Thursday, 7 April 2016

RIWAYA MPYA;NITARUDI ARUSHA

Hapo nilimwona kwa ukaribu na uzuri zaidi ,kumbe kabla sikuona kovu lililokuwa mdomoni mwake na kumfanya ongee kwa shinda kwani liliufanya mdomo wake ukae vibaya kidogo lakini aliponyanyua mdomo wake nilijua kuwa hakuwa na meno ya mbele, sikutaka kumwangalia zaidi kwani si tuu alinifanya nimwonee sana huruma bali alinifanya nimwogope kwani nilihisi natazamana na kiumbe fulani cha kutisha ambacho kilifanana sana na binadamu, kwa haraka haraka nikatoa noti ya shilingi elfu moja na kumpa.

Sikuishia hapo  kwani nafsi yangu ilinisukuma kutaka kujua Zaidi kuhusu maisha yake, akili yangu haikutaka kukubaliana na mawazo ya wengi kuwa mtu yule alikuwa na historia kama zile za ‘ombaomba’ wengine nikajikuta nikiapa kurudi tena Arusha.
Nikarudi , tena Zaidi ya mara moja.
Ilikuwa kazi ngumu kumpata kutokana na historia yake ya kutisha ambayo moyo wangu ulihisi kabla lakini kama bahati nikakutana na rafiki yake Mtoto John ambaye alinifikisha kwa mtu huyu aliyeitwa Japhet.Historia ya kusikitisha ikiwa ni pamoja na vifo vya wazazi wake, kunyang’anywa nyumba yao hadi kwenda kuishi na mama John ambaye naye alikuwa na kisa cha kutisha ambacho kiliungana na historia yangu wakati nipo sekondari nilipomzidi ‘kete’rafiki yangu kwa msichana wake,kisa kile kinaniathiri sana kabla ya kuuchukua uhai wa mama huyo masikini.
Kifo cha kukutatanisha cha mama John kinatutenganisha na John ambaye anapotelea kusikokujulikana hadi pale tulipokutana niliporudi Arusha kumuoa kipenzi changu ambaye ndiye alianzisha safari yangu ya kwanza kwenda Arusha.
Kwa ndoa ile sina namna nitaendelea kurudi Arusha kuwatazama wakwe zangu ambao wamebakiza miezi kadhaa kabla ya kumaliza kifungo walichopewa kwani niliwashtaki kwa unyama wao licha ya kuwa nilimpenda binti yao.
TEMBELEA www.kalamuyangu.blogspot.com Kuisoma hadithi hii kali.

0 comments:

Post a Comment