Wednesday, 30 July 2014

KUMBUKUMBU YA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE


LEO UNGEKUWA NANI?
Sasa miongo mitatu,wajina hatukuoni,
Wanalalamika watu,kama wewe hawamwoni,
Kuvaa vyako viatu,katu haiwezekani,
Leo ungekuwa nani,Moringe wa sokoine,


Wengi wasema raisi,wa muungano wetu,
Eti nawe ungeasi,kukiacha chama chetu,
Angekuona raisi,utunge katiba yetu,
Leo ungekuwa nani,Moringe wa sokoine.


Alokufwata monduli,tunaambiwa fisadi,
Chamani hawamjali,yuko bize na miradi,
Ilikuua ajali,kukukosa ilibidi,
Leo ungekuwa nani,Moringe wa sokoine.

Nimefika morogoro,ulipopata ajali,
Kule kuna mogogoro,leo ardhi mali,
Ninapatwa na kihoro,kuhusu yako ajali,
Leo ungekuwa nani,Moringe wa sokoine.

Nitakuja kutazama,mahali ulipolala,
Kisha nende Butiama,nyerere alipolala,
Moyoni inanichoma,sijakuona mahala,
Leo ungekuwa nani,Moringe wasokoine.

Najuta sijakuona,mie wale wa tisini,
Nimepewa lako jina,nalitumia shuleni,
Kwenye picha nakuona,nimetunza chumbani,
Ulazwe pema peponi,Moringe wa jina wangu......

0 comments:

Post a Comment