Wednesday, 27 May 2015

COUNTRY BOY ULIKUWA WAPI WENZAKO WAMEANZA KUTOKA.

Na.Moringe Jonasy
Nani hazijui hizi nyimbo, Kabwela, sikati tamaa na mateso za Stamina , Darasa na Country Boy?
Kama huzijui basi fanya haraka uzitafute hata kwa kumwomba jirani yako maana si tu utakuwa hujautendea haki muziki wa kizazi hiki hapa nchini bali hata nafsi yako itakuwa imekosa kitu cha muhimu sana.
Nyimbo zilizobeba ujumbe mkubwa na uhalisia wa maisha yetu kwa kifupi si tuu zilikuwa nyimbo bora wakati zinatoka bali zilikuwa ni nyimbo ambazo zilikuwa kama mto wa ikweta ambao unakuwa na maji kipindi chote cha mwaka.
Baada ya nyimbo hizo nilisikia nyimbo nyingi kutoka kwa wasanii hao kuanzia Alisema ya Stamina ,Sikati tamaa Remix , wambie wenzio na nyingine nyingi kutoka kwa Darasa huku country Boy akisikika sana kwenye nyimbo za kushirikiana.
Mwisho wa wiki hii Stamina atazindua album yake mpya ambayo naambiwa kiyo CD huwezi kuinakili(maendeleo hayo) wakati kwa upande wa Darasa amekuwa na nyimbo nyingi wakimwacha mwenzao Country Boy akiitambulisha wimbo mpya leo ambao nao una maudhui yale yale ya kuzungumzia maisha na kuhimiza vijana kujituma zaidi.
Wakati coutry Boy akiendeleza alipoishia wenzake wanaonekana kuhamia hatua nyingine kabisa wakati Stamina akionekana kufuata zaidi mkondo wa Fid q ambaye hana mfano wake kwa uandishi nchini namwona Darasa akiingia mlengo wa akina One incredible hivyo ule utatu wao unapotea kimya kimya hadi naanza kujiuliza Kuwa alikuwa wapi hadi wenzake wanamtoroka na kusaliti mtindo wa uandishi waliokuwa nao awali.
Unasemaje ‪#‎mwanakalamu‬ mwenzangu ?
Niandikie hapa chini

0 comments:

Post a Comment