Wednesday, 9 March 2016

RIWAYA;MUUAJI WA FACEBOOK; MWANZO


MUUAJI WA FACEBOOK

MTUNZI: MORINGE JONAS MHAGAMA

SEHEMU YA KWANZA
Nikiwa na mawazo mengi baada ya kusikia kuwa ni lazima kwenda jeshini mara tuu baada ya kufanya mitihani yangu ya kumaliza kidato cha sita,niliamua kufanya kitu kimoja kujisahaulisha na habari ile.Niliingia chumbani kwangu na 
kuwasha kompyuta ndogo na kujiunga na mtandao wa kijamii wa facebook nilikumbuka kuwa nilijiunga awali lakini nilishasahau neno siri kwani miaka miwili niliyotumia shuleni sikujishughulisha kabisa na mambo ya mitandao ya kijamii kwanza kwa sababu sikuwa na simu shuleni na kipindi cha likizo nilikuwa ninahangaika na kujisomea kwani iliaminika kwa wengi ukisoma sayansi lazima usome sana ili ufaulu.Baada ya kufanikiwa kujisajili niliamua kutafuta marafiki huku nikianza na marafiki zangu wa shuleni ambao walikuwa wananitambia sana juu ya mtandao huo.Kitu cha pili kilikuwa ni kuchukua picha zilizokuwemo kwenye kompyuta na kuziweka kwenye akaunti yangu ya facebook huku nikiwa nashangilia kila nionapo watu wananisifia hata kwa picha ambazo hata mimi mwenyewe nilijua si za kuvutia.
Nikwa naendelea kushangaa maajabu ya watu wale waliokuwa wakinisifia kwa kila kitu niliona ujumbe ukiingia kwenye simu yangu hali iliyonifanya niachanae na kompyuta.
''Mambo?'' ulisema ule ujumbe ambao sikumjua mtumaji maana ilikuwa namba ngeni.
''Poa tuu mwenzangu nani?''Niliuliza nikijaribu kukisia mtumaji wa ujumbe ule.
''Mariam'' ndilo jina lililosomeka simuni kwangu
''Mariam wa wapi?''Niliuliza sasa nilijaribu kuwafikiria akina Mariam niliwafahamu lakini sikukumbuka kama kulikuwa na Mariam ambaye namba yake sikuwa nayo.
''Mie Mariam wa facebook'' jibu lile lilinishitua Mariam wa facebook ipi mbona sikumjua na namba yangu aliipataje nilifikiria huenda akawa ni mtu aliyekuwa ananifahamu na aliamua tuu kunitania ,nilikumbuka utani wetu tuliokuwa tukifanyiana tulipokuwa sekondari shule ambayo ilikuwa ya wavulana pekee namimi nilikuwa nimezoea maisha yale kwani tangu nisome shule ya msingi na wasichana sikuwahi kusoma na wasichana hadi namaliza kidato cha sita.Hata nilivyokutana nao huko twisheni nilikuwa sina mazoea nao hali iliyowafanya wengi waniite Bruda wakinifananisha na wale watumishi wa kiroma.
Wakati nayawaza hayo mara simu yangu iliita ilikuw anamba ngeni lakini haikufanana na ya awali ,niliipokea na kuisikiliza bila ya kuongea chochote hadi niliposikia sauti ya upande wa pili.
''Hallo Magnas mimi Mariam wa facebook nimetumia namba nyingine kwani ina kifurushi'' Alijieleza yule dada ambaye alikuwa na sauti nyororo kama watangazaji wa vipindi vya mahaba redioni.
''Samahani namba yangu amekupa nani?'' Niliuliza nikiwa na hofu.
''Nimeichukua facebook'' Aliongea kwa kujiamini 
''Facebook kwenyewe najiunga sahizi wewe umeipataje?'' Niliuliza huku wazo la kuwa huenda akawa jini liliniingia na kuamua kuikata simu na kuizima.
Hamu ya kuendelea na Facebook ilinisha niizima kompyuta na kufungulia redio huku nikiwaza juu ya yule Mariam wa facebook.Simu yangu iliita tena ilipojua kuwa ni namba ile ile niliizima simu na kulala kitandani nikiliangalia dari safi la kile chumba,nilikuwa naendelea kujiuliza maswali mengi juu ya Mariam yule aliyenipigia simu sikujua kilichomfanya anipigie simu lakini wazo langu ni jinsi alivyoipata namba yangu sikuamini kam akujiunga tuu na mtandao ule basi kila mtu anakuwa na namba yako.Niliwaza sababu ya yeye kupiga simu na sikuijua nikaanza kujiona mjinga kwa kukata simu bila kumsikiliza yule mtu wazo ambalo lilinifanya niiwashe simu yangu na kutaka kumtafuta lakini kabla sijaipiga ile namba uliingia ujumbe mfupi wa maneno ulikuwa umetoka kwenye namba ambayo nayo sikuijua.Niliposoma nilijiona mpumbavu kwa nilichokifanya kwani ulieleza kuwa nilivyojisajili kwa kuingiza namba yangu basi marafiki zangu wataiona ile namba yangu na yeye aliiona,Lakini nilipojaribu kukumbuka kam anilikuwa nimempata rakini wa jina lile sikukumbuka kabisa.Pia nilikumbuka kuwa ningewaomba urafiki marafiki wa kiume tuu sasa nilishangaa alikuwaje rafiki yangu ?swali hilo lilinipelekea kuiwasha tena kompyuta na kuingia facebook na moja kwa moja niliangalia orodha ya marafiki zangu ambao hata hawakufika ishirini ajabu sikuliona jina la Mariam,
Je,ni nini kiliendelea?
Huyo Mariam ni nani?
________
Niliamua kumpigia simu lakini badala ya kupokelewa simu ile ilikatwa hali iliyonishtua kidogo wakati nafikiria hayo simu yangu iliita tena namba ambayo nilitoka kuipiga.
‘’Hallo mambo Magnas’’ Ilisikika sauti kutoka upande wa pili
‘’Poa kwa mara ya pili,samahani mbona sina rafiki yangu mwenye jina lako facebook?’’.Niliuliza huku nikiwa na hamu ya kujua nitakachojibiwa na Yule mtu.
‘’Natumia jina la Diane xweety gal’’Alinipa jina ambalo hata sikuliona kwenye orodha ya marafiki zangu jambo ambalo lilizidi kunipa hofu juu ya Yule mwanamke.
‘’Mbona sijaliona?’’ Niliuliza nikiangalia kwenye kompyuta yangu kama kulikuwa na rafiki aliyeongezeka mwenye jina lile.
‘’Lipo we angalia tuu mbona unaonekana mwoga hivyo?’’ Aliongea akicheka akinifanya namimi kulazimisha kicheko ambacho niliona kabisa hakiji.

