Friday, 22 May 2015

ALIKIBA UKIFANYA HILI UTAJIZIKA MWENYEWE


Na.Moringe Jonasy
Habari wana Afrika Mashariki, natumaini mu wazima wa afya na wale wagonjwa Mungu awape uzima na muendelee kumtumkia.
Leo nianze na kusimulia kisa fulani kilichotokea jana,

Nikiwa ndani ya daladala wakati naelekea kupata tiba hosptali ya Mkoa wa Kilimanjaro ( Mawenzi) kuna nyimbo kadhaa zilikuwa zikionesha kwenye'' screen '' ndogo iliyokuwemo ndani.Nakumbuka wakati napanda garini nilikuta wimbo fulani wa dance wa kinaijeria ulikuwa ukiishia na kuukaribisha wimbo wa shetta wa shikorobo kabla ya Snura Mushi kuja na Wimbo wake wa  nimevurugwa kisha wimbo wake wa mwisho kuutoa siukumbuki jina lake.Zilifuata nyimbo nyingine nyingi kama chuna buzi na nakomaa na jiji ambao hadi nashuka garini alikuwa akiendelea kuonesha umaarufu wa kunyonga nyonga zake.
Nilikuwa nimekaa jirani na rafiki yangu ambaye alikuwa akinipeleka hospitalini na pembeni alikuwa amekaa mzee mmoja hivi ambaye alionekana kuona aibu si tuu kuangalia nyonga na vitovu vya wanawake bali aliona hata aibu kusikikiza mashairi yaliyokuwa yakiimbwa kwani alikuwa amesafiri na binti yake aliyekuwa akitoka naye KCMC hospitali kwani wasanii hao walionekana kufurahia mashairi yao yasiyo na staha kabisa " eti mchukue um...." .
Baadaye rafiki yangu alivunja ukimya kwa kusonya kabla ya kuwalaumu wasanii kuiga umagharibi na kuuita " MAENDELEO YA MUZIKI" jambo ambalo mzee yule ni kama alionekana kusaidiwa kutumbua jipu hilo ambalo aliona likielekea kutengeneza majipu mengine makubwa.
Alilaumu sana muziki wa kisasa akidai wasanii wameishiwa mashairi na kuamua kuwafanya wanawake wakata nyonga vivutio vya video zao huku wakijisifia kutumia gharama nyingi kwa video zenye ubora.
Lakini watu wengine garini licha ya kuonekana kuelewa alichokuwa akikisema mzee yule wengi walijifanya kumwona yule mzee kama mshamba fulani lakini wengine wakikubaliana naye.
Hayo yakipita nikaacham
 Mjadala mkubwa garini bila kuchangia kitu chochote lakini kichwa changu kilikuwa kipo kwenye mjadala mkubwa wa kujaribu kufanyia kazi mawazo yale nikijaribu kuuaminisha umma hasa watu ambao umri wao ndo unaelekea ama umefika '' mawio'' juu ya uzuri wa muziki wa kizazi kipya na video zake.
Niliposhuka garini  nilimwambia rafiki yangu " yahaya si nzuri ehee?"
''Yahaya?"
''Ehhe''
''Ndo nani?"
''Wimbo wa jay dee, yahaya unaishi wapi,,,,''
''Anhaaa nimekusoma bado unajadili nyimbo za kisasa? , zipo nyingi shoga ya shaa, mwana ya Alikiba na nyingine nyingi kama kiboko yangu ya mwana fa , sihitaji marafiki na hata number one ya Almasi''
''Kweli jamani kumbe zipo nyingi kwa nini wasiziweke hizo?"
''Watawekaje hizo za kitambo halafu hawana dhamana hao,angalia video ya  mwisho ya shaa,diamond na hata huyo alikiba atavyotoa hayo machekecha sijui''Alidadavua rafiki yangu aliyeonekana kukereka na huu utamaduni tunaoita Kuvuka boda.
Hapo nilijifikirisha kidogo ,wakati huo nilikuwa nimeshafika hospitani nikapanga foleni kusubiri huduma namba yangu mkononi tukakaa pembeni na kuanza kuangalia show za wasanii wa kizazi chetu pamoja na video huku tukisonya sonya kana kwamba tulikuwa tukichukia foleni kumbe hali ya muziki wetu ikiwa sehemu mbaya sana na huku kutafuta kupigwa trace urban ndo ukiharibu kabisa muziki wetu.
Baadaye nikaajikuta nikijaribu kufikiria jinsi video mpya ya alikiba itakavyokuwa na aina ya utunzi wake ulivyo.
Nikasonya hadi kumshitua rafiki yangu.
''Vipi hali mbaya?" niliulizwa na rafiki yangu.
''Hapana , cheketua inaweza kufuata mkondo wa akina " nasema nawe" .Niliongea nikiwa nimekunja sura na kumfanya rafiki yangu ashindwe kunielewa haraka ama naumwa ama nimekereka na mada niliyokuwa naifikiria.
''Kwa nini unaamini hivyo?"
''Najaribu kufikiria muziki anaoufanya Ally kuanzia mashairi yake murua, show zake za kutumia live band hadi video zake ni mtu ambaye ameonekana kuwavutia watu wengi wanaopenda muziki halisi lakini kwa wimbo huu wa chekeche cheketua naona dalili za kupoteza kundi fulani la wapenzi wa muziki wake'' Nilivuta pumzi huku nikimwangalia rafiki yangu aliyeonekana kutonielewa.
''Kivipi?"
''Ni hivi , nimemwona Alikiba akitumbuiza wimbo wake wake wa chekecha cheketua na kila alipofikia kwenye kiitikio amekuwa akiwaita wadada kuwashindanisha kucheketua / kunengua hivyo naona dalili ya kuufanya huu wimbo uishie trace na si sebuleni kwetu tukiwa na wazazi wetu.
''Hapana nimjuavyo Ali hawezi kufanya hivyo ni mtu anayejiheshimu sana, huoni licha ya kuwa superstar hana hata tatoo? Aliongea na kunifanya nitabasamu kidogo.
''Mhhh labda iwe hivyo lakini akiiga mauno ya akina dada wa uswazi basi hata hiyo live band haitokuwa na maana kwani wapenda live band wengi ni watu wenye heshima zao ambao huweza kwenda na familia zao kuangalia muziki mtamu ila kama vitovu nje asubiri kushangiliwa mitandaoni na wahuni kuwa ni mkali lakini nafsi ikimsuta kwa kusaliti maadili kisa kuutaka umataifa kwa njia haramu.
NAMALIZIA KWA KUSEMA WAKICHEKETUA TUU BASI TUTASEMA KWA HERI.
Moringe Jonasy
21/04/2015

0 comments:

Post a Comment