Friday, 22 May 2015

WENGI TULIKUWA NA MATUMAINI

Na.Moringe Jonasy
Unakumbuka shamra shamra za mwaka mpya za mwaka huu? Achana na za miaka mingine iliyopita mwaka huu ulifanyaje?
Ulichoma matairi ya magari barabarani na kulipua baruti?
Ulikaa na ndugu zako sebuleni mkisubiri saa sita ifike mmshukuru Mungu ama mpige sherehe za shangwe za kuuona mwaka mpya?
Ulipatana na adui yako ama ulipotoka kwenye mkesha uliuchukia mwaka uliopita na kuanza kupanga mipango ya mwaka huu?
Huenda ulifanya mengi ama moja ya hayo au hukufanya chochote zaidi ya hayo.
Nakumbuka kwangu mwana mpya wa mwaka huu nilikuwa ndio kwanza najifunza kusherekea maana katika vitu ambavyo ninavyo ni pamoja na kusherekea.
Huwa naona kusherekea ni kama kujitoa ufahamu tuu na kuigiza kuwa huna shida wala tatizo lolote na kuungana na watu wengine ambao nao wanaigiza kama wewe.
Kwa nini naigiza? Kwanza naamini kuwa hakuna furaha halisi duniani kwani unaweza pata vyote unaanza kufikiria vipi wengine wenye shida je, itakuwaje nikifa? Basi naishia kutulia na kushindwa kuigiza.
Mwaka mpya huu nilijaribu kuigiza na kushangilia wakati natoka kwenye mkesha lakini nikashindwa kuendelea kuigiza nikajikuta nazama kwenye dimbwi la mawazo bila kujua kuna boda boda aliyekuwa akishangilia kwa namna yake akiendesha pikipiki yake kwa mwendokasi akanipitia na kuutegua mkono wangu wa kushoto lakini kwa bahati sikuumizwa sana na nikapona ndani ya wiki tatu na nusu.
Nilipofika nyumbani nikajifanya kusherekea tena huku nikichana kalenda ya mwaka uliopita nikilaumu kwa kuwa ni mwaka ambao niliteseka sana kwa kuumwa na mateso mengine nikiibusu kalenda ya mwaka huu kwa kudai kuwa ulikuwa ni mwaka wa furaha kwangu lakini hadi sasa mambo yameenda mrama na nusu ya mwaka huu ni wiki chache zijazo.
Wengi tunakuwa na matumaini makubwa mwanzo wa mwaka kama tuuitavyo mwaka mpya lakini ukweli ni kwamba hakuna jipya tarehe moja januari mwaka mpya zaidi ya muendelezo wa harakati zako za kimaisha.
Upya wako ni pale unapozaliwa japokuwa mwanzo huo hutanguliwa na maandalizi ya wazazi wako.
Rai yangu kwako ni kwamba nusu ya huu mwaka isikukatishe tamaa kwa kuamini hutotimiza malengo yako ya maisha baada ya kuona huna ulichokitimiza ama hata kukianza baada ya miezi sita.
Maisha yako hayakomi kufuata tarehe za miaka bali mipango ya Mungu juu yako kuishi.
NIANDIKIE MTAZAMO WAKO ‪#‎Mwanakalamu‬ mwenzangu

0 comments:

Post a Comment