilize kwa umakini mkubwa.
‘’Kama kitu muhimu ndio uwe hivyo mama?’’Niliongea kwa hofu ambayo mama yangu aliigundua na kujifanya kucheka kicheko ambacho ni kama kilikuwa na ugonjwa kwani hakikuendana na hali niliyoiona usoni mwake.
‘’Ndiyo najua hunifahamu vizuri mwanangu nataka unijue mama yako nilivyo na sababu ya mimi leo kuwa hivi maisha haya hayaeleweki naweza hata nikafa hata usijue historia yako’’Aliongea mama yangu na kuchukua kikombe cha chai kisha kunywa funda moja.
‘’Kwani si ulishaniambia juu ya maisha yako mama kwa nini unapenda kukumbuka mambo yakuumizayo tumepata nafasi ya kubaki hai basi tuendelee kuishi huku kazi yako Mungu kakubariki kuifanya na inatufanya tuishi kwa hiyo hakuna ulazima wa sisi kundelea kulalamika…..’’
Uchungu ulionishika juu ya kumbukumbu ya maisha yetu zilinifanya nishindwe kabisa kuvumilia na kujikuta naanza kulia bila kujua historia ya maisha yake iliyo ya kweli ambayo kila nikiikumbuka inanifanya niseme’’ MAMA YANGU MUUAJI’’.
*******
Machi 27 1994 RWANDA
Chuki baina ya makabila mawili makubwa nchini Rwanda ilizidi kuongezeka huku watu wa kila kabila wakiamini kuwa wenzao kutoka kabila lingine ni watu wabaya na wasiostahili
kuishi jambo lililozidi kuchochea na kuongeza mauaji yale.Wahutu waliwaona Watutsi ni watu wabaya kwao huku upande wa pili ukiamini kinyume chake na mauaji yakizidi kuongezeka kila siku huku kila usiku ukiwa ni usiku wa mauaji ambako watu wengi walikuwa wakipoteza maisha kwa mateso makubwa.Umoja wa Mataifa na nchi nyingine zilionekana kulalamikia tukio lile huku vyombo vya habari vikihamishia kamera zao na wandishi wao kwenye nchi hiyo ndogo ambayo kabla ya vita vya kwanza ya Dunia ilikuwa ni sehemu ya Tanganyika pamoja na nchi jirani ya Burundi na habari kufikia hata idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la
Uingereza(BBC) kuandaa kipindi maalum cha mambo yaliyoendelea nchini humo wakiwahoji wanachi mbalimbali huku wakiongea na viongozi wa Serikali ambao nao hisia zao za ukabila zikijionesha kila walipohojiwa. Wakati hayo yakiendelea katika kijiji kimoja kilichokuwa
Mashariki kabisa mwa nchi ile mtoto mmoja alikuwa akitetemeka kwa hofu baada ya kushuhudia wazazi wake wakiuawa kinyama kupitia kitundu kidogo kilichokuwa chooni
kwani baada tu ya yeye kuingia chooni watu wenye silaha za jadi waliivamia familia yake iliyokuwa na wazazi wake na ndugu zake wawili wa kike na wakiume na kuwaua kikatili.
Alisubiri hadi wale watu walivyoondoka na kuanza safari ya kutoroka kijiji kile huku akiwa hajui ni sehemu ipi iliyokuwa salama kwake.Harufu ya damu za wazazi na ndugu zake ilisikika kila alipokumbuka kilichomfanya atoe machozi kila wakati.Safari isiyokuwa na mwongozaji ilipitia katikati ya msitu mmoja ambao aliusikia katika hekaya za wazazi wake kuwa ni msitu uliokuwa na maajabu mengi na lilikuwa ni jambo la kawaida kupotea kwenye msitu huo.
Safari isiyokuwa na mwongozaji ilipitia katikati ya msitu mmoja ambao aliusikia katika hekaya za wazazi wake kuwa ni msitu uliokuwa na maajabu mengi na lilikuwa ni jambo la kawaida kupotea kwenye msitu huo. Japokuwa alikuwa muoga lakini kitendo cha kushuhudia vifo vya wazazi wake kilimwongezea nguvu ya kusonga mbele akiepuka mauaji yale.Akiwa katikati ya msitu ule binti huyo mwenmye umri wa miaka mitano anazidiwa na njaa na kupoteza fahamu kutokana na njaa aliyokuwa nayo.
Baada ya masaa matatu kuna sauti za watu ambao walionekana kuwa makini kwa kila hatua waliosogea,waki mvizia nyoka mmoja mkubwa ambaye walikuwa wamemfuatilia kwa umbali wa zaidi ya kilometa kumi wakitaka kumuua ili tuu wapate ngozi yake ambayo ilionekana wakiihitaji sana kwa kipindi kile.Hawakujua kabisa uelekeo wa nyoka Yule ulikuwa ni kufuata chakula ambacho alihisi uwepo wake mahali pale.Chakula hicho hakikuwa kingine zaidi ya
mwili wa Yule binti aliyeyaacha magofu yakiwa na mizoga ya watu waliouawa na binadamu wenzao kisa kikiwa ni chuki tuu za ukabila japo kwa wakati ule aliambiwa tuu watu fulani ni
wabaya lakini hakuwahi kufikiria kuwa wanaweza kufikia hatua ya kuwaua ndugu zake.