‘’Ngoja niangalie ndugu yangu’’Niliongea nikifungua tena kwenye orodha ya marafiki zangu nililiona jina lile .
‘’Sawa mie naisitisha simu yako halafu nitakuunganisha baada ya dakika tatu’’Ilisikika ile sauti nyororo ambayo kwa mara ya kwanza nilijiona navutiwa na sauti ya wanawake kwani licha ya kuitwa Bruda kwa kipindi kirefu nilijikuta Napata wazo la kukiuka misingi ya jina langu.
‘’Mhhh…mtu jini au malaika?’’ Nilijikuta natamka mara baada ya kukutana na jina lililosomeka Diane xweety gal ambalo liliambatanishwa na picha yake ambayo ilinifanya nisiamini kama ni yeye ama aliweka picha za kuzichukua mtandaoni.Lakini baada ya kuangalia picha zaidi niligundua kuwa ni yeye kwani zilionesha maeneo mbalimbali ya Tanzania na marafiki wenzake ambao bila shaka ni watanzania wenzake kiukweli alikuwa ni mwanamke aliyejaliwa sura na umbo zuri hadi nikimlinganisha na viumbe ambao wengi licha ya kutowaona tulipenda kuwasifia kuwa wana sura nzuri sana, Majini na Malaika .Nilikumbuka juu ya dakika tatu alizonipa nilipoiangalia simu yangu niliiona baado ikihesabu dakika.
‘’Hallo’’Nilijaribu kuongea ili nijue kama alikuwa hewani.
‘’Hallo siyo jini bhana ni malaika’’Aliongea akicheka jambo lillilonifanya niamini kuwa hakuisitisha simu zaidi ya kukaa kimya akinisikiliza.
‘’Kwa hiyo umesikia yote niliyoongea,ningekutukana ungenishtaki?’’Niliongea nikijichekesha huku nikiona aibu kwa kumsifia Yule mwanamke ambaye sikuwahi kumwona popote zaidi ya kusikia sauti yake.
‘’Hapana nilijua huwezi nitukana ndio maana niliamua kukusikiliza’’Aliongea akiiremba sauti yake kwa mbwembwe na madaha .
‘’Sawa ,nikuulize swali?’’Niliongea kwa sauti ambayo msikilizaji lazima angejua kuwa nilihitaji umakini.
‘’Uliza tuu Magnas’’Alijibu akinipa nafasi ya kuuliza swali langu.
‘’Huwa unampigia kila rafiki yako wa facebook?’’Niliuliza na kusubiri jibu
‘’Kwa nini umeuliza swali kama hilo kaka?’’Aliuliza akiendelea kulegeza sauti yake
‘’Kwa sababu ndiyo kwanza najiunga facebook nawewe unanipigia simu’’Niliuliza nikiangalia picha yake moja aliyopiga ufukweni akiwa na mtoto mdogo wa kiume.
‘’Wewe hujajua kwa nini?’’ Aliniuliza swali ambalo hata sikujua nimjibu nini.
‘’Sijajua kabisa ndiyo maana nimeuliza’’Nilijibu huku swali lingine nilikija kichwani kwangu kuhusu Yule mtoto ambaye kwa sura alinivutia sana pia na tabia yangu ya kupenda watoto wa umri ule.
‘’Utajua siku moja kakangu’’Alijibu na kukata simu,nilikumbuka swali langu juu ya Yule mtoto ambaye nilivutiwa naye,niliamua kumtumia ujumbe mfupi wa maandishi.
‘’Samahani nikuulize swali linguine?’’Nilisubiri jibu wakati huo nikiendelea kuzisoma taarifa zake ambapo aliandika kuwa amesoma shule ya sekondari Morogoro na chuo kikuu cha Ushirika kilichopo Moshi.Wakati naendelea kuangalia taarifa zake mara ujumbe uliingia.
‘’Uliza tuu samahani simu ilizima chaji ‘’Niliipata sababu ya simu yake kukatwa kwani nilihisi huenda maswali yangu yalimkwaza.
‘’Yule mtoto niliyemuona upo naye ufukweni ni wako?’’Macho yangu yalirudi kwenye kompyuta ambako ile picha ya Yule mtoto ilionekana kwa uzuri kabisa.
‘’Ni mdogo wangu wa mwisho’’Alijibu ujumbe ambao uliniongezea swali lingine.
‘’Kwani mpo wangapi kwenu?’’Wakati huo nilikuwa najaribu kusoma vitu mbalimbali ambavyo alikuwa ameviandika, sikuamini kwani alipenda sana kuandika masuala ya kidini na akifafanua mistari mbalimbali ya kwenye biblia.
‘’Tupo wawili tuu mimi na mdogo wangu’’Jibu hilo lilinifanya nione kama nadanganywa hasa kutokana na tofauti ya umri kati yao.
‘’Mhh yaani una ndugu yako mmoja tuu?’’Niliuliza swali ambalo sikuiona mantiki yake zaidi tuu ya kutaka ajieleze zaidi.
‘’Ndiyo kwani kuna ubaya wowote?’’Aliniuliza huku sikuwa na jibu lolote la maana kama swali langu lilivyokuwa.
‘’Hakuna ubaya wowote ndugu,mdogo wako nimempenda sana nataka awe rafiki yangu mwambie namsalimia’’Niliamua kubadili maada kwani nilijua kabisa naweza kusimulia mambo mengine ambayo sikutaka kuyajua kutoka kwa mwanamke Yule.
‘’Usijali nitamwambi nadhani atafurahi sana’’Nilijibiwa wakati huo nikiendelea kupekua pekua taarifa zake na marafiki zake.
‘’Sawa siku njema’’Niliaga na kuendelea kupitia pitia taarifa zake.
‘’Poa baadaye kakangu ,nimefurahi sana kuongea nawe’’Akili yangu ilihamia kwa binti Yule ambaye sikujua kabisa nia yake kubwa hadi akawasiliana namimi,sikumwona kama ni mtu mbaya kutoka na vile vitu alivyokuwa anaviandika huko facebook.Nilichukua simu na kumpigia rafiki yangu ambaye kwa habari za wanawake alikuwa humwambii kitu.
‘’Hallo Fred’’Niliongea nilipoona simu yangu imepokelewa
‘’Sema jembe langu’’Ilisikika sauti kutoka upande wa pili
‘’Hallo kuna demu Fulani kanitafuta facebook’’Nilimdokeza jambo hilo kwani nilijua lazima angedakia.
‘’Vipi umeamua kunilengeshea nini? Maana na ubruda wako unajifanya huna habari nao”Aliongea akinifanya nicheke kwa sauti ambayo nilihisi kusikika na mtu yeyote angepita pale nje.
‘’Hapana kuna dada mmoja anajiita Diane xweety gal amenipigia’’Nilimjibu nikisubiri jibu la Fred.
‘’We huyo una namba yake,mimi nimemtumia sana ujumbe facebook lakini hanijibu vipi una namba zake?’’Aliuliza huku nikijua kuwa Yule mwanamke hakunichanganya mimi pekee.
‘’Ndiyo ninayo nikupe?’’Niliuliza nikiangalia simu yangu nyingine ambayo nilipigiwa na Yule dada.
‘’Nipe bwana ila Yule msichana mara ajiite Mariam mara Joshua ili mradi tuu kutusumbua na vijimaneno vyake vya biblia’’
‘’Mhh kwa hiyo ni mcharuko sana ?’’Niliuliza huku nikijaribu kubashiri sababu ya kuwa na urafiki na Yule dada huenda alitumia hilo jina la Joshua nilimuomba urafiki nikidhani ni Joshua niliyesoma naye Kigonsera Sekondari.
‘’Yaani sijui nisemeje ila ni mzuri’’Alinijibu huku akiniacha kwenye fikra nyingi juu ya Yule dada.


‘’Sawa ngonja nikutumie’’Niliongea nikiituma ile namba .

‘’Poa nimeipata naona ujumbe umeingia hapa najua ni yenyewe’’Aliongea na kukata simu akinipa nafasi ya kuingia facebook kuongeza marafiki safari hii nilikuwa siangalii jinsi wala jina la mtu ilimradi tuu alionekana.Nilifanya kazi ile ka zaidi ya dakika ishirini ambapo nilikuwa na marafiki wasiozidi mia moja.Mara nilisikia simu yangu ikiita na nilipoangalia mpigaji alikuwa Fred nilibonyeza kitufe cha kijani na kusikiliza.

‘’Piga keleleeeee….’’Aliongea kwa fujo
‘’Kuna nini?’’Niliuliza huku nikijaribu kubashiri sababu ilyomfanya kufurahi vile, nilisahau kabisa habari za Mariam.
‘’Mtoto hajachomoa ,halafu anaonekana mambo safi kwao’’Aliongea akionekana kunichanganya.

‘’Nani huyo Fred?’’Nilibaki gizani nikiwa simjui mtu aliyemwongelea kwani ilikuwa kawaida kwake kupiga simu na kuniambia mipango yake ya wasichana ambayo ilikwenda vyema.
‘’Si Mariam mlokole si umenipa namba sasa hivi ‘’Aliongea huku bado akiwa na furaha nilikumbuka juu ya msichana aliyenipigia simu .
‘’Vipi ameshanaswa mtegoni?’’Niliuliza huku nikijua fika kwa furaha ile mambo yalikuwa yameshaisha.
‘’Wewe kwangu hakuna wa kunikwepa nilichotaka namba yake tuu, mara aniulize aliyenipa namba mara sijui hanijui lakini mwisho ameamua kupoa na kutulia kwa mwanaume hapa’’Alijigamba Fred hali iliyonipa wivu Fulani kwani mwanamke Yule awali alionekana kunichanganya kidogo nilijikuta najuta kumpa namba lakini niliamua kujifanya nimefurahishwa na ile taarifa.
‘’Poa bwana kuwa makini maana watoto wa siku hizi kila mtu atajifanya wa Masaki kumbe ni jirani yako wa Tandale’’Niliongea huku nikijifanya kumshauri.
‘’Wewe si umeona hata yale mapicha siyo ya matembele kila siku’’Aliongea akicheka hali iliyonifanya namimi nicheke.
‘’Hongera bwana mtukumbuke akina sisi kwa vizawadi’’Niliongea na kukata simu huku nikihisi nafsi yangu ikiwa na wivu juu y Fred kumpata kirahisi vile Yule msichana.Mwanzoni nilimpa ile namba nikiamini kuwa hatokubaliwa ila kitendo cha kubaliwa tena haraka vile hakikunifurahisha kabisa.Wazo la kwamba huenda Fred alijisifia tuu kuwa amekubaliwa huenda hata simu yake haikupokelewa lilipita kichwani mwa magnus kwani niliwahi nkusikia kuwa licha ya tabia yake ya kuwa na wanawake wengi lakini baadhi yao walimuumiza kichwa na mbinui zake zote hata za kuhonga ziliishia kugonga mwamba lakini akikusimulia utadhani huyo mwanamke ameshamweka ndani.
‘’Haiwezekani, huyu lazima awe wangu na anaonekana kama amenipenda’’Nilijikuta naongea kwa sauti ya ukakamavu nikisimama kukunja ngumi.Chuki juu ya Fred ilianza kujengeka nilimchukia yeye kwa tabia yake ya kutaka kila mwanamke mzuri awe wake.Niapa kupambana hadi mwisho ili nimmiliki Mariam maarufu kwa jina la ‘’Diane xweety gal’’.Nilichukua simu ile na kumpigia lakini nilikuta inatumika jambo ambalo lilinitia hasira likiniaminisha kuwa huenda alikuwa akiongea na Fred ambaye naye nilipompigia simu yake ilikuwa ikitumika.Nilijikuta Napata hasira na kuibamiza simu yangu pale kitandani na kutoka nje lakini kabla hata sijafika mlangoni ujumbe wa maandishi ulionekana kuingia kwenye simu yangu moja na niliporudi kuusoma uliniongezea hasira kwani alikuwa ni Fred.
‘’Kesho kanambia tukutane’’Ulisomeka ule ujumbe 
‘’wapi?’’ Niliuliza kwa kifupi na kuzima simu zangu zote na kuelekea nje ya nyumba ambako hapakuwa na yeyote kwani baba na mama walikuwa bado hawajarudi kutoka kazini kwao na ndugu zangu wakiwa shuleni kwani walikuwa kwenye shule za bweni.
Nikiwa pale nje niliwaza mambo mengi sana lakini wazo la kumpata msichana Yule lilijirudia akilini huku nafsi ikinituma kupambana kwa namna yoyote ile nimpate Mariam.
‘’Kwanza gari letu lilimpa umaarufu sana ndio maana anawapata kiurahisi na hiyo kesho lazima atadai nimpeleke nitamnyima gari’’Niliwaza pale nje huku chuki dhidi ya Fred ikizidi kukomaa kwa kasi ya ajabu sana.
‘’Hapati gari na namuwahi kwenda kwa huyo mwanamke lazima awe wangu labda afe usiku wa leo’’Nilijisemea kwa sauti ya chini huku chuki ikizidi kukua nafsini mwangu, niliusahau kabisa urafiki wetu ambao hata wazazi wetu waliuheshimu wakiamini hatungekuja kugombana hata siku moja.Nilikaa pale nje hadi wazazi wangu walivyorudi ndipo nilipoingia ndani ambako Yule hausigeli akiniangalia kwa uoga kwani nilikuwa ni kama nimemgunia kila mtu.
‘’Una tatizo gani Magnas?’’aliuliza baba wakati tunakula chakula
‘’Sina tatizo lolote’’Nilimjibu kwa kifupi nakuendelea kula
‘’Ana mawazo ya JKT huyo asijifanye kununa hapa bila sababu’’Mama aliongea huku akiwafanya wote waliokuwa pale mezani wacheke isipokuwa mimi ambaye bado nilikuwa nimekunja sura yangu.
‘’We kweli sio mzalendo badala ya kufurahia kwenda huko unatununia sisi?’’Aliongea baba huku akiendelea kucheka
‘’Na uzuri wenyewe wanasemaga lazima hakuna cha nani wala nani’’Aliongeza hausigeli ambaye muda wote alikuwa msikilizaji lakini alipoona mada ile imemfurahisha yeye na mabosi wake aliona atie neno.
‘’Nawewe Semeni unasema nini?’’Niliongea kwa hasira na kusima na kwenda kunawa mikono yangu na kuingia chumbani nikiwaacha wakila huku Semeni akionekana kupatwa na uoga.
‘’Achana naye huyo’’Nilimsikia mama akimwambia Semeni lakini sikujali na kuingia ndani. 
Nilipofika ndani niliwasha simu zangu na baada ya muda kidogo ujumbe ulianza kuingia kwa kasi mwingi ulikuwa ni kutoka kwa Fred ambao niliufuta bila hata kuusoma.Macho yangu yalitua kwenye ujumbe ambao ulikuwa na namba ngeni ambayo niligundua kwa namba yake ya mwishoni ni kama namba ya Mariam akili yangu ilikaa tayari kutaka kujua kilichokuwemo kwenye ule ujumbe.Niliufungu nilichokiona kilinifanya nipanue mdomo wangu kwa mshangao.
‘’Magnas nimetokea kukupenda,naomba kama una muda kesho tuonane’’Nilisoma ule ujumbe huku uso wangu ukipambwa na tabasamu na nilijiona mshindi wa vita ile bila hata kupambana.Niliamua kusoma ujumbe mwingine ulioingia kwa kasi kwenye simu yangu.
‘’Nimekuudhi Magnas? ni moyo wangu ndio unitumao kukupenda usinifikirie vibaya’’Ulisomeka ujumbe mwingine wakati nafikiria jinsi ya kumjibu simu yangu iliita na migaji alikuwa ni Yule nikiyekuwa nikisoma ujumbe wake .
‘’Halloo Magnas mbona ulinizimia simu?’’Alianza kuongea na kunitupia swali ambalo niliwaza haraka haraka jibu la kumridhisha.
‘’Samahani simu ilidondoka na imeharibika kabisa na hapa natumia simu ya mama’’Niliamua kudanganya.
‘’Jamani wangu pole sana,kwa hiyo wamrudishia?’’Alibadilisha sauti yake na kuilegeza kama ilivyokuwa kawaida yake.
‘’Siirudishi nimemwomba niitumie usiku wa leo’’Nilizidi kumdanganya wakati huo furaha ya kuambiwa nimependwa na msichana ambaye kwa wakati ule alikuwa ameuteka moyo wangu ikizidi kunifanya niwe mchangamfu,nilienda kufunga mlango wa chumbani kwangu huku nikiongea na kujilaza kitandani nikining’iniza miguu yangu ikigusa zulia la mle chumbani kwa shida.
‘’Waoh tutaongea usiku kucha wangu,au ulipanga kuonga na wifi yangu?’’Aliuliza akicheka

