MWANDISHI;MORINGE MHAGAMA
MSIMULIAJI;GODWIN
Miale ya jua ilimulika ikipiga mapaa kutokea upande wa magharibi
kuashiria machweo yalikuwa yakichukua nafasi weakati huo.Sauti za watoto
wakicheza nje ya nyumba zao ziliongeza uhai wa eneo lile, mbuzi nao
walikuwa wakirudishwa mabandani mwao na wamiliki ama vibarua waliokuwa
wameletw akuishi pale kwa ajili ya kazi hiyo.
Nyasi za kijani kibichi pamoja na majani ya kiti mirefu ya kupandwa yalikuwa yakipelekeshwa na upepo huku na kule kadiri ulivyotaka .
Sauti za matairi ya magari yaliyokuwa yakisugua barabara ya lami
zilisikika kutoka mbali huku sauti zikerazo za pikipiki zikisikika kama
vile zikishindana na na sauti za ngurumo za magari makubwa.Honi za
pikipiki na taksi zilisikika si kutaka kupishwa bali kusaka abiria ambao
wengi walikuwa wakitoka kazini na wachache walikuwa wakiiingia kazini.
Kina mama na mabinti zao walisikika wakipepeta mchele na kuagizana
vibandani kununua viungo ambavyo ama havikununuliwa ama havikutosha ,
huku akina baba nao wakiwa na vijana wao wa kiume wakimwagilia bustani
na kuchuma mboga za majani ambazo walipenda kudai kuwa walikuwa
wakizipalilia kw akupunguza majani yaliyokuwa yamezidi.
Wakati hayo
yakiendelea, ndani ya nyumba moja kuna kijana alikuwa amekaa tuu
akisikiliza muziki ambao hata baada ya umeme kukata na redio kuzima
aliusikia ule muziki huku akiimba kwa kumung’unya maneno ambayo
hakuyakumbuka. Mwalimu Godwin Joseph alikuwa akiendelea kuimba nyimbo
za msanii wa Bongo Fleva Sam wa ukweli ambazo alikuwa akizisikiliza
kabla ya umeme kukata bila kujua kuwa kulikuwa na mtu aliyekuwa
akigonga mlango wa nyumba yake kwa muda mrefu hadi aipochukua uamzi wa
kuingia pale ndani.
‘’Shikamoo mwalimu’’Alisalimia Kurwa mwanafunzi wake shuleni Njombe sekondari ambaye kwa kipindi hicho alikuwa likizo.
‘’ Mhh-m-maa-Marhhabaa vipi umegonga sana?’’Alibabaika Godwin akisugua
macho yake yalikuwa makubwa kama ma apple ya Uwemba kwa viganja vyake
vilivyonyimwa nyama za kutosha kushikilia viunzi .
‘’Ndiyo
mwalimu Sikai sana kuna barua yako amenipa mkuu amesema ilitumwa kwa
anuani ya shule’’Aliongea Kurwa akimpa barua iliyokuwa imewekwa kwenya
bahasha iliyovutia kwa rangi na urembo wake.
‘’Asante sana karibu
Soda ipo kwenye jokofu fungua hapo jihudumie’’Aliongea Godwin
akielekeza kidole kwenye jokofu lililokuwa limejee pombe nyingi ingawa
hakuwa mnywaji wa pombe alipenda sana kuwawekea rafiki zake ambao wengi
walikuwa wakipenda kunywa pombe.Alikuwa amejaribu kunywa pombe zaidi ya
mara nne lakini aliishia kutapika na kupata homa hivyo akaamua kuachana
nayo zadi ya kuzitazama kwenye ndani ya jokofu lake.
‘’Asante mwalimu kuna mtu nilikuwa na miadi naye namuwahi’’Alijibu Kurwa akifungua mlango na kutaka kutoka.
‘’Vipi shem nini? Maana watoto wa uzunguni ukiwakosa wakiwa na nafasi
basi utasubiri mwaka tena unakuja kumwona na mshikaji mwingine wahi
bhana’’Aliongea Mwalimu Godwin akicheka.
