Tuesday, 29 July 2014

MWAWATUMA WAKAIBE

MWAWATUMA WAKAIBE
Habari za leo rafiki,nina neno dogo kwenu,
Mie sina unafiki,hili nalileta kwenu,
Najua mtaafiki,nalosema mwenzenu,
Mwawatuma wakaibe,napenda waibe kwenu.

Juzi nipo safarini,hili nilishuhudia,
Niliumia moyoni,mie ningemlipia,
Sijui kauza nini,kalizwa nashuhudia,
Mwawatuma wakaibe,napenda waibe kwenu.


Nakumbuka njia panda,wa moshi mnapajua,
Mama basi amepanda,kuna kitu kanunua,
Kumlipa hakupenda,chenji inamsumbua,
Mwawatuma wakaibe,napenda waibe kwenu.

Mara gari laondoka,mama hakulipa pesa,
Kweli nilihuzunika,mama heshima kakosa,
Kweli alidhurumika,kwa bosi wake ni kosa,
Mwawatuma wakaibe,napenda waibe kwenu.

Mtu amesaka kazi,ili asije kuiba,
Sisumbue wazazi,pia mizigo abeba,
Wamwibia waziwazi,sijute kiwaibia,
Mwamtuma akaibe,napenda aibe kwenu.

JAMANI MUWE NA UTU,THAMINI KAZI YA MTU.

0 comments:

Post a Comment