Sunday, 2 October 2016

Ya Kajiandae na Nai Nai... Je historia kujirudia??


Na Steven Mwakyusa (Mtu Makini)
Jina la Ommy Dimpoz lilianza kusikikika miongoni mwa walio wengi miaka ya 2010 baada ya kuimba kibao matata kwa wakati huo kilichokwenda kwa jina la Nai Nai.. Ndani ya NaiNai kulikuwa na sauti ya Alikiba ambayo kwa upande mwingine iliwavuta wengi kutaka kujua hasa huyu Ommy ni nani?? Nainai iliweza kuteka soko la muziki na kumuweka Ommy katika ramani ya muziki!!

Ommy hakulala kwani aliendelea kutikisa na vibao kama Baadaye,  Tupogo aliyoimba na Jmartins,  Me & u ambayo iliweza kumtambulisha Vanessa Mdee pia Ndagushima na Miss Koi koi (ambayo haikuwa official release) ziliendelea kuwa hits zilizosumbua sana!!

Ilifika wakati kila msanii akatamani aimbe na Ommy,  kwa uchache Steve Rnb na kibao chake cha radio alifanya vizuri huku Number One ya Nemo nayo ikipasua anga la Bongo Fleva achilia mbali Chukua time ya Summa Mnazareth na Utamu ya Dully Sykes!!

Kuna wakati Ommy alisakamwa sana na vyombo vya habari za udaku wakati wa msiba wa Mangwea kwa kauli yake kwamba hataki kufa maskini na wamechoka kuzika wasanii maskini,  Ommy alishikiwa bango kwamba kamtukana Ngwea,  hivyo jina La Ommy likaendelea kusumbua vichwa vya habari vya magazeti pendwa na mitandao ya kijamii pia!!

Miaka ilisogea, Ommy alionekana akiwa na Tuzo za Alikiba kwenye tuzo za KTMA,  Baadaye tukasikia kaimba Wanjera ambayo ilishindwa kufua dafu mbele ya kazi zake zilizotangulia,  Achia body ni ngoma iliyofuatia lakini bado trend yake ikazidi kushuka chini!!

Sasa ni kama Ommy kashtuka kwamba anakoelekea siko,  ndipo akaamua kurudi alikotokea mwaka 2010 na NaiNai.. Hapa ndipo ikasikika project ya #Kajiandae humo ndani akiwemo yule yule aliyemuweka Ommy kwenye ramani ya muziki!

#Kajiandae imewakutanisha kwa mara nyingine Ommy Dimpoz na Alikiba.. Je tutegemee nini toka kwa hawa wawili?  Je watavunja rekodi ya NaiNai au uteam utaenda kuwabeba??

0 comments:

Post a Comment