
Kaditama nimetua, sisongi sirudi tena,Mambo nimeyatibua, hata nife hutoguna,Kweli yote nimejua, ulianza mbali sana,Basi.Nilihisi tunaota, kumbe ninajidanganya,Ilipita myaka sita, sina nililolifanya,Mwenyewe ukajipata, mwenyewe sikujiponya,Basi.Nikaiweka busara, kumbe linaletwa shari,Kaona kovu imara,...