ads

Sunday 27 July 2014

SI KAMA MUNGU NA SHETANI

SI KAMA MUNGU NA SHETANI
Moja ya maswali magumu ambayo nilipata ugumu kuyajibu lilikuwa ni Nani niliyempenda kati ya mama na baba lakini nilipofikia umri Fulani nilijikuta najibu kuwa nawapenda wote kwani si dhambi kama kumtumikia mungu na shetani kwa pamoja.
 Juzi alfajiri  nikiwa  usingizini nilishtushwa na  sauti ya simu yangu ambayo ilionesha nimepokea ujumbe kupitia whatsap na nilipoangalia nilikuta umetoka kwa mtu  mmoja Makini Stephen Mwakyusa ulikuwa ni  wimbo na ujumbe mwingine  uliandikwa UJIO WA KIBA  nilijikuta nafurahi kabla hata ya kuusikiliza wimbo ule ambao maelfu ya waafrika waliusiri  usiku kucha kuusikia mara tuu utakapoachiwa.Mtandao kusuasua  na simu kukata chaji ndivyo vilivyonipelekea kuusikiliza ule wimbo saa moja na nusu asubuhi  
Tangazo la voda  lilipoanza nilijikuta naanza kujiuliza kilichomo halafu zile sauti za vyombo vya Combination sound  zilinifanya  nimkumbuke Alikiba ,alikiba Yule wa Njiwa ,cindelera na my everything  lakini  nilijikuta natokwa machozi ya furaha mara nilipomaliza kuusikiliza  ule wimbo kwa mara ya pili  ‘’kweli amerudi ‘’Nilimjibu mMwakyusa kwa ujumbe  huku nikiona kama hautomfikishia hisia zangu zote  niliona nimpigie tuu.
  Sipo hapa kumsifia Alikiba na ujio wake bali kujaribu kuliongea hili jambo ambalo mimi kama msikilizaji na mpenzi wa muziki wa bongo  naona litatupeleka tusipotaka kufika .
  Kwa muda mrefu Alikiba alikuwa kimya huku watu wakiongea hili na lile juu sababu iliyomfanya asitoe wimbo wake jambo ;lililochangiwa na watangazaji wengi kwani hawakuisha kumuulizia lakini swali lao lilikuwa na jambo ambalo linaniweka hapa leo hii.
‘’Vipi huoni Diamond atachukua nafasi yako, Kwa nini usifanye kazi na Diamond? ‘’ Na mengine mengi yamekuwa  maswali ambayo si tuu yanakera lakini pia yanatengeneza kile mkiitacho BIFU kati yao yaani ni kama  Mwalimu kumfuatilia mwanafunzi hadi siku atajikuta anakosea ndicho kilichotokea wanablog wakalishupalia jibu la kiba kuwa kiti chake kina vumbi kama ni bifu  hahahaaaaa!  Mnachekesha ndugu zangu  hilo jibu siyo jungu wala bifu ni  jibu zuri na sahihi kutokana na swali walilouliza.
 Si waandishi na mashabiki wa mziki kwa pande zote(sijui nani kazitengeneza) Wamekuwa wakitumia lugha mbaya kumsiliba mmoja katio ya Diamond na Alikiba  kutokana tuu na mitazamo yao.
  Hawa watu ni wasanii ambao tunatakiwa kujivunia licha ya tofauti ndogo (ambazo waandishi wanatulazimisha kuamini kama zipo), wamefanya kazi kubwa katika  kuinua muziki wetu ambapo kila moja
kwa wakati wake ameliwakilisha taifa letu kama siyo Afrika mashariki katika anga la kimataifa  sasa hizi chokochoko twazitoa wapi watanzania?
 Juzi baada ya kiba kutoa wimbo wao Diamond akatukanwa matusi eti mfanya biasha mara mtu wa scandal  na mengine mengi kama scandal zinasababisha waatu wapate mafanikio aliyoyapata Diamond kwa nini wengine wasifanye afanyazo na kuhusu kuwa mfanyabiashara  kwani ni dhambi kufanya hivyo, wengine wanafanya muziki kwa malengo yepi?  Tukubali tukatae lakini muziki unabaki kuwa biashara  na burudani kwa upande wa pili kwani kama watu hawaburudiki  na kazi zako sidhani kama waweza kufanya biashara.
  Leo Diamond katwaa tunzo tumeanza ‘’Alikiba atasubiri mara sijui hamfikii’’  na maneno mengi ambayo yanatengeneza picha mbaya hasa kwa tunaopenda kazi za Alikiba na Diamond. Kwa nini tusiwapende wote , hatakama hatuwezi kufanya hivyo tusisubiri kuumizwa na mafanikio yao tukajifungia ndani .Alikiba licha ya  kuonekana amefulia lakini anabaki kuwa msanii ambaye  naamini hata akae miaka mitano bila kutoa  wimbo lakini kwa kipaji alichonacho atapokelewa na wafuasia aliowatengeneza  na wakiongezeka wengine.
  Nawaomba watanzania ,hasa wafuatiliaji wa muziki wetu hatuna haja ya kuwatukana hawa watu  ambao wamejijengea heshima katika muziki huu  alikiba amewatoa wasanii wengi ambao sidhani kama tungewasikia lakini amekuwa ni miongoni mwa wasanii wachache ambao wamedumu muda mrefu akiungana na Dully sykes ,pro  jay ,fid q, juma nature  na wengine wengi kama j mo.Wakti Diamond amekuwa msanii wakwanza wa bongo fleva kuvunja rekodi nyingi alizoziweka  a,mbazo zinamweka juu kila siku jambo linalonifanya niamini ni mwisho wa chamilione kutawala Afrika mashariki.
 Si dhambi kuwapenda wote kama ilivyo kumtumikia mungu na shetani.
Huku Mdogo mdogo huku Mwana lazima nijivunie kuwa mtanzania….
        Naomba kuwasilisha
Moringe Jonasy Mhagama






0 comments:

Post a Comment