Kwa kuwa jioni ilikuwa imekaribia watu waliokuwa wakimwinda yule nyoka ili tuu wamuangamize ili wapate walichokitaka bila ya kuvunja masharti ya mganga wao
aliyewataka wampelekee ngozi ya nyoka huyo ambaye alikuwa hajatoka kumla mtu ili dawa yao ifanye kazi vizuri.Na sharti gumu kabisa lilikuwa ni kumuua yule nyoka  saa kumi na mbili na
nusu jioni vinginevyo wasingepata walichokitaka,lakini ghafla walishtuka baada ya kumwona nyoka yule akiongeza mwendo na kuwafanya wahisi kuwa huenda aligungua kuwa alikuwa
anafuatiliwa ama kuna chakula mbele yake kwani nyoka huyo ilisemekana alikuwa akila nyama hasa za watu na hiyo ndiyo sababu ya watu wengi kuuogopa msitu ule na mara chache
alikuwa akivamia vijini na pwani ya ziwa Tanganyika na kuwavamia wavuvi.Ilisemwa kuwa nyoka huyo alikuwa ni Mungu wa kabila fulani nchini Burundi lakini makao yake
makuu yalikuwa ni katika msitu huo uliokuwa umepita kuanzia Burundi hadi sehemu ya Rwanda.
Hatimaye nyoka Yule alikuwa hatua mbili kabla ya kuufikia mwili wa msichana Delphine Daniel ambaye alikuwa amepoteza fahamu huku sababu kubwa zikiwa ni njaa na
uchovu wa safari ya kutwa nzima
‘’Shiii……’’ilisikika sauti iliyomshtua yule nyoka wakati huo zilikuwa zimebaki dakika kama kumi ufike muda waliomabiwa na mganga wao kuwa walitakiwa kumuua Yule nyoka, na
kumfanya yule nyoka aachane na chakula kilichokuwa mbele yake na kuwageukia maaadui wake ambao hakujua walimfuatilia kwa takribani masaa matatu yaliyopita.
Mapambano ya mikuki na mishale kutoka kwa watano waliokuja pale kwa lengo moja tuu la kumuua yule nyoka saa kumi na mbili na nusu.Lakini waliakiwa kumzuia tuu asiwadhuru ili dakika kumi zilizobaki ndipo wammalize.Sumu kali alizozitema ziliwafanya wawili kati yao wapoteze uwezo wa kuona wkani zilifika moja kwa moja machoni mwao na hata wale wengine walipata na muwasho uliowapunguzia umakini.
Hawakujua kabisa kama mwenzao aliyewekwa kwa ajili ya kuwasomea muda alikuwa amepoteza uwezo wake wa kuona hivyo walipambana tuu akisubiri wakati ufike.
‘’Mhh muda haujafika?’’Aliuliza mmoja wao huku akijikuna shingoni kwake baada ya kutemewa mate yenye sumu na yule mtu.
‘’Jamani sioni’’Alijibu Yule msoma muda akijaribu kumpa saa mwenzake., lakini kabla hata ya kuipokea ile saa aliona ile saa ikirushwa mbali na mkono wake ukikoswa koswa na
sumu iliyorushwa na yule nyoka.Tofauti na nyoka wengine Yule alitumia sumu kumdhibiti adui yake kasha kummeza akiwa bado anauhai hivyo sumu ndiyo ilikuwa ikitumika sana katika mapambano yake.
‘’Puuuh…..’’Ni mlio uliosikika baada ya joka lile kuelemewa ma mkuki mmoja uliokuwa na sumu kali ulipita karibu kabisa na kinywa chake.
‘’Poleni jamani kwa hiyo hamuoni kabisa?’’Aliongea Yule aliyeurusha ule mkuki akimsogelea Yule myoka mkubwa kabisa amabaye akipita sehemu ni kama gari lilikuwa limepita.
‘’Ndiyo lakini si mbaya umasikini kwa heri’’Aliongea mmoja kati ya wawili waliokuwa wamepoteza uwezo wa kuona akijikuna karibu kabisa na jicho lake.
‘’Bado kazi kubwa sana kumchuna ngozi yake ya tumbo na kupita nayo hadi kufika Ukerewe kwa mtaalamu’’Aliongea mwingine huku lafudhi yake ya kihehe ikishindwa kujificha.
‘’Harafu yure ariyerara pale ni nai’’Aliongea Mwita ambaye alikuwa ni kama kiongozi wao.
‘’Sasa we Mkurya unaniuliza mimi wakati sioni si utani huu?’’Alisikika kijana mwingine aliyeonekana ni kabila watani na wakurya ambaye licha ya kupoteza uwezo wake wa kuona furaha yake ya kuukwepa umasikini ilimfanya asijute kabisa kupatwa na tatizo lile.
‘’Ngoja tukamwone aliinuka Mwita akiwaacha wenzake wakiendelea kumchuna Yule nyoka ngozi yake ya tumboni.