‘’Hayupo ndugu yangu tutaongea tuu hadi shemeji yangu akikupigia’’Niliamua kumtega kwa swali la kizushi ili tuu nijue kama kweli hakuwa na mpenzi mwingine na nihakikishe juu ya habari alizonipa Frank.

‘’Jamani Magnas ningekuwa na mtu ningekupigia usiku huu?’’ Alinijibu kwa hasira kidogo hali iliyonitisha na kunifanya niwe mpole ghafla.
‘’Jamani Mary hutaniwi?’’Niliongea kwa kubembeleza.
‘’Nawe hutaniwi? Namimi nilikuwa nakutania tuu wangu shemeji yako hayupo upo wewe’’Alongea kauli ambayo licha ya kumpenda lakini ilinitisha kwani nilijua aliamua kunitania kunipima tuu kama nina msimamo halafu anidharau.
‘’Mimi tena kuanzia lini?’’Nilijifanya kuuliza.
‘’Jamani inamaana hujasoma meseji zangu’’Aliongea kwa kulalamika wakati huo nilifikiria haraka haraka jibu la kumpa .
‘’Nimeziona lakini hatujakubaliana’’Niliamua kumwambia tuu ukweli.
‘’Ndio maana nimekupigia tukubaliane wangu’’Alizidi kulalamika.
‘’Siamini kwa uzuri ulionao kama utakuwa huna mwanaume au umeachika umeona uje kutulia kwangu?’’Niliuliza swali ambalo lilimfanya akae kimya kwa muda kidogo.
‘’Halloo,,, ‘’Nilijaribu kumshtua kama alikuwa hewani.
‘’Samahani nimeitwa na baba mara moja nitakupigia wangu’’Aliongea na kukata simu akinipa muda wa kuvua nguo na kubaki na nguo za kulalia pekee.Niliona mambo yale niliyoamua kujiingiza yananichanganya kwani kitendo cha kukata simu na kudai aliitwa na baba yake kiliniuma na wivu juu yake ulikuwa umeshaanza kunitesa.

Niliamua kupiga ile namba lakini iliita bila kupokelewa hali iliyonifanya niamini kweli alikuwa ameeitwa lakini nilipoamua kumpigia Fred simu yake ilionekana kutumika.Nilijipa moyo kuwa huenda alikuwa akiongea na wanawake wengine aliokuwa akiwadanganya kuwa aliwapenda lakini lengo lake lilikuwa ni kuwachezea tuu na kujisifia kwetu huku akiwaponda kwa uchafu,na kile alichopenda kukiita GOGO (najua wenye uzoefu na mambo hayo watanielewa) na mambo mengine mengi ilimradi tuu kuwashusha thamani.Lilikuwa ni jambo lililozoeleka kusikia mwanamke ambaye alimsifia akimpa sifa za Majini na Malaika kabla ya kuwa naye akimwita ‘’Mchafu kunuka’’ baada ya kumchezea.Licha ya ushauri na maneno mengi ya busara kutoka kwa rafiki zake(nikiwemo) tabia ile haikubadilika na wakati ule alikuwa akipambana na niliyeitwa Bruda katika vita ambayo hakuijua kama anashindana wakati yeye akiwaza kumchezea mimi niliwaza kumfanya awe mchumba ili nije kumuoa.
‘’Kwetu pazuri….nimeshapakumbukaaaa’’Ni mlio wa simu yangu ambao ulinishtua kutoka kwenye lindi la mawazo ,na nilipoangalia mpigaji alikuwa ni Fred .Nilitamani kuikata ile simu lakini niliona ni suala la kijinga kama niliamua kupambana na mtu ambaye hakujua kama hapambani ni bora tuu kumfanya asijue ili iwe rahisi kujua hatua alizokuwa amefikia ili niharibu mipango yake.
‘’Kamanda shemejio amedata kabisa na saa hii hajielewi ameoza kabisa ,kesho si kama kawaida nilivyokuambia kwenye meseji’’Aliongea mfululizo maneno ambayo hakujua kama yalinikera lakini niliamua tuu kumsikiliza ili asijue chochote juu ya mipango yangu.
‘’Hivi huyo mwanamke kweli,mmeongea leo tuu kesho anataka mkutane mie mbona nina mashaka naye?’’ Nilijaribu kumvunja moyo.
‘’We acha upadre wako ,au unamtaka? Maana ameniambia kuna mtu alikuwa akimtongoza wakati nampigia na amemkatia simu na nilikuwa nakupigia ule muda ulikuwa unaogea ‘’ALliongea maneno ambayo licha ya kuwa na ukweli ndani mwake yaliniumiza na kunikera sana.
‘’Wapi mimi bado sana kwanza mke wangu yupo darasa la pili sina habari na mizigo muiokotayo’’Niliongea kwa dharau kidogo huku nikijua fika moyoni nilimhitaji Yule mwanamke kuliko kitu kingine chochote isipokuwa uhai wangu.
‘’Haya bwana Bruda, na mwaka huu lazima ninenepe maana mtoto kaniambia ndo wakufungua ofisi ,ananiongezea tuu idadi, Monika,Dorah,Halima,Sophia wote hao mimi mfunguzi subiri na huyu wakujiita Mariam’’ Alipiga majigambo kama vile alikuwa jukwaani huku hajui kabisa kama alinikera.
‘’ Ha! Unafungua ofisi kesho mbona na yeye ana haraka hivyo?’’Nilijaribu kumpima Fred .
’’We hukuelewa nilivyokuandikia kwenye meseji,tatizo mnajifanya watakatifu hadi mnashindwa kuelewa mafumbo ya kijanja’’Alizidi kutoa tambo zake ambazo nilikuwa kama naanza kuzizoea,hakujua kama hakuna ujumbe wa maandishi hata mmoja alioutuma kwangu nikausoma.
‘’Mhh haya bwana kazi njema ila asije kukudanganya kuwa we wa kwanza kumbe hata Yule mtoto akawa wake’’Nilizidi kumkatisha tama.
‘’Wewe Yule mtoto wa mamake mdogo yupo chuo’’Aliongea kwa madaha jambo ambalo lilizidi kunipa mashaka juu ya Yule mwanamke kwani kwangu aliniambia ni mdogo wake kwa baba na mama yake.

