Wednesday, 20 May 2015

UMEFANYA NINI KWA MAMA WA JUZI ,LEO NA KESHO?

Na.Moringe Jonasy
Husemwa kuwa nani kama mama , hapo wanajaribu kuuliza ni nani mwenye upendo kumzidi mama yako mzazi hapa Ulimwenguni( achana na wale wa mama punguani wenye kutupa watoto wao kwa kigezo cha ugumu wa maisha na sababu nyingine).

Utaumwa, utapata kilema na hata utafanya mambo ya kuaibisha wengi ambao ni marafiki na ndugu watakukwepa na kufurahia taabu zako wengine kuwa mashuhuda tuu kwa wengine wakisimulia matatizo yako, lakini mama atabaki upande wako.
Kwa kifupi anaweza asicheke nawe wakati ukicheka na marafiki na ndugu uchwara lakini yeye atakuwa anachekelea furaha uliyonayo akiwa chumbani, jikoni,anapoenda kisimani,sokoni ama ofisini kwake( japokuwa wengi tumezaliwa kwenye zama familia za baba wa ofisini na mama wa nyumbani) utakapolia na kuumia ye atalia ama kuumia kukuizidi. Kwa kifupi mateso yako mateso yake mara mia.
Umekimbiwa kimya kimya na mpenzi wako kisa ulemavu? Umetabiriwa mabaya kisa ugonjwa? Huna anayekupigia simu wala kukutumia ujumbe kwa kua anamini utamwelezea matatizo yako? Unamtafuta mama yako lakini kama mama alitangulia mbele ya haki basi unamwomba Mungu wakati mwingine unaweza kwenda kugalagala juu ya kaburi lake ukihitaji faraja.
Hakuna mwinine kati ya mama na Mungu yeye ni kiungo kati yako na imani.
Lakini licha ya huu ukweli umemfanyia nini mama yako?
Umemfanyia nini mama wa mwingine ambaye ni kiungo kikubwa cha imani?
Umefanya nini kwa mama wa baadaye ambaye kutwa haishwi kupigiwa miluzi na wanaotaka kumchezea kisha kumtupa?
Umefanya nini kwa mama wa baadaye ambaye anahaingaika kungombania usafiri awahi shule?
Hujafanya lolote? Hujachelewa sana anza leo wafanye mama kuwa miongoni mwa watu wenye furaha duniani.
Mfurahishe mama wa mwanao, mama yako , huyo unayemwona na kumwita demu ama mzee alopitwa na nyakati, mheshimu na umuombee kwa Mungu.
Hilo ndilo neno langu msije sema sikuwaambia wakati nilijua.

0 comments:

Post a Comment