Lakini kabla hata ya kumfikia Yule binti mvua kubwa ilianza kunyesha eneo lile walilokuwa na hata walipojaribu kutoka kuna nguvu ya ajabu iliwazuia kufanya hivyo.
‘’Haya maajabu mvua gani ituzunguke sisi pekee?’’Alisikika kijana mwingine akiacha kufanya kazi ya kumchuna Yule nyoka.
‘’Jamani huyu nyoka ana maajabu tuna upofu halafu anatuletea mvua ya namna hii’’Aliongea mmoja wa wale vijana waliokuwa wamepoteza uwezo wa kuona.
‘’Ila mtaalam alitueleza hatari ya huyu nyoka’’Alisikika kijana mwingine aliyekuwa akiendelea kuhangaika kuchuna ngozi ya Yule nyoka licha mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha huku
miale ya radi ikionekana katika giza lililokuwa likiongezeka kadiri muda ulivyosonga mbele.
‘’Arisema kuwa joka hiri ni Mungu wa makabira ya huko Bunjumbula’’Mwita naye aliongeza wakati huo alikuwa amefanikiwa kutoka kwenye eneo lile palipokuwa pana mvua na kumfikia Yule mtoto ambaye baada ya kumgeuza geuza aligundua kuwa alikuwa na uhai.
Swali alilojiuliza ni kivipi mtoto Yule alifika pale msituni,na je kuna uhusiano wowote kati ya Yule nyoka na mtoto na maswali mengine mengi yaliyokosa majibu sahihi.Baadaye
alimwinua na kumpelekea chakula cha akiba walichokuwa nacho na kuanza kumlisha,Delphine alijitahidi kula huku Mwita akiwa na hamu ya kumuuliza juu ya sababu ya yeye kuwa pale.Lakini hata baada ya kushiba na kupumzika siku ule hakufanikiwa kuongea naye kwani hawakuelewana lugha kwani licha ya kuwahi kukisikia Kiswahili Kiswahili alichokiongea Mwita kilimchanganya na kumtisha hasa mtindo wake wa kumkazia macho kila alipoongea ulisababisha akose kabisa kumwelewa.
Wakati hayo yakiendelea wale vijana wengine waliokuwa wametingwa na kumchuna Yule nyoka walikuwa wakihangaika kutoka kwenye lile eneo bila mafanikio yoyote.Mvua kali
iliyokuwa ikinyesha kuzunguka eneo walilokuwa iliwafanya hata baadhi kuachana na kazi ya kumchuna Yule nyoka na kuhangaika kutoka pale.Lakini mmoja wao alizidi kuichuna na
kuitengeneza vizuri ile ngozi ya nyoka ambayo mganga wao aliwaeleza kuwa wakiipeleka basi wangetengenezewa dawa ya kupata utajiri.
Umasikini ni kitu ambacho kijana Henrick Mbawala kutoka Mbinga alikichukia kuliko kitu chochote duniani, ambaye harakati zake za kutafuta maisha zilimkutanisha na kijana
Mwita katika machimbo ya dhahabu ya Masuguru kabla ya kwenda Geita ambako walikutana na wenzao ambao juhudi zao za kuukwepa umasikini zikiishia kwa Mganga mmoja wa
jadi ambaye aliwataka wampelekee ngozi ya tumboni ya nyoka hatari aliyepatikana katika msitu uliokuwa kati ya Rwanda na Burundi upande wa mashariki.Chuki dhidi ya umasikini na tamaa za kupata mali ziliwafanya vijana wale kupanga safari kwa takribani mwezi mmoja kabla na kuelekea Kigoma mwishowe walifika msituni hapo. Mvua ya ajabu iliyoendelea kunyesha pale ni kama ilimwongezea nguvu kijana Henrick na kutoijali kabisa kama wenzake walivyofanya.Alikumbuka maneno ya mganga wake kuwa walitakiwa kuziweka roho zao rehani ili kufanikisha zoezi lile.
‘’We Mngoni pesa itakuua wewe yaani hiyo mvua huiogopi kabisa’’Aliongea kijana mwingine kutoka Iringa baada ya kufanikiwa kutoka pale mvua ilipokuwa ikinyesha , ambaye kila mara alikuwa akitaniana na Henrick na kujivunia utani wao ambao mara nyingi ulionekana kuwashangaza waliowasikia na kuwatazama wakifikiri wangeweza hata kupigana.
‘’Kama umekuja kufanya utafiti ugopa mvua utaletewa turubai la Umoja wa Mataifa kuikwepa mvua mie nimekuja kutafuta huku baba yangu ni mcheza Mganda huko Ndumbi anategemea nimpelekee kaptura yake nyeupeee na kilo ya nyama kila jumamosi ,we wajivunia kwenu mnakula mbwa machungu ya pori mnaaita sijui mnafu na mzee wako anaogopa kukukaripia usije kujinyonga’’Alitania Henrick na kuwafanya wenzake wacheke hali iliyomshtua na kumwogofya Yule binti.
