Thursday, 2 October 2014

ZAWADI KWA DIAMOND PLATNUMZ: UISHI MIAKA MINGI

Kwanza nikupe salamu,kaka yangu almasi,
Leo nashika kalamu,siombi kazi kwa bosi,
Japo kwako ni vigumu,vya kusoma huvikosi,
Uishi miaka mingi,Mungu akupe hekima.
Dangote sijui Chibu,nijuavyo ni Nasibu,
Sitaki nipe jawabu,kuna wengi wa kujibu,
Si lazima iwe Dhahabu,hata salamu thawabu,
Uishi miaka mingi,Mungu akupe hekima.
Sikujui kiundani,si lazima kwenye hilo,
Kazi ya wako mwandani,najua wajua hilo,
Sie tuko redioni,twangoja wako ujio,
Uishi miaka mingi,Mungu akupe hekima.
Najua wengi watega,kujua wapewa nini,
Wala usiwe muoga,kipewa hata sabuni,
Upendo uzidi kunoga,na muingie ndoani,
Uishi miaka mingi,Mungu akupe hekima.
Mwisho nimeufikia,nisikuchoshe kusoma,
Mema ninakutakia,nazipenda zako ngoma,
Siogope kuchukiwa,ukipata vyawauma,
Uishi miaka mingi,Mungu akupe hekima.

0 comments:

Post a Comment