Wakati nawaza hayo niliona simu yangu ikiita wakati huo Fred bado alikuwa hajakata simu nilipoangalia mpigaji nafsi yangu ilishindwa kabisa kuamua cha kufanya.


Niliamua kukata simu ya Fred na kuamuanumsikiliza Mariam ambaye alionekana kupiga

simu yangu kwa muda mrefu.

??Jamani Magnas mbona bize muda wote huu???Alilalamika Mariam mara tuu alipojua
simu yake ilikuwa imepokelewa.
??Nilikuwa naongea na rafiki yangu mmoja nilikuwa nasoma naye??Nilimjibu nikisubiri kuona
jibu langu kama lilizalisha swali lingine kutoka kwake.
??Wa kike au wakiume???Aliuliza swali sauti yake ikiwa imepunguza ukali kidogo.
??Wakiume jamani??Nilimjibu na kujifanya nalalamika kiume kidogo.
??Nitajuaje rafiki gani saa zima mnaongea??Aliuliza kwa sauti ya kulalamika tena.
??Hata dakika kumi hazijapita ,halafu mimi mbona sijasoma shule za mchanganyiko tangu
shule ya msingi??Niliongea nikitumai jibu lile lingemtosheleza na kujiona mjinga kunifikiria
hivyo lakini tofauti na matarajio yangu ilikuwa ni kama nimemwongezea maswali na
tuhuma juu yangu.
??Nyie zenu kila mtu anasema amesoma shule za wavulana tuu ,kwani hao wa shule ya
msingi si marafiki zenu acheni uongo nyie wanaume??Aliongea huku akionesha haamini
kabisa nilichokuwa nimemjibu .
??Kwani ni nani mwingine aliyekudanganya juu ya kutosoma shule moja na
wasichana???Niliuliza huku nikitaka kujua kama aliongea na Fred ama alinidanganya.
??Hapana ndio kawaida yenu ninyi wanaume wengi sana huwa wanasema hivyo??Alinijibu
huku nilichotaka kumpima nikikikosa.
??Naomba uniamini na hata ukitaka nimpigie umuulize hata simu yake nimekata na
kupokea yako??Niliamua tuu kumwambia ukweli.
??Unaweza kumpanga tuu akakubali siwaamini kabisa??Aliongea na kukata simu.
Nilijikuta msimamo wangu wa awali wa kutowapenda wanawake hadi ntakapooa
unajirudia akilini,kitendo cha Yule mwanamke ambaye sikuwahi kumwona popote.Nilijiona
mjinga kuteseka na kumnyenyekea Yule mwanamke sikutaka tena kuumia juu yake
mwanamke ambaye alionekana kumkubalia rafiki yangu Fred lakini akijidai
kunipenda.Niliamua kutopokea simu yake tena wala kujihusisha naye kwa namna yoyote
ile na hata huko Facebook nilipanga kwenda kumfungia urafiki nawala asinione
tena.Nilimpigia tena simu Fred ambaye naye niliona simu yake inatumika huku lengo
langu ni kumwomba msamaha juu ya kitendo cha kukata simu yake na kupokea nyingine
huku nikipanga kumdanganya mtu aliyenipigia .Baada ya kupiga simu zaidi ya mara tatu
na kukuta bado namba yake ilitumika niliamua kuachana na mpango huo na kutaka tena
kuingia mtandaoni ili nimtoe Yule dada kwenye orodha ya marafiki zangu na kumfungia
kabisa asinione.
??Mhh huyu dada ni jini au mwanga,mbona simuoni??Nilijikuta naongea peke yangu
??Alisema Diane xweet gal,Mariam mara Joshua mbona simuoni??Niliendelea kujiongelesha
peke yangu huku nikiwa nimeamua kumtafuta kwa kuangalia picha zake.Kosa lingine
nililolifanya ni kile kitendo cha kuongeza marafiki wengine bila hata ya kujua majina yao
kazi yangu ya kumtafuta Mariam kwa kutumia picha ilicheleweshwa na picha nyingine za
warembo ambao walinikubalia urafiki ambao walinifanya nikataka kuangalia sura zao
kwenye picha zao nyingine.
Nikiwa bado nahadaika na uzuri wa wanawake wale macho yangu yalitua kwenye picha
ya mwanamke Fulani nakunifanya nizubae kwa sekunde kadhaa nikiangalia picha
yake.Alikuwa ni msichana ambaye alionekana mwenye mchanganyiko kati ya mwafrika
na mwarabu na kuifanya rangi yake kumvutia kila aliyemuona.
??Mambo ?? Ni ujumbe ulioingia kwenye akaunti yangu ya facebook ukitoka kwa rafiki
yangu mwingine mwenye jina la Aneth.
??Poa mzima???Nilijibu na kumuuliza swali.
??Mi mzima habari za wapi???Nilikutana na swali lingine kutoka kwa Yule mwanamke
mabaye wakati huo nilikuwa nimeangalia picha zake mbili tatu ambazo nazo zilionesha
uzuri wake japo alikuwa mzuri lakini uzuri wake haukufikia kwa Mariam au Yule chotara
wa kiarabu.Wakati bado namfikiria Yule msichana mara simu yangu iliita na mpigaji
akiwa ni Fred huku nikibishana na nafsi yangu juu ya kuipokea au kutoipokea kwani
habari ya Mariam ndizo nilizoamini kuwa angeziongelea .
??Sema kamanda hueleweki wewe?Aliongea Fred mara baada ya kupokea simu yake.
??Hivi kati ya wewe na mimi nani haeleweki???Nilimrudishia swali lile badala ya kulijibu.
??We hueleweki ulinikatia simu bila hata kuniambia shemeji alipiga au ndo shobo
tuu???Aliongea maneno yaliyonichoma huku nikiwaza la kumjibu.
??Alipiga simu jamaa mmoja alikuwa akimuulizia baba nikaamua nimpelekee nisameha
Fred na wewe wakati nakupigia nikakuta unaongea sijui hiyo mali mpya
ulopata???Niliongea nikicheka.
??Poa ila naomba kesho kampani nataka nikaonane na Yule mtoto mchuma si
upo???Aliongea jambo ambalo sikulipenda kabisa kulisikia.
??Mhh sijui kama itakuwa poa maana nilitaka niipeleke gereji nikiwahi nitakupeleka kwani
utaenda saa gani??Niliamua tuu kumweleza ukweli kwani licha ya kutopenda uhusiano
wake na Mariam lakini niliamua kutohisiwa vibaya na rafiki yangu kisa Yule msichana.
??We muda wowote mradi isiwe usiku??Alinijibu akicheka
??Sawa itanibidi niipeleke asubuhi ili saa tisa iwe tayari??Nilimjibu huku nikishangaa ule wivu
wa awali ukinitoka kabisa.
??Ndo nikupendeacho Magnas huna kinyongo na mashemeji zako maana nilihisi kama
hujaridhika mimi kumchukua Yule malaika??Aliongea kitu cha kweli ambacho sikujua kama
alijua hilo suala alikuwa na uhakika nalo.
??Angalia wasije kuwa majini ukasema malaika??Niliongea nikicheka.
??Wewe Yule mtoto wa ukweli hakuna cha jini wala nini??Alinijibu akijiamini.
??Poa usiku mwema bwana ngoja nilale ??Niliamua kukatisha maongezi baada ya kuona
uju mbe ukifululiza kwenye simu yangu huku shauku ya kutaka kuusoma.
??Haya kamanda ngoja nikamuage shemeji yako??Aliongea na kukata simu.
??Magnas nakupenda sana na nitaka tuonane?? Ujumbe wa kwanza ulisomeka hivyo na
kuniacha mdomo wazi.
??Kwani huyu mwanamke ana lengo lake nini??? Niliongea huku nikipiga ngumi ukutani,
kwani kitendo cha yeye kumkubalia Fred huku akidai ananipenda kilinifanya nimchukie
Yule mwanamke niliyekuwa nimeamua kumpenda na kuingia katika vita ya kumshindania
na rafiki yangu muda mfupi uliopita kutokana na mambo aliyokuwa ameyafanya tangu
nianze kuwasiliana naye. ??Samahani nina mpenzi wangu na sitoweza kuonana na wewe
??Nilimtumia ujumbe ule na kuzima simu yangu na kuingia mtandaoni kuangalia kama
kulikuwa na ujumbe niliotumiwa.Ni kama vile niliota kwani nilikutana na ujumbe kutoka
kwa Aneth. ??Magnas habari za wapi???Ulisomeka ule ujumbe ambao niliona ni kama
mkombozi wangu kwani niliona ni bora kujibu maswali ya Yule dada kuliko kuendeleza
mawasiliano na mwanamke ambaye alikuwa ni kama muuaji kwa kitendo chake cha
kumpenda kila mtu . ??Nipo Tanzania Dadangu wewe je???
Nilijibu kijeuli kidogo kutaka tuu kumpima Yule dada. ??Najua Tanzania ila Sehemu
gani???Niliulizwa swali ambalo lilijua fika ndilo lingefuata. ??Nipo Dar mwenzangu uko
wapi???Nilijibu na kumrudishia lile swali lake kama ilivyo kawaida ya watanzania wengi.
??Mie nipo Arusha ila kwetu hapo Dar?? Ulisomeka ujumbe kutoka kwa Yule msichana.
??Vipi unasoma ama unafanya kazi???Niliamua kuendeleza yale maongezi yetu kwa swali .
??Huku nilikuwa shuleni ila tumetoka kumaliza wiki hii nitarudi Dar??Nilijibiwa huku nikiamini
naye alikuwa ni mhitimu wa kidato cha sita kama ilivyokuwa kwangu. ??Hongera ulikuwa