‘’Jamani nimeukumbua ughali macho yeyewe hayaoni’’Alinun g’unika kijana mmoja wa Kisukuma wakati huo Henrick alikuwa ameshamaliza kazi ya kumchuna Yule nyoka ngozi
iliyohitajika lakini kazi ilikuwa kutoka nayo eneo alilokuwepo. Alitumia zaidi ya nusu saa huku giza likiwa limeingia Kurunzi walizokuwa nazo wenzake wakimmulikia hazikumsaidia kuona
chochote hadi alipokanyaga mwiba wa lile joka kwa bahati mbaya na kuanguka chini kama mzigo akiangukia kiu kilichokuwa kikitoa harufu kali na kumwingia usoni mwake akianza kubabuka ngozi.
‘’He! Ngozi hii hapa ila huyu mngoni mbona haonekani?’’Ili sikika sauti iliyojaa utanio bila kujua kilichompata mwenzao ,
Mwita aliichukua ile ngozi na kuanza kuondoka hukua kiwa amemshika mkono Yule binti ambaye moyo wake ulimtuma kumsaidia na kwenda kumlea na familia yake.
‘’Mungu wangu jamani Henrick Yule anayeyuka ‘’Aliongea Yule kijana kutoka Iringa akiangalia mwili wa Mtani wake ukiyeyuka kutokana na nyongo ya Yule nyoka iliyokuwa kali.
‘’Twende wewe urizani aliposema sadaka arimaanisha nini huyo sadaka hujui Tumemwua Mungu wa watu?’’Sauti ya kutisha ya Mwita iliwafumbua macho kuwa Henrick alikufa
kama sadaka wapate kupata ile ngozi.
Kama msafara wa watumwa, watu watano walikuwa wakipita chini ya miti mirefu ya msitu ule huku wakiwa na mizigo kichwani na kamba moja ikiunganisha viuno vyao ili
kuwasaidia waliopoteza uoni wao kutokana na sumu ya nyoka.Walijua uelekeo wao ulikuwa sahihi kuokana na miti waliyoiona mchana huku Mwita akionekana kama mwenyeji wa ule msitu kwani kila mara alikuwa akiwakumbusha wenzake kuwa sehemu Fulani walipita mchana wa siku ile.
Baada ya mwendo mrefu miguu ya binti Yule ilianza kulegea na hatimaye kupoteza nguvu kabisa na kujikuta akikaa chini kama mzigo,kumbukumbu za vifo vya ndugu zake asubuhi ya
siku ile huku yeye kiherehere cha kuangalia choo kila aamkapo kikimkwepesha na kifo kile zilipita haraka haraka kichwani mwake naye akifumba macho tayari kwa kuwafuata wazazi wake na ndugu zake kwa kufa kwani aliamini kuwa kifo kilikuwa kimemfuata kila alipoenda licha ya muda tuu kuchelewa yeye kufa.
‘’Jamani ngoja nisaidie huu mzigo mie nimbebe huyu mtoto’’Aliongea Mwita akimtwisha ile ngozi mwenzake na kumnyanyua Yule binti safari ikianza tena.Huku yote yakiendelea akili ya Yule binti ilishindwa kuamini kabisa kama wale watu walikuwa wema kwani hakufanikiwa kuwaelewa kama walikuwa watu wa wapi japo lugha waliyoongea aliifananisha na lugha iliyoongelewa na watu kutoka nchini Kongo na Tanzania akielewa baadhi ya maneno ambayo hayakumsaidia kuwaelewa wale watu vyema.
‘’Tutaweka kambi hapa halafu kesho tutaendelea na safari yetu’’Mwita alitoa amri ambayo ilifuatwa na wote waliifuta na kuwekka mizigo yao chini.Licha ya kunyeshewa na mvua na kupata baridi waliogopa kuwasha moto kwani moja ya sharti walilopewa lilikuwa ni kutowasha moto ndani ya msitu kwani kwa kufanya hivyo mambo makubwa yangetokea na kushindwa kufanikisha kilichowapeleka huko. Walikula viazi vitamu walivyovibeba wakishushia kwa maji chakula ambacho binti wliyemwokota ilimuia vigumu kuvila lakini kutokana na njaa aliyokuwa nayo ilimbidi kujilazimisha kula.Sehemu yakulala iliandaliwa na wakajipanga na kulala huku Yule mtoto akiwekwa katikati kabisa. Asubuhi ya siku ya pili iliwakuta lakini walijikuta wapo pale pale walipopambana na lile joka na kuliua huku ile ngozi ikiwa imerudi kwenye mwili wa lile joka ambalo lilikuwa liihanaika kujiinua.Mwili wa Henrick haukuonekana zaidi ya kiatu chake kioja kilichokuwa na kipande cha mguu wake wa kushoto.
‘’Jamani hali mbaya likipona tumekwisha’’aliongea mmoja wa wale vijana waliopoteza uwezo wa kuona na kuwafanya wenzao wajue kuwa walipona macho yao.
‘’Kwa nini we kipofu’’sauti ya matani ilimtoka kijana mwingine ambaye naye alipatwa na tatizo jana yake.
‘’Kipofu wewe mie mzima kabisa naliona joka likijiviriga vema kutufuata’’Alimjibu na kushika vitu alivyoona vya lazima
 kukimbia navyo.
‘’Tuondoke hapa si sarama’’Sauti ya kukwaruza ya Mwita ilisikika akimwinua Yule binti na kuanza kuondoka naye.