‘’Hapana mwalimu , baadaye
nitakuja tuongee’’Kurwa akiongea akiwa nje ya ile nyumba.Alimzoea
mwalimu wake wa Geography ambaye alikuwa ni kama rafiki yake tuu lakini
alikuwa akimficha sana juu ya masuala ya mahusiano kwani licha ya
mwalimu wake kupenda sana nyimbo na tamthilia za mapenzi hakuwahi
kumwona akiwa na mpenzi wala kusikia akimwongelea, alijua labda kwa
kuwa aikuwa akimwona kama mwanafunzi hivyo aliamua kumficha.Kauli ya
kumwambia kuhusu wasichana wa uzunguni ni kweli wana tabia kama zile ,
je miezi tisa aliyokaa Njombe ilitosha kuzijua tabia zao bila
kujihusisha nao?. Hayo ni baadhi ya mambo aliyokuwa ametoka nayo Kurwa
kwa mwalimu wake ‘’msela’’ kama alivyokuwa akiiitwa na wanafunzi wake
bila kujua.
Mwalimu Godwin alijikuta akipata kigugumizi kuifungua
ile barua ambayo kwa mwonekano wake ilikuwa ikionesha kabisa ni suala la
mapenzi lilikuwa ndani mwake lakini ni nani ambaye alikuwa ameiandika,
kwa nini atumie anuani ya shule?, kwa nini aandike barua badala ya
kumpigia simu? Hakuifungua ile bahasha nzuri ambayo kuifungua tuu
kungekuwa kama kuharibu nakshi zake zaidi ya kuigeuza geuza pengie jina
la mwandishi wa barua lingeandikwa nyuma ya ile barua lakini hakuona
chochote zaidi ya nakshi za’ I Love You’ zilizokuwa na maua ya kuchorwa
na kubandikwa.
Mra simu yake ilionesha kuwa palikuwa na ujumbe
uliokuwa umeingia akawahi kama kibaka akikwapua mkoba wa ‘ Sister Duu’
na kufungua ujumbe ambao akili mwake alijua utakuwa umetoka kwa mtu
ambaye ana wiki mbili hapatikani simuni alitamani kupata ujumbe
wake.Alitamani kusikia kilichomfanya asipatikane , alikumbuka kuwa mara
ya mwisho kuongea naye walibishana juu ya jambo fulani na simu
ilipokatwa na huyo mtu haikupatikana tena.
‘’NDUGU MTEJA KIFUSHI
CHAKO CHA CHEKA KIMEKWISHA, SASA UNAWEZA KUONGEA BURE BAADA YA DAKIKA
TATU ZA KWANZA, asANTE KWA KUTUMIA VODACOM’’
Ulisomeka ule ujumbe na
kumfanya asonye kwa sauti , hakutegemea kukutana na ujumbe ule aliouita
wa kipumbavu kwani kila muda ule ulikuwa ukiingia simuni mwake na
alijiunga tena na huduma ile kwa matarajio ya kumpata mtu ambaye wiki ya
pili alikuwa akimtafuta simuni bila mafanikio.
Akiwa na na hasira
juu ya ule ujumbe simu ujumbe mwingine uliiingia na haraka haraka
akaufungua na kukutana na kitu ambacho pia kilimkera.
‘’NMB
INAKUKUMBUSHA KUHAKIKISHA TAARIFA ZAKO ZA BENKI KABLA YA MWAKA KUISHA
KUEPUKA USUMBUFU WA KUFUNGIWA AKAUNTI YAKO’’ TUNAKUTAKIA SIKUKUU NJEMA
YA X-MASS NA MWAKAMPYA’’
Baada ya kuusoma ujumbe huu wa pili
ulimkera ukampa mwanga fulani juu ya ile barua aliyokuwa ameipokea
alijua lazima itakuwa ni kadi kwa ajili ya kumtakia sikuu njema , lakini
hakuweza kutabiri aliyekuwa amemtumia kadi hiyo.
Aliifungua ile
bahasha kwa umakini mkubwa, lakini ujumbe mwingine uliingia simuni ,
huku akisonya sonya alifungua tena ujumbe ule huku akitegemea kitu
ambacho kisingemkera lakini baada ya kusoma alijikuta akiongea
mwenyewe.
‘’Haya mameseji yao ya kudownload yananiboa’’alifuta ule
ujumbe bila hata ya kumaliza kusoma , ulikuwa ukihusu kuisha kwa mwaka
na kuanza kwa mwaka mwingine.
Akairudia tena bahasha na kuifungua
yote ambapo aikutana na picha ya mtu aliyekuwa akiisubiri simu na
meseji yake kwa takribani wiki mbili na barua ambayo aliifungua kwa pupa
kama mtoto afunguavyo zawadi iliyofungwa kwenye boksi.