unasoma mchepuo upi???Niliuliza huku nikiangalia picha zake nyingine. ??Nilisoma KLF
kakangu??Alinijibu Yule dada wakati huo macho yangu yalitua kwenye picha ambayo
ilinichanganya sana.
??Hongera dadangu unataa uwa mtangazaji nini???Niliuliza swali wakati huo macho yangu
yakiwa bado kwenye ile picha ambayo ilinifanya nikose amani kwani ilikuwa ni picha
ambayo ni kama niliiona sehemu au Yule mtu nilishawahi kumwona kabla ya pale. ??Ndiyo
kakangu napenda sana kuwa mtangazaji ,vipi wewe unasoma au unafanya kazi???Aliniuliza
swali lililonifanya nipate kigugumizi kidogo kwani nilihisi kujieleza kwa kila mtu
kungeniweka matatani kwani hata mtu ambaye alikuwa na nia mbaya kwangu ingekuwa
rahisi kwake kuniangamiza.Nilipata jibu ambalo nilijua lisingetoa mwanya wa kuyajua
zaidi maisha yangu. ??Nipo tuu nyumbani kwani ??Nilijibu huku nikisubiri swali lingine
kutoka kwake.
??Mhhhh??Alijibu huku nikishindwa kuelewa alichomaanisha. ??Mbona unaguna
dadangu???Niliamua kuuliza ??Sidhani kwani shule ulimaliza lini??? Aliuliza swali lililonipa
kigugumizi kidogo kulijibu. ??Nilimaliza kidato cha nne mwaka juzi ??Niliendelea
kumdanganya. ??Mhh mbona nimeona picha zako nyingi sana kama upo
shuleni???Aliendeleza maswali yake magumu . ??Huwa naenda shuleni kwa washikaji
zangu kuwatembelea??Niliendeleza uongo wangu ambao sikujua kama ungejulikana.
??Sawa halafu unaonekana kwenu maisha mazuri maana mara gari hii mara lile??Aliuliza
swali ambalo lilinifanya nijutie kitendo cha kuweka picha tulizopiga kwenye magari yetu
ya pale nyumbani. ??Hapana ni magari ya watu tuu huwa tunavizia kupigia picha??Nilijibu
nikiamini jibu lile lingemfanya aamini nilichokuwa namwambia kwani licha ya kuwa na
maisha mazuri huku nikianza kumiliki gari langu nikiwa kidato cha nne sikutaka kabisa
watu wajue kuwa ninaishi maisha ya kitajiri.Nilitaka kuishi maisha ya kawaida sana
nikiamini ndiyo maisha niliyostahili kuishi na zile mali sikuamini kama zangu kwani
sikuchangia chochote katika kuzichuma. ??Sawa kaka usiku mwema??Ulisomeka ujumbe
wake wa mwisho ??N a uwe hivyo kwako dada??Nilimalizia na kuanza kazi ya kuziangalia
zile picha tena kwa umakini mkubwa lakini wasiwasi wangu mkubwa ulikuwa kwenye ile
picha ambayo tangu mwanzo ilinipa mashaka Fulani.Ilikuwa ni picha ya Yule mtoto
ambaye nilimwona kwenye picha za Mariam hali iliyonifanya nianze kuhisi kuwa huenda
watu wale kama hawakuwa ndugu basi walikuwa ni marafiki.Akili yangu ilishindwa kabisa
kuamua moja huku nikianza kumchukia Anneth sababu ikiwa ni kuwa na uhusiano na
Mariam kwani hadi wakati ule nilikuwa nimchukia Mariam na yeyote aliyejihisha naye
nikimwona kama ni mwanamke aliyetumia udhaifu wa wanaume kuhadaika na uzuri wake
kuwaingiza kwenye mtandao mkubwa wa mapenzi.NIlizima kompyuta yangu na kuamua
kulala japo sikuwa na tabia ya kutozima simu zangu usiku lakini siku ile niliamua
kutokuwasha simu zangu kwani nilijua lazima ningekutana na ujumbe kutoka kwa Mariam
ambaye licha ya kumchukia ilinibidi kumsindikiza rafiki yangu siku iliyofuata hadi kwake
japo nilimhurumia Fred juu ya mwanamke Yule ambaye nilimwona ni mcharuko zaidi
yake na siku hiyo ni kama Azam wanakutana na TP Mazembe lazima mkubwa
angejulikana. Asubuhi ya siku iliyofuata nilijiandaa haraka na kulipeleka gari gereji
ambako ilichukua masaa mengi hadi kumalizia marekebisho yake nilianza safari ya
kurudi nyumbani huku mambo mengi yakizunguka kichwani mwangu kuanzia habari za
Mariam hadi Aneth ambaye nilihisi kuwa kama alikuwa na uhusiano Fulani na Mariam
kutokana na kuwepo kwa Yule mtoto kwenye moja ya picha zake.Nilipofika nyumbani
nilikutana na Fred akiwa amependeza zaidi ya siku zote ambazo tulikuwa tukitoka naye
na hata nguo alizozivaa sikuwahi kumwona amezivaa kabla ya siku ile. ??Mhh we unaenda
kuomba kazi nini???Niliuliza mara tuu baada ya kushuka garini.
??Kawaida sana si unajua siku ya kwanza kukutana na mtoto mkali kama yule??Aliongea
Fred huku akijiangalia kwenye kioo kilichokuwa chumbani kwangu. ??Kaka baba alisema
kama utaondoka umpelekee kwanza gari yake gereji??Ilisikika sauti ya mfanyakazi wetu wa
ndani ambaye Fred alikuwa ameshampitia jambo ambalo nusura livunje ukaribu wetu
kwani nilimchukulia kama dada yangu siku hiyo alitumia uaminifu wa baba yangu kwake
akimtaka kwenda kumchukulia gari yake gereji na kulipeleka nyumbani ambako alimkuta
Yule mfanyakazi akiangalia tamthiliya sebuleni akamshawishi huku akijua nilikuwa
nimetumwa kibaha.Baada ya kufanikisha lengo lake alijikuta akijisifia mbele yangu jambo
ambalo lilinikea sana ikizingatiwa Yule binti nilimchukulia kama dada yangu wa
damu.Tulikuja kupatana tena kwa kinyongo aliponiomba msamaha na kudai asingerudia
tena.
??Sawa dada nitapeleka??Nilimjibu wakati huo niliingia bafuni kuoga na baada ya kujiandaa
nilimtaka Fred aendeshe gari langu na mimi niendeshe gari ya baba niiache gereji halafu
twende huko kwenye miadi ile.Baada ya kuliacha gari gereji nilichukua gari langu
uendesha kwani Fred hakuwa na leseni ya kuendesha gari licha ya kuweza kuendesha
gari kitu ambacho alijifunzia kwenye gari langu. ??Mhh yaani leo kila nguo niliona hainitoi
hadi niliamua kumwazima Hussein??Aliongea Fred muda huo tulikuwa tunakaribia kufuka
eneo la miadi ambapo nilimtaka Fred aende namimi nibaki garini jambo ambalo Fred
alilipinga kwani kwa kupenda sifa alitaka niende naye na anitam,bulishe kama rafiki yake
na hata lile gari ni lake.Baada ya kubishana kidogo ilibidi nimwambie kuwa nitaondoka
kwenda sehemu nyingine wakitaka kuondoka anishtue na anitambulishe kama dereva
wao na yeye siku ile hakujisikia vizuri kuendesha jambo ambalo alikubaliana nalo kwa
asilimia miamoja. Nilishuka na kumkabidhi funguo Fred kasha nilienda kukaa kwenye
Mgahawa mmoja ambao haukuwa mbali na hoteli ile ambayo alienda kukaa Fred
akimsubiri mgeni wake.Kwa bahati sehemu ile ilionesha kila kitu kilichoendelea kwenye
eneo alilokaa Fred.
Niliagiza juisi na kunywa taratibu nikiangalia upande ule aliokaa Fred.Mara kuna gari
ilikuja pale na msichana mmoja mrefu akashuka kasha kushika simu yake na kuongea
kama akipata uelekeo aliokuwa mwenyeji wake baada ya kumwona alimwelekeza kwa
ishara Yule dereva aliyekuja naye akimtaka aondoke.Baada ye nilimwoka Fred akiinuka
alipokaa na kwenda kumkumbatia Yule mrembo ambaye alimzidi kidogo urefu na
kujenga picha Fulani iliyowachekesha watazamaji.Walikaa chini na kuagiza vinywaji
ambavyo hata kabla ya kuvimaliza waliviacha na kuondoka kuelekea garini.
Gari liliondoka huku mwendeshaji akiwa Fred jambo ambalo lilinitisha kidogo na
kunifanya nisimame na kuanza kundoka hali iliyomfanya Yule mhudumu anifuate akidai
malipo yake ,nilimushia noti ya elfu kumi bila hata ya kusubiri chichi nilikuwa
nimeshaondoka japo nilikunywa juisi ya elfu moja tuu akili yangui yote ilikuwa juu ya lile
gari ambalo Fred alimua kuliendesha bila leseni tena katikati ya jiji.Nilipanda teksi
ambayo dereva wake ailuwa akiniuliza nilikokwenda mara tuu baada ya kukaa vizuri.
??Lifuate gari lile jeusi lililotoka sahizi??Niliongea kwa sauti ya kuamrisha. ??Kuna nini mbona
hivyo???Aliuliza swai Yule dereva bila hata ya kuondoa gari hali iliyonitia hasira. ??We
twende bwana kama vipi nipishe niendeshe??Niliongeea kwa hasira nikimtaka anipishe
niendeshe gari lile.