‘’Sauti ya kilio kutoka kwa Yule msichana baada ya kuliona joka lile la ajabu ililifanya lile joka kuanza kuvimba kwa hasira tayari kwa mapambano wakati huo mbele yake kulikuwa na Mwita na Yule binti pekee ambapo wale wengine walikuwa wameshafika mbali. Mwita hakuwa na chakufanya zaidi ya kujaribu bahati yake kwa kutaka kukimbia na Yule binti lakini kabla hata ya kumaliza mita tatu alijikuta akibwagwa chini na kujikuta alimwachia Yule mtoto kutokana na sumu iliyotemwa na lile joka.
‘’Hesuuuu hesuuu hesuuu uleembu’’Sauti iliyopangiliwa ilisikika na kumfanya Mwita ageuke na kuangalia ilikotokea ,hakuamini alichokiona na kujikuta akitetemeka.
Lile joka lilitulia na wale watu waliliinamia huku wakiongea maneno Fulani ambayo bila shaka ilikuwa ni ibada fulani.
Baada ya kama dakika ishirini kitendo kingine kilifuata ambako ng’ombe wawili waliokuwa wamefungwa jirani walichinjwa wakati huo Mwita alikuwa ameganda pale chini akishuhudia yale mambo lakini hakuweza hata kusogeza kidole chake huku Yule mtoto akiwa kama hana fahamu kutokana na mwonekano wake. Hatimaye ibada ile iliisha na mmoja kati ya wale watu alimsogelea Mwita na kumwamuru kwa ishara kuwa aondoke kitu kilichofanywa kwa haraka sana akimbeba Yule mtoto na kuanza safari ya kurudi Tanzania.Safari iliyojaa uoga ilichukua zaidi ya masaa sita hadi walipofika kando ya ziwa Tanganyika ambako kama bahati kwao walikutana na boti iliyokuwa ikijiandaa kuondoka kuelekea Kigoma na kama bahati alikutana na wale wenzake waliokimbia kule porini.
‘’Mnyalu yuko wapi?’’Lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa Mwita mara baada ya kuwachunguza wenzake.
‘’Hatujaonana naye tulidhani mpo wote’’alijibu kijana mwingine akimwangalia Yule mtoto kwa huruma kwani alionekana amelegea sana.
‘’Mhh kweli tumeshindwa’’sauti nyingine ilisikika kuitoka kwa kijana mwingine ,wakati huo boti lilikuwa likiondoka.
Safari iliyochukua siku tatu iliishia mbele ya kinyumba Fulani kisiwani Ukerewe ambacho mwonekano wake kwa mbali ulionekana kuwashtua waliokuwa wakielekea pale.Watu wengi walionekana kukaa kwa makundi makundi kila mtu akiwa ana cha kuongea.
‘’Hii ni ajabu nyoka mkubwa vile kutokea majini na kummeza mtu si hatari hii’’Ilisikika sauti ya mmoja wa watu waliokaa karibu kabisa na waliposimama akina Mwita.
‘’Tatizo …’’alinong’ona Mwita na kuwafanya wale wenzake warudi nyuma na kujadiliana kidogo kasha kuanza safari ya kuelekea sehemu nyingine ambako walilala na hatimaye kuvunja rasmi kundi lao huku kila mtu akipanga kufanya kitu kingine cha kujikibu maisha yake.Mwita akiwa na Delphine
walianza safari ya kuelekea kwao Mugumu ambako naye aliona ni sehemu sahihi ya yeye kwenda kuishi baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kutafuta riziki.
Hali ya Delphine kiafya ilidhoofu kutokana na siku zile za mateso na maumivu makali huku kumbukumbu za vifo vya wazazi wake zikijirudia kichwani na kumpa maumivu makali,hali iliyompelekea kuumwa sana mara tuu walivyofika Mugumu.
Lakini kama hiyo haitoshi Delphine alikutana na mapokezi hasi si tuu kutoka kwa wazazi wa Mwita bali hata kwa watoto wenzake ambao walimwona kama kituko Fulani kutokana na sura yake ya Kinyarwanda ambayo haikujificha licha ya kuwa na umri mdogo wa miaka mitano tuu.Kwa waliobahatika kujua alikotokea ,kuna waliomwita jini,mkimbizi ,mtoto wa nyoka ili mradi tuu kumnyanyasa.
Hakuwa na jinsi zaidi ya kuvumilia kwani hakujua pa kukimbilia wala hakumwona wa kumweleza matatizo yaliyomkuta zaidi ya Mwita ambaye shughuli zake zilimtenganisha sana na Delphine.Alitamani aelewe lugha ya wenyeji wake walau ampate rafiki wa kumfariji lakini kila aliyemwona alijitenga naye huku sauti za vicheko vya kebehi vikisikika kutoka kwa kila aliyemwona.