CHUO KIKUU CHA MWENGE
S.L,P 2676,
MOSHI.
17/012/2014
Mpedwa Godwin
Salamu nyingi zikufikie hapo ulipo ,najua u mgonjwa kwa kunikosa
hewani kwa zaidi ya wiki moja ila kwa upande wangu bado si mzima tangu
uliponiachia homa yako kali ya Upendo.
Matilaba ya barua yangu ni
kutaka kukuambia mambo machache ambayo naamini unatakiwa kuyajua hasa
katika kipindi hiki kigumu ulichonacho.
God unajua jinsi gani
nakupenda na unavyonipenda hata kabla hatujaambiana habari za mapenzi
lakini pia najua hujui kuwa kuna mtu ambaye nampenda zaidi yako tana
mbaya zaidi huyo mtu tumefahamina miaka miwili baada ya penzi letu.
Naamini nawe unamjua kwani mara nyingi umekuwa ukinikataza
kujihusisha naye japokuwa mara nyingi nimekuwa nikikwambia kuwa pendo
langu kwake halitaharibu mahusiano yetu lakini umekuwa kaidi na
kuniambia kuwa nikitaka kumpenda basi nisiwe nawe kwani sikusikilizi
kisa huyo mtu kitu ambacho nikuambie tuu ukweli kuwa SIWEZI KUACHA
KUMPENDA.Niampenda na nitampenda japo nawe nakupenda sana .
Pengine
unaweza ukawa unaisoma barua hii kwa kuacha na kuendelea kwa hasira ,
kwani nakufahamu God wangu nikupendaye mwanaume wangu wa kwanza na wa
mwisho lakini kwa hali hii naamini hutokuwa wa mwisho.Nikupendaje we
mwanaume? Nimekataa vingapi kwa ajili yako we mwanaume? Mara ngapi
nimeishi kwa mashaka baada ya kuwakataa wenye mamlaka na pesa zao kwa
ajili yako? Kwa nini unapenda kunitukana na kunilaumu kwa kukataa
kukubaliana nawe juu ya kuwa na huyu mtu nimpendaye siku zote UANDISHI
WA HADITHI FACEBOOK NA POPOTE PALE ndiye mtu nimpendaye pengine zaidi
yako lakini sijui wivu , chuki na lawama zako juu ya suala hili
limekufanya unitishie ama uniache zaidi ya mara tano kwa sababu ya huyu
mtu.
Pengine unaamini nikiwa maarufu kwa kuandika hadithi
nitafuatiiwa na wengi, lakini ujue nimefuatiliwa na wengi sana hata
kabla sijaanza kuandika hadithi na nikabaki nawe. Au sijakuelewa huenda
ni sababu yako ya kutaka kuniacha na kuwa na mwingine umpendaye zaidi
yangu?. Sawa nitabaki na Huyu nimpendaye kwani kila uniumizapo amekuwa
akiniliwaza na kujikuta nasamehe bila masharti yoyote lakini unamwona
ni adui wa penzi letu.
Mwisho nikuambie nimeamua kuwa naye huyu na
sitokuwa nawe hata uje na mtazamo upi kwani umeniumiza sana maksudi
kwa kigezo cha kuwa sikupendi kwa sababu sikusikilizi , je wewe
usiyetaka kunisikiliza unanipenda, Au imeandikwa asikilizwe mmoja tuu?.
We si yule ambaye ulijafanya uko bize na kazi ya kufundisha wakati
facebook upo bize ukipeana miadi na wasichana wako wengine na
mkibadilisha namba na wasichana hao miongoni mwa namba unayowasiliana
nayo sana ni yangu nimetumia jina la Bitric Jochim, umeshtuka ehee we si
ulisema bado humjui msichana mimi Bhoke Binti Joshua hukunivua nguo
zangu? Sawa baba endeleza ujogoo wako tukuzike na kilo mbili.
Siongei sana baba nikutakie sikuu njema ya krismass na mwaka mpya 2015
ila usisahau kunitumia zawadi ulosema unanitumia kwa jina la Bitric.
Aliyekupenda……..
Bhoke Joshua Masatu…
Godwin aliirudia ile barua akiruka ruka maneno na kujikuta akilia
alishindwa pa kuanzia juu ya jambo lile ambalo aliona ni gumu kuliko
mambo yote aliyowahi kukutana nayo.
JE WEWE UNGEMSHAURI NINI?
0 comments:
Post a Comment