Saturday, 23 May 2015

UNAPOJIWEKA HAZINA KWA UAMINIFU WAKO

Na.Moringe Jonasy
Umewahi kupoteza kitu halafu kuna mtu alikiokota na kukurejeshea?
Ama umewahi kukosea kumpa mtu chenji halafu akakurudishia ?


Umewahi kumwona mtu akisahau kitu cha thamani halafu ukaamua kumpa hata kama unauhakika kuwa asingekumbuka haraka?
Au umewahi kufanya kazi kwa mtu kwa uaminifu mkubwa licha ya kwamba ulikuwa na matuamaini kwako?
Basi kama hujawahi kufanya hayo hapo juu basi kuna uliloshuhudia ama kusikia miongoni mwa hayo niliyokuuliza.
Mara ngapi umeona watu wakikosana kisa mamedhurumiana ama kutolipana madeni? Yote hay= sababu ya kukosa uaminifu.
Basi leo naomba niuongelee huo uaminifu kwa nyanja tofauti kidogo;
Mtu anakutafuta na kutaka uwe mfanyazi wake saloni, dukani,kiwandani ,shambani na hata nyumbani.
Huyo amekuamini kweli maana anajua wewe unaweza kufanya shughuli hiyo kama ambavyo angefanya au zaidi yake na kama chini ya hapo basi kwa kiwango kidogo nayo hutokana na wewe kukosa ufahamu wa jinsi alivyogharamika kwa muda ,nguvu na hata fedha ili kuwekeza katika hicho anachotaka ukiendeshe.Hategemei kukuweka hapo ili umwangushe japokuwa katika kila kitu kuna mtazamo hasi lakini hadi kukuweka wewe basi kautoa huo uhasi kwako.
Mbunge, mkuu wa wilaya ama mkoa, mwalimu ,mwanafunzi na hata mwanafasihi amepewa dhamana na watu wengi walio nyuma yake wakiwa na matumaini makubwa kwao je, dhamana hiyo wameitumia kwa uaminifu mkubwa ama wanafanya bora liende?
Uaminifu wa kuichukulia dhamana uliyopewa kama yako na kuthamini ndiyo silaha ya ama kupata umiliki wa hiyo dhamana milele ama kunufaishwa kwa kiwango kikubwa kuliko matarajio na malengo yako.
Labda nikupe mifano kadhaa;
Kuna kijana alipewa kazi ya kulisha ng'ombe na tajiri mmoja kijana huyo allifanya kazi kwa uaminifu mkubwa na kumzalishia yule tajiri faida mara kumi na aliyotegemea , unajua alichokifanya yule tajiri?
Hakufanya kitu kingine zaidi ya kumwongezea malipo na kumzawadia ng'ombe mmoja wa maziwa ambaye yule kijana alimtunza huku akiuza maziwa kabla ya kuja kupata mtaji wa kununua maziwa ya ng'ombe wa bosi wake na kuyauza kwa wanunuzi wakumbwa na kupata faida kubwa iliyopelekea kujenga kiwanda cha kusindika maziwa na kutengeneza bidhaa mbali mbali zilizotokana na maziwa.
Baadaye yule kijana alikuja kuwa mfanya biashara mkubwa mwenye kumiliki viwanda zaidi ya kimoja cha maziwa hata katika mikoa ya mbali ambako hata hakuwahi kupata bahati ya kufiria kuwa angefika huko.
Watu zaidi ya hamsini wakaajiriwa kwenye viwanda vyake wakati huo tajiri wake akawa amebadili mradi ,aliaachana na ufugaji wa ng'ombe.
Siku moja akiwa katika moja ya ziara zake za kutembelea viwanda vyake alipokelewa na mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda kimojawapo ambaye alimshitua.
Alikuwa mtoto wa bosi wake ambaye alikuwa akisomea masuala ya kilimo na alihangaika muda mrefu akitafuta kazi kabla ya kupata katika kiwanda hicho.
Walifurahi sana na akamkabidhi milki ya kiwanda hicho.
Unajua kwa nini alifanya hivyo.
Jibu ni dogo tuu Uaminifu wao na wa familia ya kijana kwa tajiri ulifanya kazi naye ameamua kuundeleza.
Mfano mwigine ni rahisi tuu, si umewahi kuona wabunge wakiwa kama baba wa familia yaani mbunge anapitwa bila kupingwa na hata akitokea wa kumpinga haambui kitu kwani mbunge huyo anakuwa mwaminifu kwa jamii yake hivyo uaminifu umekuwa dhamana kwake.
Mwisho ukiwa mwaminifu kwa Mungu na kutenda yampendezayi basi nawe tegemea fadhila na mengi usiyoyategemea kutoka kwake.
Je, wewe ni mwaminifu hata kwa mpenzi wako?
Niandikie hapa chini mtazamo wako ‪#‎mwanakalamu‬ mwenzangu

0 comments:

Post a Comment