Siku ,wiki miezi hatimaye miaka ikapita huku Delphine akiilelewa lugha ya wenyeji na kuwa miongoni mwa wanawali wa pale Mugumu ubaguzi juu yake ukafutika na hakuna aliyekumbuka tena kama ni mtoto wa kuokotwa porini .Vijana kama ilivyokuwa ada walianza kumsimamisha njiani iwe alipoenda kisimani ama porini kukusanya kuni yote ni kutaka kujaribu bahati ya kuonja tunda ya Yule binti wa Kinyarwanda aliyemvutia kila aliyemwona hasa kwa akicheka kwani mwanya wake ulizidisha uzuri wake ukiachana na uso wke mrefu ulioonekana kama ni wa kuchorwa machoni pa wengi.
Licha ya kuwa na ujirani na ukaribu na familia ya mwita ambaye kwa umri aliokuwa nao hakuwa na mtoto wala mke zaidi ya watoto wa kaka na dada zake waliomwita baba mdogo ama mjomba Delphine alikuwa na urafiki wa karibu sana na bibi mmoja ambaye licha ya kujulikana kama mkunga pia alikuwa ni ngariba aliyehusika na ukeketaji wa wasichana wa kabila lile. Ukaribu wao uliwachanganya wengi na hata kumtisha Mwita lakini mara nyingi alipomuuliza alimjibu kuwa anajifunza kuwa mkunga na Yule bibi alisisitiza hilo.
Lakini akiwa hajui lolote kuhusu ukeketaji siku moja akiwa katika kuandaa vifaa vya ukeketaji bila kujua akiamini ni vya ukunga Yule bibi anamtaka aingie bandani kwani kuna kitu cha muhimu kilipangwa kufanyika.
‘’Ni nini hicho bibi?’’aliuliza Delphine akionekana kushangazwa na wingi wa watu waliokujwa wakiongezeka hasa wanawake na wasichana wa umri wake.
‘’Uende ndani leo nakuachia rasmi kasi yangu ya kusalisha ‘’alijibu Yule bibi na kutangulia ndani , huku akiamini kuwa Delphine angemfuata .Tofauti na alivyodhani Delphine alizunguka nyuma ya kibanda kile akijiamini akipishana na watu kadhaa kabla ya kuanza kukimbia kuelekea shambani ambako aliamini lazima angemkuta Mwita na kama alivyotegemea alimkuta akinywa maziwa baada ya kulima kidogo.
‘’Nini wewe mbona unanishtua’’Lilikuwa ni swali la kwanza la Mwita baada tuu ya kumwona Delphine kwani ujio wake haukuwa wa kawaida.
‘’Sijui ila sipo salama’’alijibu Delphine akiangalia alikotoka ambako aliona kundi la wanawake wakielekea upande walikokuwa.
‘’Nenda kajifiche pale kichakani ,nimeshaelewa’’Alielekeza Mwita akijifanya anaendelea kunywa maziwa yake.
‘’We Mwita hujamwona Dela huku?’’aliuliza mama mmoja akionekana mwenye hasira.
‘’Sijamwona si yupo kwa bibi?’’alijibu kwa swali hali iliyozidi kuwaudhi wale wanawake.
‘’Tumetoka huko na katukimbia si ulisema unataka kuoa wewe utamwoa mwanamke ambaye hajasafishwa?’’Swali linguine lilimtoka Yule mama ambaye alihisi kuwa Mwita alijua aliko Delphine na aliamua kumficha.
‘’Si lazima kuoa mwanamke aliyesafishwa’’Sauti nzito ya Mwita ilisikika akionekana kukerwa na utaratibu ule huku akisahau kama Delphine alisikia kile alichokiongea.
‘’Anataka kunioa mimi? Kusafishwa? Kivipi? Mhhh naondoka ‘’aliwaza Delphine pale kichakani na kuamua kunyata akielekea porini zaidi akipita mashamba kadhaa ambayo yalikuwa ni kama yamesahaulika na wamiliki wao kutokana na nyasi zilivyokuwa zimesonga mazao.
Aliamua kukimbia kijiji kile kwani licha ya kusaidiwa na kuokolewa na Yule mtu hakufukiria kuolewa naye ,alimchukulia kama baba yake sasa kusikia suala la kuolewa naye kulimfanya aamue jambo moja tuu kukimbia na kutorudi tena Mugumu.
Kukimbia alikimbia tena kukimbia haswa na hata kama kungekuwa na mashindano angejizolea medali katika kila mbio ziwe fupi au ndefu lakini swali lilikuja kichwabni mwake angekimbia hadi wapi mpaka lini na alielekea wapi?
Nguvu za kuendelea mbele zilimwishia baada ya kukimbia kama kilometa ishirini hivi na kujikuta akikaa chini kama mzigo ulioangushwa huku simulizi za wanyama wakali kutoka mbugani Serengeti zikipita akilini mwake na kumfanya ainuke na kutaka kuanza safari.Lakini kabla ya kupiga hatua yoyote
kuna sauti ilimshtua na kumfanya aanze kutetemeka huku haja ndogo ikionekana kulowanisha gauni lake chakavu na ile sauti ikizidi kuongezeka kadri muda ulivyosonga mbele.
Gari dogo la kitalii lilionekana kwa mbali kilima na kumfanya Delphine apate tumaini jipya kwani akili yake ilimwaminisha ilikuwa ni sauti ya simba.Alijiweka vizuri kuomba msaada lakini alama ya michilizi ya mkojo uliotokana na hofu zilishindwa kufichika.
