Friday, 29 May 2015

YA ALIKIBA NA TAYLOR SWIFT NA KINACHOITWA KUVUNJA REKODI!!

Na.Steven Mwakyusa
Jambo lolote linapofanyika nje ya mazoea basi ni kawaida kuacha maswali yanayojibika na yasiyojibika pia!! Kwingineko huitwa kuvunja rekodi, hivyo mtu anaweza vunja rekodi yake mwenyewe au zilizowekwa na wengine!!
Hapa nyumbani tuna tuzo ambavyo zimejijengea heshima kubwa mpaka sasa, si nyingine bali tuzo za KILI. Licha ya kuwepo malalamiko Lukuki kam zilivyo tuzo nyingine duniani hili bado halijazuia wao kufikia malengo waliyojiwekea! Wakati naangalia nomination za tuzo za KTMA nilipata pia wasaa wa kupia nominees za tuzo za BILLIBOARD pia washindi waliopatikana usiku wa may 17!!
Katika tuzo za KTMA Alikiba ametokea katika category 7, 6 zikitokana na wimbo wa Mwana huku uliobakia ikiwa ni Kiboko yangu alioshirikishwa na Mwanafa!! Hii inakuja baada ya kimya cha takribani miaka mitatu, wimbo mmoja category 6 kwa maana ya
1. Wimbo bora wa mwaka
2. Wimbo bora wa Afro pop
3. Video bora ya mwaka
4. Mtunzi bora wa mwaka
5. Mtumbuizaji bora wa mwaka
6. Msanii bora wa kiume
Wakati Alikiba akiwa katika category 7, Taylor swift alionekana katika Category 13 ikiwa ni matokeo ya wimbo wa "Blank space", Tuzo za Billboard Zimefanyika May 17 huku Taylor Swift akinyakua tuzo 7, hii ni rekodi yake ya kwanza kwake kuiweka akiwa na umri wa miaka 25 tu!! Mpaka sasa anasumbua na wimbo wa "Bad blood remix" ambao amemshirikisha Kendrik lamar, mpaka Jana digital copy zaidi ya laki 3 zieshauzwa toka uachiwe rasmi!!
Tukirudi hapa kwetu tuzo za KTMA zinasubiriwa kwa hamu, Alikiba kama alivyo Taylor Swift kule Marekani, Chekecha Cheketua ndiyo kazi inayotrend baadaya ya Mwana. Je Alikiba atatwaa tuzo ngapi? Anaweza vunja kinachoitwa rekodi? Je mpaka sasa wimbo wa Mwana umeuza digital copy ngapi?

0 comments:

Post a Comment