Sunday, 24 January 2016

WASIKILIZAJI WA MUZIKI NI KAMA NDEGE WA RANGI MOJA

Na.Steven Mwakyusa (Mtu Makini)
Tokea kuwepo kwa maisha katika hii dunia, binadamu wamekuwa wakitafuta kila namna ya kufurahi na kuburudika (pengine ndiyo tafsiri ya maisha), katika kufanishikisha hili kumekuwako na burudani za kila aina kuanzia vichekesho, maigizo, michezo ya aina mbalimbali pia muziki!! Kati ya haya yote muziki umetokea kuwa ndiyo kitu kinachosikilizwa karibia na kila mtu katika hii dunia( hapa haijalishi ni aina gani ya muziki ambao mtu anausikiliza). Hivyo basi muziki ndiyo burudani inayoongoza kwa kuwa na wapenzi wengi katika pande zote za dunia!

Katika huo huo muziki kuna aina lukuki kuanzia Rap/Hiphop, RnB/Soul, Zouk, Pop/Rock, Blues, Metal, Hard Rock, Electro/house, Jazz, Reggae,Taarabu, mduara, dansi, Bongo Flava, country, Bolingo na aina nyingine nyingi!!

Katika usikilizaji huu ndipo tunakuja kutofautiana pale ambapo unaweza ukawa unasikiliza aina fulani ya muziki na mtu akakushangaa kwamba unasikiliza vitu gani?? Na katika huo huo muziki unaweza ukawaona wasanii ni wakubwa lakini mwingine asiwajue hata kwa majina yao achilia mbali hits zao na tuzo wanazobeba kila siku!

Kwa mfano mimi mbali na Bongo Flava na RnB nasikiliza sana Pop/Rock, na nikijua pia mtu anapenda pop/rock namuona kama ndugu! Sina miaka mingi toka nimeanza kusikiliza aina hii ya muziki ila nimekuja kugundua nilikuwa namiss burudani ya kipekee!! Hii imenifanya nifukue albam za sasa mpaka za miaka ya nyuma!! "Firework" ya Katy Perry ambayo niliisikiliza accidentaly ndiyo ilifanya nihamie huku moja kwa moja!!

mpaka sasa Taylor Swift, Katy Perry, Miley Cyrus, Avril Lavigne, Adele, Bruno Mars, Sam Smith, Ariana Grande, Ellie Goudling, One direction, Kelly Clarkson na Jessie J naowaona ndiyo wasanii bora wanaoendelea kufanya vizuri na kutoa burudani ya uhakika!!

Vivyo hata ukienda kwenye Hardrock/metal nako kuna wababe wake kama Epica, Metallica, Anvil, Paradise Lost, Def Lepard, styx, Scorpions pia Trivium!! Vivyo hivyo hata kwenye country, Rap au metal kuna watu wanaotawala huko ambao kama hufatilii muziki husika ni ngumu kuwafahamu!!

Hivyo basi si busara kukaa na kumshangaa mtu kwanini anasikiliza hiki, wakati hata unachosikiliza wewe pengine wengine hata hawakijui!!

Mwisho niwakaribishe kwenye muziki wa Pop/rock maana ni burudani ya aina yake, pia kama kuna burudani nyingine ambayo siyo popular hapa kwetu kama Country
naweza nishawishi pengine kuna kitu nakikosa!!

0 comments:

Post a Comment