''We binti huogopi hapa porini?''aliuliza baba mmoja mara baada lile gari kusimama.
''Nina matatizo makubwa hapa nilipo baba yangu''Aliongea Delphine akiangalia garini ambako kulikuwa na watu wasabi huku dereva aliwa ni mwafrika pekee wengine wote wakiwa wazungu.
''Haya panda gari haraka tukupeleke sehemu salama''Alimrisha Yule baba akianza kuelekea garini.
Delphine alipanda kwenye lile gari la kitalii na kukaa kwenye moja ya siti zilizokuwa garini akiwaacha wale wengine wakiwa wamesimama wakiendelea kupiga picha wanyama na miti iliyoonekena kama muhimu sana kwao kwa wakati ule kwani ndicho kilichowapeleka kule porini.
Hakukuwa na mzungu hata mmoja aliyejishughulisha na Yule msichana zaidi ya kumsikiliza Yule mtu aliyekuwa akiwaeleza kuhusu mambo mbalimbali waliyoyaona kila walipopita.
Katikati ya mazungumzo hayo ambayo lugha ya kifaransa ikitawala , ambapo maneno machache tuu yalipata maana kwenye ubongo wa Delphine amabaye alishtuka kila alipowaona simba. Aliwaza kama angeendelea kutembea mle mbugani peke yake kama angefanikiwa kutoka salama kwenye
mbuga ile iliyokuwa kubwa sana Afrika Mashariki.
Taswira ya ndugu zake wakiuawa ilijirudia akilini mwake na kujikuta akitoa machozi na hakujua sababu iliyomfanya awakumbuke wakati ule kwani alikuwa hajawakumbuka kwa muda mrefu kufikia hatua ya kutoa machozi.Ilitokea mara chache sana kwake kuwalilia wazazi wake waliokuwa wamepoteza maisha miaka zaidi ya kumi iliyopita na kila alipofikia hatua hiyo alitamani kurudi tena Rwanda kulipiza kisasi juu ya mambo yaliyotokea kipindi kilichopita.
Aliwachukia sana watu wale akiapa kutowasamehe milele wale watu kwani aliamini hata kwa toba ipi wasingesamehewa hata na Mwenyezi Mungu.
Alijua wao ndio waliosababisha awe katika hali ile ya kukimbia kimbia , tena akiwakimbia wanadamu wenzake ambao kila mmoja hakuwa nania njema kwani wakati akikimbia kukeketwa anakutana na jambo jipya la kutaka kuolewa na mwanaume ambaye kwake alikuwa ni kama baba yake.Yote hayo yalitokana uhasama wa kikabila uliochochewa na siasa chafu nchini mwake, alitamani kuona siku watu wale wakiadhibiwa kwa mateso makali ambayo huenda yangekuwa ni pozo la moyo wake.
Gari la kijani aina ya LAND CLUISER lilisimama mbele ya jengo moja ambalo lilionekana ndiyo mwisho wa safari ya watu wale waliokuwa garini waliomtaka Delphine ashuke pamoja nao.
Walipofika ndani ya jengo lile waliletewa chakula huku Delphine akihimizwa na kila mmoja kula na baada ya kula alipewa mavazi ambayo alitakiwa kuyavaa baada ya kuoga kwani mavazi aliyotoka nayo kijijini yalikuwa kmachafu sana. Mavazi yale yalifanamna na mavazi waliyovaa wafanyakazi
waliokuwa wakifanya kazi ya upishi katika nyumba ile iliyokuwa ni hoteli ya kitalii, jambo lililomshangaza Delphine kwani awali aliamini kuwa ni watalii tuu sasa ilikuwaje wampe mavazi yaliyokuwa sare za wapishi wa iile hoteli ya kitalii.
''Unaitwa nani?''Lilikuwa ni swali la kwanza alililoulizwa Delphine mara tuu alipoketi kitini baada ya kuoga na kubadili zile nguo zilizomfanya aonekane kama mmoja wa wapishi wa ile Hoteli.
''Delphine Mwita''alijibu huku akionekana kuwa na uoga wa ajabu kwani alijikuta akiamua kuwadanganya wale watu ili apate msaada.
''Umetokea wapi na kwa nini ulikuwa pale porini?''Aliuliza maswali mfulizo Yule mtu huku akionekana kuwasikiliza sana na kuwaelekeza wale watalii wa kizungu .
''Nimetokea Mugumu huko walitaka wanikekete na kunioa katika umri huu mimi yatima jamani"Aliongea Yule binti akitoa kilio cha hisia kilichowafanya wale watu wamhurumie sana
kabla hata ya kuelekezwa maana ya alichokiongea na Yule aliyeonekana kama mkalimani wao.
Baada na maelezo mengi yaliyojaa uongo uliokuwa wakiwango cha juu kufikia hatua ya kumtoa machozi mama mmoja ambaye alionekana naye kama ana mamlaka kwenye ile hoteli kutoa machozi akimtaka amshukuru sana Mungu kwa kumwepusha na mauti akiwa mbugani , mbuga ambayo ilikuwa na wanyama wengi hatari kwa maisha ya wanadamu hata wanyama wenzao.
