Sunday, 18 May 2014

USHAIRI: ULIPENDE JINA LAKO, SITAMANI LA MWENZAKO


                JINA
Mie alinipa baba,na leo nimelipenda,
Hata angenita zoba,singemwona aniponda,
Maana lililobeba,ndiyo yeye kaipenda,
Ulipende jina lako,sitamani la mwenzako.

Eti lile maarufu,nami nitafanania,
Kaliona uchafu,mama alokupatia,
Nawe uwe maarufu,wengine kuwavutia,
Ulipende jina lako sitamani la mwenzako.

Mie langu nalipenda,popote nitalitaja,
Hata wakija niponda,eti walone kioja,
Na kamwe siji kukonda,watachoka kuningoja,
Moringe ninalipenda,japo simjui Morani...

0 comments:

Post a Comment