Thursday, 7 August 2014

KWA WAKO UMPENDAYENIKUACHE NENDE WAPI
Nasema nina imani,nimependa sitamani,
Penzi lile la zamani,zidisha mara sabini,

Nataka twende nyumbani,nimekuweka moyoni,
Nikuache nende wapi,nipo nawe siku zote.

Yasemwa mi limbukeni,eti sina nguvu tena,
Kama kusema semeni,nampenda tena sana,
Hizo chuki zidisheni,sie huku twapendana,
Nikuache nende wapi,nipo nawe siku zote.

Simfwati wa zamani,mama ukinikosea,
Ukisema samahani,jua nitapotezea,
Akija wako wa zamani,mwambie amepotea,
Nikuache nende wapi,nipo nawe siku zote.

Juzi mama aongea,vipi hutaki kuoa,
Nilipo kuongelea,mama alichekelea,
Asema nimepatia,wewe mke wa kuoa,
Nikuache nende wapi,nipo nawe siku zote.

Wakikuonesha mali,sema mali zetu twazisaka,
Tutapata zetu mali,na pesa kuja kushika,
Si za urithi mali,za kwetu tunazotaka,
Nikuache nende wapi,nipo nawe siku zote.

Mwisho mama angalia,wakora wakumezea,
Wengine wakutishia,mama watakuchezea,
Marafiki angalia,wivu wanakuonea,
Nikuache nende wapi,nipo nawe siku zote

0 comments:

Post a Comment