Baadaye alitakiwa kulala na mmoja wa wapishi wa hoteli ile huku wakiahidi kumpa msaada alioumba ambao ulikuwa ni kuwa mbali juu ya watu wale waliotaka kumfanyia mambo ambayo hakupenda kabisa yatokee kwake.
Uchovu na kilio cha jioni ile vilimfanya Delphine apate usingizi mapema sana mara tuu alipojitupa kitandani akimwacha mwenzake aliyetakiwa kulala naye akihanagaika hangaika mle ndani na pilika zilizokuwa hazina maana, mara akashike chanuo mara ajaribu gauni mara akwangue kucha za miguu ili mradi tuu hatulii.Usiku wa manane Delphine alishtuka kutoka usingizini baada ya kuota ndoto Fulani ya kutisha ambayo Marehemu Mama yake alimtokea ndotoni akimwambia kuwa
wale watu aliokuwa nao hawakuwa wema hata kidogo ajitahidi kuondoka pale mapema sana kabla mambo mabaya hayajamtokea.
Alipoangalia Pembeni yake ambapo Yule mwanamke aliyeambiwa angelela naye hakuona chochote zaidi ya shuka lililokuwa kimekunjwa kana kwamba kakukuwa na mtu aliyelala pale. Aliogopa, hasa kutokana na ile ndoto ambayo ilimhusisha mtu aliyefariki miaka mingi iliyopita , tena hakuwahi kumwota hata siku moja tangu alipouawa kinyama na wale watu.Alianza kupata hofu juu ya wale watu ambao hakujua walikuwa na kazi gani japo walionekana kama watalii lakini walikuwa na mamlaka sana tofauti na walivyokuwa watalii wengine waliokuwa pale hotelini. Akiwa katika kutafakari juu ya mambo hayo alishtushwa na sauti ya hatua zilizokuwa zikionekana zikielekea katika chumba kile alichokuwa amelala, wazo la haraka lilimjia akijamini kuwa alikuwa ni Yule rafiki yake waliopangwa kulala pamoja.
Bila kutarajia alijikuta anachukua uamzi wa kusimama na kujificha nyuma ya kabati la nguo lililokuwa mle ndani , na Yule mtu alipoingia alikuwa ni mtu ambaye alimfanya ashindwe kuelewa sababu iliyompeleka pale ndani muda ule. Alikuwa ni mmoja wa wale watu aliosafiri nao wakitokea
Mbugani akiwa ndiye Dereva wao , ambaye moja kwa moja alienda kitandani kujilaza na kujifunika ile shuka iliyokuwa imekunjwa pale pembeni ya alipolala Delphine . Akiwa nyuma ya ile kabati ndogo Delphine alitetemeka sana baada ya kuona Yule mtu akiamka na kuanza kuangaza huku na huko mle ndani kabla ya kutoka nje ya kile chumba.Yule mtu alirudi muda mfupi baadaye akionekana bado akitafuta kitu mle ndani jambo ambalo Delphine alilinganisha na ndoto aliyokuwa ameiota. Sala nyingi zilipita kichwani mwa Delphine kwani aliamini kuna jambo baya lilikuwa mbele yake kwani mwonekano wa Yule mtu haukuonekana kuwa na jema lolote kwake.Mapigo way moyo wa Delphine yaliongezeka baada ya Yule mtu kumsogelea alipokuwa amejificha na bila kuongea chochote alimnyanyua kwa nguvu na kumtupia kitandani na kumvua nguo zake akitaka kumbaka jambo lililopingwa na Delphine ambaye alijitahidi kwa nguvu zake nyingi kujinasua kutoka katika mikono ya mwanaume Yule aliyedhamiria kumtendea kitendo cha kinyama akiendeleza ,matukio ya ajabu nay a kikatili kuyashuduia kwa macho yake.
Baada ya purukushani za hapa na pale hatimaye Yule mwanaume alifanikiwa kumbaka Delphine akimsababishia maumivu makali na majeraha makubwa sehemu zake za siri hali iliyomfanya atoe kilio cha maumivu.Hakujua sababu ya mambo yale katika maisha yake kuanzia kuuawa kwa wazazi wake na ndugu zake hadi alipokimbia kukeketwa kule kwa akina Mwita kabla ya kujua kuwa alikuwa katika mipango ya ndoa ya Mwita .
Akiwa katika mawazo yale watu wengine wawili waliingia mle chumbani ambapo kutokana na lugha waliyokuwa wakiitumia aligundua kuwa hawakuwa ni waswahili kama aliyetoka kumsababishia maumivu muda mfupi uliopita .Walionekana kana kwamba hawakuwa na baya kwake kwani walimwangalia sehemu alizojeruhiwa na kuzifuta na shuka walilochukua pale kitandani.
Akiwa na aibu kubwa usoni kutokana na kufanyiwa usafi ule na watu wa jinsi tofauti na yake ,hasira moyoni mwake iliongezeka baada ya kumwona mbaya wake akiwa mbele yake bila kuchuliwa hatua yoyote.
Nini kilifuata?
TUKUTANE KESHO


0 comments:

Post a Comment