Monday, 25 May 2015

SIMULIZI YA KWELI;BARUA KUTOKA KUZIMU


MTUNZI;Moringe
Wapendwa wazazi,
Salam nyingi ziwafikie hapo mlipo,mtakapo kujua hali yangu mimi si nzuri kutokana na hali ya mazingira niliyopo.
Najua mliamini na mnaanini kuwa nipo na malaika tukimsifu mungu lakini naomba niwaambie ukweli tuu kuwa nipo jehanamu nikipata mshahara wa matendo yangu.
Jemima mtoto wenu wa kwanza na wa pekee kupata kazi rasmi inayoeleweka nipo kuzimu baada ya ajali ile mbaya mnayoamini kuwa ni ya kupangwa.
Ni kweli ilipangwa lakini mpangaji si binadamu bali ni SHETANI ambaye aliamua kunipandisha cheo baada ya kufurahishwa na kazi yangu niliyoifanya vyema.Naomba ieleweke kabisa hapa SIKUAJIRIWA na SHETANI bali nilikikuta nafanya kazi yake vyema hadi siku ile nilipopata ajali mbaya ya gari iliyoharibu mwili wangu na kuwapa taabu ya kuutambua mwili wangu kabla ya mazishi hadi pale njia za kitaalamu zilipotumika.
"Mliumia sana".
Najua kwani mlinililia sana kufikia hatua ya kupoteza fahamu kea zamu siku mnaiona maiti yangu.
Mliamini nilikuwa safarini kwenda kurekodi ablam yangu ya kwanza ya nyimbo za injili nikiwa na meneja wangu aliyeamua kunidhamini kwa kila kitu,mliamini ni mtoto wa pekee niliyekuwa masaada kwenu na kwa wadogo zangu hata ndugu waliohitaji msaada ,binti niliyejitoa kwa hali na mali kusaidia ujenzi wa kanisa letu hapo kijijini, kuwashauri wasichana wenzangu kusoma na kumtumikia Mungu huku wakiheshimu wakubwa wao.
Kwa kifupi nilikuwa mtu mwema kwa kila mtu hapo kijijini hata mngepewa mamlaka ya kuteua mtakatifu mgeniteua lakini leo mimi nipo kuzimu na niwakala wa SHETANI.
Ukweli ni huu;-
Ingawa kweli huwa naimba nyimbo za dini sikuwa njiani kuelekea studio bali nilikuwa na mume wa mtu ambaye nilimfanya aisahau familia yake kwa jinsi nilivyomchanganya na penzi langu,tulikuwa tukielekea Dar es saalam kwa ajili ya kupata starehe.
Hamkulijua hili ndiyo maana hamkuisha kumlalamikia Mungu kwa kitendo cha kunichukuwa ningali Mdogo 'poleni sana kwa hilo'.
Mlipoozwa na kiasi kikubwa cha fedha mlichokikuta kwenye akiba yangu lakini hamkujua tuu katika maisha yangu sijawahi kutumia mshahara wangu zaidi ya kuwachuna waume za watu waliokuwa tayari kunikabidhi mishahara yao bila uoga wowote,'hamkujua hili kutokana na umbali wetu na ufinyu wa njia za mawasiliano'.
Lakini si hivyo tuu nilijikuta nimeanza kuwashawishi hata viongozi wa dini walioanza kama utani hadi wakafikia hatua ya kuligawa kanisa kule kijijini nilikofanya kazi, 'Mungu naomba uwasamehe'.
Hamjui tuu kilichofanya nisifukuzwe kazi kipindi kile niliikuwa huko nyumbani kwa takribani miezi miwili ,,,niligawa penzi kutoka taifani hadi wilayani nikawa mgonjwa kweli kama nilivyomtaka yule daktari baba nani sijui aliyekufa kabla yangu nipo naye huku kwani michezo aliyocheza na wajawazito na watoto wa shule ilitosha kumleta hapa hata bila kuongezea ile tabia yake ya kuuza dawa huku wananchi wakijifia.
'Hamjui hayo mnaamini binti yenu nitakuwa nikiimba na watakatifu wengine kutokana na jinsi nilivyojipambanua kwenu'.
Wasalimieni sana wadogo zangu na rafiki yangu mama Mage najua hakujua kama hata mumewe ni miongoni mwa wanaume mia tano niliwaambukiza virusi vya ukimwi na kupelekea kuzaa mtoto mwathirika, anisamehe sana natamani yawe ndoto lakini akhaaaa mumewe alizidi sana kwani mara ya kwanza alinibaka nilipoenda kisimani kipindi hata hajaoa na akanitaka nimkumbushie enzi, nipo naye anajaribu kusoma nikiandikacho bila mafanikio kwani macho yake yameungua sana.
Ningependa niendelee lakini BOSI WANGU, SHETANI amenikazia macho kwa ukali.
Wasalamu
Mwanenu mpendwa.

MWISHO.

0 comments:

Post a Comment