‘’Subiri kijana una leseni lakini nitaendesha ‘’Aliongea yule dereva wakati huo nilikuwa nimeshamto na kuliondoa gari. ‘’Twende bwana’’ Niliongea kwa hasira nikiendesha kuilifuata garil iliyokuwa mbele huku magari matatu yakiwa kati yetu.

‘’Umemwona Yule trafiki nipishe niendeshe’’Sauti ya kuombeleza ilisikika sauti ya Yule dereva baada ya kuwaona askari wa barabarani wakati huo lile gari likitupotea hali iliyoniongezea hasira na kupitisha gari kwa kasi mbele ya wale askari. Nilizidi kuongeza mwendo hadi nilipoliona lile gari likiwa limeingia barabara kuu iliyoelekea mikoani huku foleni ikiwa kikwazo kikubwa kwangu. 

‘’Hakuna njia nyingine tutokee mbele yao?’’Niliuliza mara baada ya kuona foleni ingenifanya nilipoteze lile gari ambalo nilihisi mwendeshaji hakuwa Fred kwani kasi yake ilikuwa kubwa kuliko nilivyomzoea. 
‘’Hapa labda turudi nyuma halafu tuingiee ……’’hata kabla hajamaliza nilisonya kwa sauti iliyomshtua Yule dereva mara baada ya kulipoteza lile gari. 
‘’Vipi kijana kuna nini?’’yule baba aliuliza kwa uoga kidogo.
‘’Wamenipotea ‘’niliongea nikilazimisha kupitisha gari sehemu ambayo palikuwa na ukarabati wa barabara na kuwafanya madereva wa daladala wanisindikize kwa matusi mengi kwani iliwabidi kunipisha kuzuia ajali kutokana na kasi yangu. 
‘’Hawa madereva teski sijui wanavuta?’’Ilisikika sauti ya kondakta mmoja aliyekuwa mmoja ya walikereka na kitendo kile,sikujali zaidi ya kuongeza mwendo huku foleni ikiwa imepungua nikiyapita magari machache yaliyokuwa yakienda kwa mwendo wa kinyonga. ‘’Gooood !’’niliongea kwa sauti baada ya kuliona lile gari likionekana kuongezwa mwendo nadahani kufidia muda walioupoteza kwenye foleni.
‘’Huku niachie tuu kijana hapo mbele hapakosi trafiki’’Alibembeleza Yule dereva sauti mbayo nilihisi ni kama alinisisitiza kuongeza mwendo wa gari. Magari machache yaliyokuwa kati yetu yalifanya nilipoteze lile gari lakini mara chache nililiona huku ikijaribu kuyapita magari yale nikiwa na lengo moja tuu la kuliokoa gari langu akilini nilijua lazima Fred atakuwa alitekwa na Yule mwanamke huku akili nyingine ikinitaka kutoa taaria polisi lakini niliogopa jambo hilo kwani miongoni mwa mambo ambayo wazazi wangu walinikataza ni kulitumia lile gari kama chambo ya kuwanasa wasichana. ‘’Kwani kuna nini mle kijana tutakufa bure?’’Aliuliza Yule dereva na nikijifanya sijasikia alichokisema zaidi ya kuongeza mwendo wakati huo kulikuwa na gari moja tuu kati yetu na lile gari alimokuwamo Fred. ‘’Kama kuna mtu ametekwa piga simu polisi’’Aliendelea kushauri Yule dereva na kunifanya nipate hasira zaidi japo yeye aliona ananishauri. ‘’Kama huwezi kunisikiliza toka nje’’ niliongea nikimwonyeshea bastola jambo lililomtisha Yule dereva na kukaa kimya kama mtu aliyetekwa.
Hatimaye nilikuwa nyuma ya gari alilokuwemo Fred ambalo liliongeza kasi na kila nilipojaribu kulipita lilizuia njia na kunifanya nishinde kulipita kama nilivyotaka.Sauti ya kingora cha gari la wagonjwa ndiyo iliyonishitua na kunifanya niaihirishe jaribio langu la mwisho la kutaka kulipita lile gari nikiificha bastola jambo ambalo lilikuwa ni kama kosa kwani niliruhusu magari mengine kuingia kati ya gari nililokuwa naliendesha na alilokuwa amepanda Fred. ‘’Basi tenaaaa…..’’Niliongea baada ya kuona mshale wa mafuta ukionesha kuwa mafuta yaliisha na kunifanya nikose tumaini kabisa. ‘’Nini kijana?’’Aliuliza Yule dereva kwa uoga. 
‘’Tatizo lenu ubahiri ona huna hata mafuta’’Niliongea kwa dharau hali iliyomfanya Yule dereva aniangalie kwa hasira kidogo lakini baada ya muda akawa mpole nadhani kutokana na kukumbuka kuwa nilikuwa na silaha ya moto.
‘’Lakini kitue kile pale kama una akiba unaweza nisaidia kwani hapa nilipo tangu asubuhi nimeeingiza elfu tatu tuu tena nimejibana kula 
‘’Sauti ya unyonge ya Yule dereva ilinifanya niingiwe na huruma lakini nilijifanya sijaumizwa na hali yake nikishikilia usukani na kuliingiza gari kwenye kituo cha mafuta nikimwamrisha mhudumu wa kike niliyemkuta pale kujaza mafuta nikimpa kiasi kikubwa cha pesa hali iliyomfanya aniangalie kwa jicho la kichokozi ambalo badala ya kuniteka ni kama aliniongezea hasira kwani nilimgombeza kwa sauti kubwa iliyowafanya hata watu walionisikia kunigeukia. ‘’Elfu sabini na nane tuu, chukuwa chenji’’Ilisikika sauti ya Yule binti lakini nilijikuta naondoka bila kumjibu lolote na kuacha kelele za vijana zikishangilia. 
‘’Lazima baadaye akupitie hakuna cha bure hapa ujipange tuu kuhudumia’’Aliongea mmoja wa wafanyakazi na kuwafanya wenzake kucheka kwa sauti ya kimbea, kwa mara ya kwanza licha ya kuwa na nidhamu ya kutumia fedha nilijikuta natumia pesa vibaya huku nikiacha fedha mikononi mwa watu bila sababu yoyote ile,sikujuta sana kwani nilijua nilikuwa naokoa kitu chenye thamani kubwa kuliko zile pesa maisha ya rafiki yangu na gari langu nikiamini Yule msichana hakuwa mtu mwema kabisa kutokana na hali niliyoiona. 
‘’Lile paleee…’’Aliongea Yule dereva akionesha gari lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara na kunipa tumaini jipya huenda waliishiwa mafuta ama kuharibika na kurahisisha kazi yangu ya kuwafukuzia.Niliongeza mwedo hadi nilipoikaribia ambako nilipunguza mwendo na kusimama nilishika vizuri silaha ambayo mara nyingi nilikuwa nikiiba chumbani kwa baba na kuirudisha bila yeye kujua mara nyingi nilipokuwa natoka kwenda sehemu ambayo nafsi yangu ilihisi kulikuwa na usalama mdogo.
Sikujua hata sababu ya baba kuimiliki ile silaha kwani sikuwahi kuikosa kila nilipoenda kuiangalia , niliikaribia ile gari nikitetemeka kwani nilihisi kitu tofauti kila nilipopiga hatua. 


Nilichomoa bastola na kuielekeza garini ambako nilikutana na kitu tofauti kabisa kabisa na nilivyotegemea,Ulikuwa mwili wa yule msichana ambaye nilimwona akiondoka na Fred ulikuwa umeegamia usukani huku ukitoka damu kichwani.

Nilirudisha silaha yangu na kutaka kurudi garini lakini kabla hata ya kugeuka nilisikia sauti ikiniamrisha .

