Saturday, 17 May 2014

USHAIRI: BE BEST IN BEST HOPE


Ukiweka  lako lengo,lazima ulitumai,
Ukiifata mipango,kusaka hutokinai,
Hata vya ndani ya pango,kupata hatushangai,
Weka lako tumaini, kwenye  kila lengo lako.

Hilo litakupa nguvu,kupata ukipangacho,
Shuleni ama kazini,hakuna ukikosacho,
Kama vile yako mboni,itunzavyo  lako jicho,
Weka lako tumaini,kwenye kila lengo lako.

Pia kushinda vikwazo,uvikutavyo njiani,
Tumaini ndiyo nyenzo,huwezi kwama njiani,
Hukuza wako uwezo,pia kukupa imani,
Weka lako tumaini,kwenye kila lengo lako.

Hata mandiko yasema,kutumai jambo jema ,
Siseme wananisema,ukaacha kusimama,
Utawashinda daima,wakakosa lakusema,
Weka lako tumaini,kwenye kila lengo lako.

Sisi hapa twatumai,wewe kuvipata bora,
Kaoza hatushangai,ukisema  sisi bora,
Hatuji kusema bai,hata tuchapwe bakora,
Weka  lako tumaini ,kwenye kila  lengo lako.

Tumaini likidumu,tutafika tutakako,
Kwenye swala la elimu,pia huko kwingineko,
Tumaini ni muhimu,liwe kila siku kwako,
Tumai ukatumai,ukapata kicho bora.

0 comments:

Post a Comment