Sunday, 24 May 2015

UNAPODHANI UMEFICHAMA BILA KUJUA UMEJIFICHA NA UNAYEMKIMBIA

Na.Moringe Jonasy
Umewahi kucheza kombolela? kama umewahi kuucheza ama kusimuliwa hadithi  zake utakumbuka kuwa kulikuwa na mabingwa wa kufichama na kutoonekana hata mnapomaliza mchezo yeye anakuwa bingwa.
Walikuwa na mbinu nyingi sana za kujificha ikiwa ni pamoja na kwenda kujificha sehemu ambayo wengi mnazidharau na kuziona kama si mahali palipojificha.

Pia walikuwa wakienda kujificha mbali sana na eneo la mchezo na kuwafanya watafutaji waombe msaada kila mwisho wa zamu zao.
Achana na kombolela labda nikukumbushe tuu kitu kingine cha utotoni , uliwahi kuiba mboga ama hela halafu mkubwa wako asikugundue hata baada ya kukuhoji sana na ukakataa.
Labda umewahi kumdanganya mpenzi wako kuhusu kitu chochote iwe kumsaliti ama kumdanganya historia yako ya mahusiano, na asijue kama ulimdanganya?.
Najua umewahi kufanya moja kati ya hayo niliyokuuliza hapo juu ila kuna mtu alikuwa akijua vyote hivyo na hukumjua.
Huyo si mwingine bali ni wewe mwenyewe, kila unapodanganya nafsi ama akili yako inajua kuwa unadangaya.Hapo ndipo unaweza kukubaliana na mimi kuwa Mungu hahangaiki kutumia njia nyingine za kupata habari zaidi ya nafsi yako amabayo haiwezi kukudanganya.
Unaweza kumdanganya mzazi wako, mpenzi wako, mwalimu wako, jirani yako na hata adui yako ,Je unaweza kuidanganya nafsi yako? 
Hapana huwezi kuidanganya hivyo hivyo huwezi kumdanganya Mungu wako kwa namna yoyote ile.
Kama unaiba ,unazini ,unadhulumu ama unafanya chochote kinyume na mapenzi ya  Mungu ukifikiri kuwa hakuna anayekuona ila  nakwambia:
 Niambie Mtazamo wako  #Mwanakalamu mwenzangu

0 comments:

Post a Comment