??Baki kama ulivyo upo chini ya ulinzi??Nilijaribu kugeuka ambako nilikutana na silaha kama mbili zilizokuwa zimeelekezwa kwangu,nilitii amri na kuruhusu kufungwa pingu huku askari mwingine akiingia kwenye ile taksi na mimi nikiingizwa kwenye gari la polisi kurundi tena jijini.
Tulirudishwa hadi katikati ya mji kwenye kituo cha Polisi ambako Yule dereva aliruhusiwa baada ya kuhojiwa kidogo huku nikiwataka wale askari kumwachia kwani alikuwa mateka wangu.Aliondoka akiagizwa kuwa kila atakapohitajika angeitwa.
Taarifa ya habari ya kituo kimoja maarufu cha televisheni ndiyo iliyowashtua wazazi wangu baada ya kuliona gari langu eneo la tukio la mauaji na utekaji wa mvulana asiyejulikana na kutoka naye kuelekea Bara.
Lakini kilichowakanganya ni taarifa ya mtuhumiwa mmoja kukamatwa na jeshi la polisi baada ya kukutwa na silaha eneo la tukio,baba aliinuka na kwenda alipokuwa akiiweka bastola yake na kupigwa na butwaa baada ya kuikosa.
??Magnas aliondoka saa ngapi??? baba alimuuliza mfanyakazi wetu.
??Waliondoka mchana alikuwa na Yule rafiki yake??alijibu akitetemeka kutokana na mwonekano wa bosi wake ambaye ilikuwa nadra sana kuwa kwenye hali kama ile.
Mama alikuwa akilia tuu pale sebuleni akihofia usalama wangu hasa baada ya kusikia kuwa niliondoka na Fred hivyo hakujua ni yupi aliyetekwa na yupi alikuwa kiytuoni kwa mahojiano.
??Haloo,,, ndiyo nasikia yupo kituo cha Bunju sijui Ostabey ??Aliongea baba simuni na kumfanya Yule mfanyakazi amtumbulie macho kwa mshangaa.
Dakika tano baadaye gari la polisi lilifika nyumbani lakini likiwa na mtu mmmoja tuu ambaye alipiga honi mara mbili tuu na baba alitoka nje ya nyumba na kuingia garini bila hata ya kusalimiana.Gari liliondoka dakika moja baadaye huku waliokuwemo wakikaa kimya hadi walipokaribia mwisho wa safari yao mbele ya kituo cha polisi nilichokuwa nashikiliwa.Baba alielwkwzwa kubaki garini huku Yule askari mwenye cheo kikubwa pale kituoni akishuka kabla ya kupanda ngazi zilizoelekea ofisini kwake akipuuza saluti alizokuwa akipigiwa na askari aliowapita bila kuonesha ishara yoyote.
Ndani ya ofisi nzuri ya mkuu wa kituo kile cha polisi mazungumzo yaliendelea huku kila mmoja akitaka wazo lake lifanyiwe kazi na la mwenzake likionekana ni kichekesho tuu.
Mkuu wa kituo kile ambaye ndiye aliyeenda hadi nyumbani kwetu kumchukua baba alitaka niachiwe huku askari mwenzake akiona jambo lile kama kitu ambacho hakiwezi kufanyika kwa namna yoyote.
?Haiwezekani kwani taarifa imeshafika kwenye vyombo vya habari na kamanda ameshathibitisha we rudisha tuu hizo pesa??aliongea askari mwenzake aliyeonekana kumdharau sana mwenzake ambaye alikuwa mkuu wake kazini.
??Wewe hili suala linawezekana tunaweza kumkamata kijana yeyote na kumpa kesi unajua mzazi wa Yule kijana ni mtu mkubwa jeshini ni afisa usalama yule??alitahadhalisha mkuu wa kituo akimshtua Yule mwenzake kwani hakuwa na ufahamu wowote juu ya baba yangu.
??Kwa hiyo kama ni mtu mkubwa tukubali kuaibishwa na ukweli kwa sababu ya cheo chake???aliendelea kuhoji Yule askari lakini safari hii akionekana kama ana hofu Fulani wakati huo Yule mwenzake alikuwa akiongea na mtu simuni akimtaka kuingia mahali walipokuwepo.
??Karibu mzee ??aliongea Yule askari mdogo baada ya kumpigia saluti baba huku akimpisha kiti.
??Asante sana habari za kazi???alisalimia baba akiwaangalia wale askari kwa zamu .
Yule askari mdogo alimkumbuka mtu aliyekuwa mbele yake lakini alikumbuka pia kiapo alichokula mbele yake cha kuitetea sheria ya nchi maisha yake yote.Hiyo yote ni kutokana na kitendo cha uvunjifu wa sheria walichokifanya siku chache zilizopita, alikumbuka tukio zima hadi kufikia kula kiapo mara ya pili baada ya kile alichokula mafunzoni.
**********
Ilikuwa siku ya jumapili ambapo jeshi la polisi katika wilaya zote za mkoa wa Dar es saalam lilifanya oparesheni ya kutokomeza uharifu ukiwemo ujambazi na uuzaji wa madawa ya kulevya.Miongoni mwa askari waliopewa jukumu la kusimamia oparesheni alikuwa ni mkuu wa kituo kile cha polisi na msaidizi wake ambao waliongoza kikosi kilichokuwa na askari wasiopungua thelathini kusimamia oparesheni hiyo.
Hadi kufikia saa sita ya usiku vituo vingi vya polisi vilikuwa vikielewa kwa idadi kubwa ya wahalifu waliokuwa wamekamatwa usiku ule.Kulikuwa na vibaka,majambazi na wabakaji waliokamatwa sehemu nyingi huku maeneo ya makaburi ya Kinondoni yakiiongoza kwa kutoa wahalifu wengi sana.
Wakiwa njiani mbele kabisa ya magari matatu yaliyokuwa na watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya uharifu waliona kitu kilichowashtua kidogo na kuamua kuyapisha magari yaliyokuwa nyuma yao kabla ya kushuka na kyuelekea eneo lile.
Mizigo iliyofungwa vema kwenye maboksi ilishushwa kutoka gari moja kwenda lingine iliwapa hofu askari wale wazoefu na kuamua kuwaweka chini ya ulizi wale watu kabla ya kutaka kukagua mizigo ile.
??Usipate shaka afande haya ni maboksi ya sabuni ??Aliongea mmoja ya wale watu kwa kujiamini akimwelekeza Yule mkuu wa kituo.
??Ngoja nikague sabuni gani usiku huu hapa kichakani???aliuliza Yule askari akianza kufungua maboksi yale ambapo baada ya kufungua maboksi kama manne hivi alikutana na miche Ya sabuni.
??Gari yetu iliharibika mku??aliongeaza mwingine.
??Hapana ngoja nikague yote ??yule mkuu wa kituo aliongea akipanda garini na kupekua maboksi yaliyokuwa chini kabisa huku akielekeza silaha yake kwa mtu aliyekuwa garini.
??Hizi ndio sabuni eeheee???aliuliza Yule askari baada ya kukutana na pakti nyingi za madawa ya kulevya jambo lililomfanya mmoja wa watu wale kutaka kupambana naye lakini kabla hajafanya chochote risasi ya mguu ilimfanya awe mpole kama awali.
??Kwa kutumia redio ya mawasiliano Yule askari mwingine alifanikiwa kuwasiliana na askari waliokuwa kituoni waliokuja dakika tatu baadaye na kuwachukua watuhumiwa wale wakiacha maboksi kumi na tano yaliyokuwa pale chini.
??Ushahidi ulioenda unatosha kwa nini tusiuze huu mzigo mwingine ???alishauri Yule askari mdogo.
??Wakija kusema kuwa waliacha makasha mengine tutajiteteaje???alihoji Yule mkuu wa kituo akionekana kuingiwa na tama ya fedha kwani alikuwa akijihusisha na biashara ile kwa siri huku akitaka Yule mwenzake asijue lolote juu ya biashara ile haramu aliyoifanya kwa muda mrefu.
??Tutasema ni maboksi ya sabuni mkuu , jiongeze bwana yaani hapa vitapaa na utajiri nje nje??Aliongea askari mdogo akitumia lugha ya mtasani si kiofisi tena.
??Haya fanya haraka tuondoke aliamrisha mkuu wa kituo na kuanza kubeba yale maboksi na kuyaweka garini.
Walipofika eneo walilopanga kuweka mzigo wao walikutana na kitu kilichowastua na kuwafanya wazibe vinywa vyao kwa mshangao.


"Wekeni mizigo yenu chini" aliamrisha mtu waliyemkuta ndani ya chumba cha siri nyumbani kwa mkuu wa kituo.

Badala ya kuweka mizigo chini walichomoa silaha zao na kuzielekeza kwa yule mtu.

