Friday, 29 May 2015

UNAPOJISAHAU NA KUJIONA KOBENa.Moringe Jonasy
Niliwahi kusoma na rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa akipenda kunukuu kauli ya wahenga kuwa '' Uzee haukwepeki''.Alikuwa akipenda kutumia kauli hii hata pasipokuwa na ulazima wa kuisema lakini kwangu ilikuwa na maana sana.
Nakumbuka simu moja alimwona mwanafunzi mwenzetu aliyekuwa na umri mkubwa na ndevu nyingi akinyoa ndevu zake mara kwa mara hali iliyomfanya awe na videvu visivyo na ndevu kama sisi tuliokuwa tukiitwa watoto lakini tofauti ilikuwa katika ukomavu wa kidevu chake.
Nimeanza na kisa cha huyo rafiki yangu kwa lengo moja tuu la kukumbusha kuwa uzee haukwepeki labda kwa kifo.
Mara ngapi umeshuhudia mtu akimtenga mzee kwenye mazungumzo na kumwona amepitwa na wakati?
Mara ngapi umeshuhudia wazee wakifanya kazi zinazoonekana za dharau kama kufagia barabara licha ya vijana wenye nguvu zao kuwepo na hawana kazi za kuwaingizia kipato?
Hahaaa atafanyaje kazi hiyo wakati ni Brazemen ama sista duu? Hizo kazi za aibu bwana.
Si ndivyo wasemavyo? Ila kwa wenzetu ng'ambo mtu anaweza kujivunia hiyo kazi.
Haya labda nikuuulize mara ngapi umewaona wazee wakiteseka kufanya kazi ngumu kama kulima kwa jembe la mkono huku wajukuu zao wakitumia jasho lao kujipendezesha?
Inawezekana hujui kwa kuwa upo mjini lakini kule kwetu ni kawaida kumwona brazamen Juma akidunda mtaani huku bibi anayekaa naye hana hata mafuta ya kulainisha ngozi yake japokuwa ndiye msuka mikeka anayoiuza na hela ndo anayotanulia Juma pia kule si ajabu kumwona Rose aking'aa na kuwatatanisha akina Fred kwa nguo ambazo hela yake ilikuwa ya kunulia mboga nyumbani.
Na wazee hao wanakubali na kusema ''ndo ujana huo lazima wapendeze , ni wakati wao''
Mara ngapi umesikia mzee akilaal;ikiwa kuwa ni mchafu wakati licha ya kutokuwa na uwezo wa kufuata maji bombani ama kisimani kwa ajili ya usafi ama hata uwezo wa kujisafisha mwenyewe hana wakati amezungukwa na watu wenye uwezo wa kumsaidia ?
Au ni mara ngapi umeshuhudia babu wa watu akikosa huduma hospitalini kwa kukosa fedha licha ya serikali kutaka watibiwe bure?
Labda jiulize ni mara ngapi umesikia wazee wakiuawa kisa wana macho mekundu kwa kuhisiwa wachawi wakati ukweli ni kwamba matumizi ya nishati ya kuni yamewapa mateso hayo?
Masikini babu/bibi wa watu badala ya kupata tiba ya macho anauawa,,,
ndo Afrika hii inayowalaumu wazungu kuwatawala na kuwapa kasumba kibao zinazosababisha migongano bila kufikiri ujinga wetu ambao wazungu hawakufanikiwa kuutoa hadi wakati wanaondoka tunawaua wazazi wetu kwa imani za kipuuzi ona sasa tumerejerea kuwaua Sope(albino) kwa kudanganywa na weusi wenzetu eti utajiri.
Leo wazungu wanajiri watu wawahudumie wazee wao kwani wanajua uzee haukwepeki lakini kwetu TUNAJIHISI KOBE KUWA HATUTAZEEKA DAIMA ila tujue na hizi nakshi zetu za kemikali tutazeeka vibaya sana na kuwafanya watoto wetu waamini kuwa tulitokana na SOKWE.
Unasemaje
‪#‎mwanakalamu‬ mwenzangu niandikie hapa chini.

0 comments:

Post a Comment