Sunday, 27 July 2014

HAPPY BIRTHDAY MY BROTHER

MUNGU AKUPE HEKIMA
Miaka mingi imepita,tangu uziache nepi,
Hekima umezichota,na kuyaacha makapi,
Na mengi umeyapita,sijui myaka mingapi,
Mungu akupe hekima,kaka yangu Tumsifu.

Kama vile jina lako,Mungu wetu twamsifu,
Mema yote yaje kwako,na ujazwe utukufu,
Pongezi za ndugu zako,kamwe zisije kukifu,
Mungu akupe hekima,kaka yangu Tumsifu.

Mama amepata mwana,mwana mwema naamini,
Hasemi mtundu sana,bali unajiamini,
Wewe kaka ndiwe shina,nduguzo twakuamini,
Mungu akupe hekima,kaka yangu Tumsifu.

Baba anajivunia,kuwa nawe kila siku,
Kwa watu kujisifia,atamani uwe huku,
Kakangu unatulia,huna papara za kuku,
Mungu akupe hekima,kaka yangu Tumsifu.

Mwisho njoo kalamuni,wataka vitu jamani,
Wakutaka hadithini,ubuni picha jamani,
Wasema uje ubuni,ukuze yako thamani,
Mungu akupe hekima,kaka yangu Tumsifu

0 comments:

Post a Comment