Kwa ustadi na umakini yule mtu alirusha mateke yaliyowafanya watue chini huku silaha zao zikiwatoka mikononi.
" Askari wakubwa tunaowategemea kupambana na magenge ya biashara hii haramu itupotezeayo nguvu- kazi ndio kwanzaa mnajijengea stoo za siri kuikuza" aliongea yule mtu huku silaha yake iliyokuwa mkononi mwake ikielekezwa kwa wale askari.
"Tusamehe mkubwa tukaongee" aliongea yule mkuu wa kituo huku akijiuliza kichwani mwake kama kweli palikuwepo na mtu aliyeijua stoo yake iliyokuwa aridhini zaidi yake kwani aliijenga kwa siri kubwa kutokana na kuwa mwashi kabla ya kuwa askari polisi.
"Haya simamemi!" Aliamrisha yule mtu.
"Sasa mtakula tena kiapo cha kuwa askari bora" aliongea yule mtu kitu kilichofanywa na wale askari bila kipingamizi.
Waliapishwa kwa zamu na kutakiwa kufikisha yale madawa kituoni kitu walichokitekeleza bila usimamizi wowote kwani walijiona wenye bahati kubwa kuponea chupuchupu kupoteza kazi zao na kufungwa kwa kosa ambalo lilionekana kuwa na hukumu kali nchini sambamba na kuua na kubaka.
Yule mtu aliondoka baada ya kuhakikisha kuwa walikuwa wameingia na ule mzigo kituoni, akiwaachia maswali mengi juu yake wale askari.
"Huenda ni afisa usalama" aliongea yule askari mdogo mara baada ya kuingia ofisini.
" Kweli maana alivyoturusha na visilaha vyetu" aliongeza mkuu wa kituo.
Yule mtu akawa rafiki wa mkuu wa kituo ambaye licha ya kuwa,askari hakubahatika kumwelewa yule mtu zaidi ya kujikuta akitoa siri zake nyingi kwake licha ya kujilaumu kila mara baada ya kujua kuwa karibu kila swali aliloulizwa lilikuwa na kitu kilichosaidia kumchunguza kwa kiasi kikubwa lakini baada ya kujibu maswali yale ndipo alipogundua matilaba ya swali husika.
Hakujua chochote zaidi ya ofisi aliyokuwa akifanya kazi yule mtu huku ikiwa haina uhusiano kabisa na habari za usalama.
****
Yule mtu alikuwa mbele yao, lakini safari hii akiwa na suala la kushikiliwa kwa mwanaye wa kiume aliyehusishwa na mauaji.
"Shikamoo mzee, karibu sana" yule askari mdogo aliongea akitetemeka.
Mkuu wa kituo alitoka akiwaacha baba na askari mwingine ambao walitazamana bila kuongea kitu.Baadaye yule mkuu wa kituo alikuja na kumwomba baba atoke nje na kuja garini aliponikuta na kunikumbatia kabla ya kufunga mlango akimnyoshea kidole kama akimwonya yule askari na kutoa gari ambaye kwa kutumia mlango wa siri tuliotokea alirudi ndani.
" Tutafanyaje kuhusu taarifa ya kukamatwa kwake iliyotangazwa kwenye vyombo vingi vya habari?" Aliuliza yule askari mdogo.
" Kuna mtuhumiwa tuliyemkamata kwenye oparesheni tutampa zigo kwani anaonekana kuwa na maisha mafupi, kutokana na kipigo" alieleza yule mkuu kwa kunong' ona.
" Na gari lake?" Aliendelea kudadisi yule askari.
" Gari limeshafika nyumbani kwake muda mrefu" alijibu yule mkuu wa kituo akimshangaza msaidizi wake jinsi lile suala lilivyoenda.
" Mbona suala hili lipo tofauti sana?" Aliuliza yule msaidizi wakati huo kuna taarifa waliipata kupitia 'Radio call' iliyokuwa pale ndani iliyodai kuwa kuna maiti ilikutwa chumbani kwenye nyumba ya kulala wageni huko Kibaha
"Wewe yule baba amemaliza katibu askari wote kila mtu amekutana na lake na kupewa kiapo cha pili" alinong'ona mkuu wa kituo baada ya 'Radio call'kumaliza lakini sauti nyingine ya kile kifaa cha mawasiliano iliwafanya washtuke na kuweka umakini.
" Msichana mmoja ametoroka akiwa chini ya ulinzi wa polisi waliokuwa wakimpeleka kwenye kituo cha polisi Kibaha akihusishwa ma mauaji ya kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Fred Joachim,, amemteka dereva taksi na wanaelekea katikati ya mji , tunaomba ushirikiano wenu kwa kukagua magari yote yaingiayo mjini ova..." redio ile ya mawasiliano ilikata na kuwafanya wale askari kutazamana kwa muda kabla ya kuanza kuulizana.
"Yule kijana tuliyemwachia si alisema alimfuata Fred Joachim aliyetekwa na msichana?" Yule askari mdogo alihoji.
" Ndiyo inabidi tumrudishe ili isije kuwa hatari baadaye huyo binti akikamatwa'' alijibu yule mkuu akichukua simu na kutaka kumpigia baba, lakini kabla ya kupiga simu yake ilionesha kulikuwa na simu iliyokuwa ikiingia lakini ikiwa na namba ngeni.
" Hallo..! "Aliongea kwa uoga kwani ile simu alikuwa akiitumia kuwasiliana na wakubwa wake kikazi pekee.
" Njooni mmchukue muuaji yupo hapa stendi mpya ya Mbezi" aliongea yule mtu na kukata simu na hata alipojaribu kumpigia haikupatikana tena.
" Kuna nini tena?" Aliuliza msaidizi wake baada ya kuona mabadiliko ya usoni mwa mkubwa wake, lakini kabla ya kumjibu kuna askari aliingia ofisini na kutoa salamu.
"Kuna mahabusu amefariki Afande" aliiongea yule askari lakini kabla hata ya kujibiwa redio ya mawasiliano ilisikika tena na kuwafanya wote wawe kimya.
"Gari lililombeba Msichana aliyetoroka mikononi mwa polisi huko Kibaha limepata ajari na kusababisha kifo cha dereva na msichana amekamatwa na polisi wakati akijaribu kutoroka ova''
Wale askari wawili mtu na msaidizi waliondoka na kuelekea kule alikofia mahabusu lakini badala ya kumkuta waliyemtarajia walinikuta nikiwa nimejilaza sakafuni sina habari.Walitazamana na kuelekea mapokezi walipokutana na mtuhumiwa wa mauaji yale aliyekuwa chini ya ulinzi wa askari.
" Ameumia vibaya sana" aliongea mmoja wa askari aliyekuwa amemleta.
"Mpelekeni hospitalini akiwa chini ya ulinzi" aliamuru mkuu wa kituo na kuingia ofisini kwake.
" Kuna mtu ana maongezi na wewe " aliongea mmoja wa askari aliyeingia mle ofisini dakika chache baada ya mkuu wa kituo kukaa.
"Nani usiku huu?, mwambie aje kesho" alifoka mkuu wa kituo.
" Anaonekana mtu mk....." kabla hata ya kumalizia sentensi yake mkuu wa kituo alibamiza mkono mezani kwa nguvu.
"Tokaaaa nimesema sitaki kuonana na mtu saa hizi" aliongea na kuufunga mlango kwa kuubamiza baada ya yule askari kutoka lakini kabla hajazungusha funguo afunge mlango kuna mtu alifungua mlango na kuingia kibabe,jambo hilo lilimshtua mkuu wa kituo na kumwangalia yule mtu usoni na kugundua kuwa alikuwa ni mtu aliyemfahamu.
"Shikamoo mzee"alisalimia mkuu wa kituo baada ya kumwona yule mtu.
Alikuwa Kamishina wa jeshi la polisi nchini Ndugu Fabian Milinga mtu aliyefanikisha yeye si tu kuwa mkuu wa kituo bali hata kuwa askari polisi akitumia cheti cha rafiki yake aliyekuwa nje ya nchi.
"Marhaba ,pole na kazi" alijibu akikaa kitini.
"Asante mkuu, yaani hapa akili hata haifanyi kazi"
"Pole sana ndugu yangu, si umeona nilivyokuja, sijaja kiofisi" alivuta pumzi kabla ya kuendelea.
"Huyo mtoto anayeshikiliwa ni mwanangu wa pekee" aliongea kwa sauti ya chini yule Kamishna wa polisi.
"Anayeshikiliwa yupi?" Aliuliza mkuu wa kituo kwa hamaki.
"Aliyepata ajali" Alijibu.
"Pole sana ,tutafanyaje mkuu?" Mkuu wa kituo aliuliza huku akiwa hajui cha kufanya.
" Sikiliza mwanangu yupo hospitalini chini ya ulinzi na hali aliyonayo haitamaniki hasa miguuni, kuna maiti iliyotokana na ajali ,tutaipa tuhuma hiyo maiti na mwanangu nampeleka Afrika kusini kwa ajili ya matibabu''
"Sawa baba ngoja tufanye haraka haraka" alijibu na kutaka kuinuka.
"Waweke sawa askari wako wasifuatilie tena hii kesi" alimaliza na kuodoka.
Bwana Milinga aliwapigia simu watu kadhaa na kuamua kuelekea nyumbani baada ya kuhakikishiwa kuwa mwanaye alikuwa kwenye mikono salama ya wafanyakazi wake aliowaamini sana akiandaliwa kwa ajili ya safari ya kuelekea Afrika kusini kwa ndege ya kukodi.Alijua suala lile lingemweka matatizoni kama ingekuja kujulikana kuwa mtoto wa mtu mwenye cheo kikubwa jeshini kufanya mauaji ya kijana ambaye kila aliyepata habari ile alikuwa mpenzi wake.
Huku nyuma mkuu wa kituo hakumwelewa kabisa bwana Milinga kwani ilifahamika kuwa hakuwa na mtoto wa kike zaidi ya watoto wake wa kiume wawili waliokuwa wakifanya kazi nje ya nchi.
Alijua kuwa alikuwa na mfanyakazi wa kike aliyekuwa akimlea mtoto aliyeokotwa baada ya kutupwa na mama yake jalalani.
Hakujua suala la mtoto wa kike muuaji kuwa mtoto wa kamishina wa polisi nchini.
"Labda michepuko " alijikuta akiropoka na kumfanya msaidizi wake aliyekuwa mbele yake acheke na kumshitua.
"Michepuko tena? Kweli umechoka hadi unaota hivyo, saa hizi ni saa saba za usiku tumekuwa kama ma-CRO tuondoke tuu bosi" aliuliza na kumshauri mkuu wa kituo.
"Mhh tuondoke jamani hii ni overtime ya ajabu"aliongea mkuu wa kituo na kuinuka.
Lakini kabla ya kuondoka radio ya mawasiliano ilisikika na kutoa taarifa ya kifo cha msichana aliyetuhumiwa kwa mauaji na kuwafanya washushe pumzi kwa pamoja kwani miongoni mwa mambo yaliyowachanganya siku ile lilikuwa ni suala la mauaji ya watu wawili kwenye matukio mawili yaliyoonekana kuwa na uhusiano mkubwa.
" Vipi kuhusu yule kijana wa mzee wetu itatubidi tukamtoe ili kesi iishie vifo"alishauri mkuu wa kituo.
"Sawa ngoja tukamwangalie"aliongea msaidizi wake na kuanza kuondoka kuelekea mahabusu.
Walishtuka baada ya kufika kwenye kile chumba nilichowekwa, lakini cha kushangaza hawakuniona jambo lililowapa mashaka na kushika vichwa vyao kwa taharuki.
Baada ya kutafakari kwa muda wale askari walitoka kimya kimya na kuingia garini na kuondoka.Njiani hakuna aliyemsemesha mwenzake hadi pale mkuu wa kituo aliposhuka na kumwaga mwenzake ambaye alionekana kuwa kwenye lindi la mawazo.
" Tumefika shuka afande" alitania mkuu wa kituo ambaye mkewe alikuja kumkumbatia.
" Jirani hamkulala tuu? " yule askari mwingine aliuliza baada ya kutoka garini akimwangalia mke wa mkubwa wake kazini.
Alikumbuka mwaka ule alipanga aoe baada ya kukaa bila kuoa kwa muda mrefu tangu aahirishe mpango wake wa kuoa baada ya msichana waliyepatana kuoana, kuolewa na askari mwenzake tena wa cheo cha chini kabisa pale kituoni ambaye alihama siku chache kabla ya kumnyang'anya mkubwa wake mchumba.
Aliwaangalia majirani wake na kuelekea nyumbani kwake huku wazo la ndoa likiwa na nguvu kuliko hata misukosuko ya kazini, alimwonea wivu mkubwa wake aliyepokelewa kwa Upendo mkubwa na kwenda kusahaulishwa mambo yote mabaya.
Alienda moja kwa moja kujilaza kitandani huku akijipangia kula asubuhi iliyofuata kutokana na usiku kuwa mkubwa.
____________________
ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment