Friday, 22 May 2015

DUNIA BHANA INAZUNGUKA SANAAAA


Na.Nyemo Chilongani

Nakumbuka nilipokuwa mdogo, nilipenda sana kusoma hadithi za Shigongo bila kujua kwamba hata mimi pia nina kipaji cha utungaji. Nilipoanza kuandika mwaka 2004, nikajiuliza, hivi siwzi kuandika kama yeye? Na hata kama nitashindwa, siwezi japo kufuata vikorombezo fulani kwenye hadithi zake, nikasema ngoja nijaribu. Hadithi yangu ya kwanza kuandika ilikuwa PASTOR BEN AND SISTER ROSE.
Bahati nzuri, mtu wa kwanza kabisa kusoma alikuwa Odero Taiya, form one hiyo. Alipoisoma, akaniambia Nyemo umeandika hadithi kama Shigongo, nikashtuka sana na kusema kwamba kumbe najuajuaeeee, ngoja nisonge.

Nikajiandikiaandikia weeee, wanafunzi waliiba sana macounter book yangu. Kwa sababu nilitumia fedha sana kwa ajili ya hadithi, wisho wa siku na mimi nikasema kuna watu nao watakiwa kutumia fedha kila siku au kila wiki kwa ajili yangu, nadhani imetokea kwani mtu anakwambia nafuatilia hadithi zako gazetini...nafurahi sana.

Baada ya kila siku kusema my role model ni Shigongo, nikaona ni lazima na mimi nimtengeneze mtu ambaye atasema Nyemo, wewe ni role model wangu. Ilikuwa ngumu, kumtengeneza role model kwanza ni lazima uumie sana, upate maumivu sana, upitie mashimo, majangwa, vizuizi vingi ila mwisho wa siku, akajitokeza rafiki mmoja Facebook, hakunificha, akaniambia tu Nyemo story zako zinaniinspire sana, you are my role model.

Najua wengi wanatamani kuandika hadithi kama zangu, nahisi zinapendwa kwa sababu mtiririko wake nahisi umekaa kipekee sana. Kwa sababu aliniambia mimi ni role model wake, nikawa na hamu ya kumuona. Ni juzi tu katia miguu Dar, kitu cha kwanza kanitafuta. Kukutana naye ilikuwa shughuli sana, ubize mwingi ila mwisho wa siku nikampa mualiko home, akaja, nikapiga naye stori, tukashauriana sana. Huyu ni Moringe Jonasy Mhagama hapo pichani.

Labda alifikiri Nyemo angekuwa baba fulani au mtu wa suti, alipokuja, picha limeanza nimemfuata lodge na kaoshi, kichwani kofia, kiunoni penzi ya jinzi, chini sendozi, akalowa

Ukitaka kujiona kwamba wewe ni mwalimu mzuri, ni lazima darasani kwako watoke walimu, ukiona darasani kwako hawajatoka walimu, jua ulikuwa mbovu tu.

Namkumbuka ticha wangu wa History, Noah Simon Mwasongwe, alinifanya nitamani kuwa mwalimu wa historia, mwisho wa siku nikawa mwandishi, ila ningekuwa mwalimu, basi ningefundisha historia. Ndiyo hivyo bhana, kipaji kikawa zaidi ya elimu.

Jiandaeni kusoma simulizi yangu mpya ya NISAMEHE LATIFA uone jinsi msichana wa Kihindi alivyotengwa na familia yake kisa kapewa mimba na mtu mweusi bila kujua kwamba ni mtoto wa aina gani angezaliwa

0 comments:

Post a Comment