Tuesday, 26 May 2015

ULIAMINI ANAKUPENDA AMEKUACHA?

Na.Moringe jonasy
1.ULIMDANGANYA
Huenda ilikuwa ni njia mojawapo uliyoitumia ili azidi kukupenda, lakini ikiwa atakuja kugundua kuwa uliyomwambia yalikuwa ni uongo basi ujue upendo wake kwako unageuka kwa kiwango hicho hicho ukawa chuki. Mwishowe unakimbiwa vinginevyo kama ulimdanganya jitahidi kumweleza uongo wako katika hatua za kwanza kabisa za mahusiano kabla hajaufanya uongo wako sababu ya kukupenda.

2. YEYE SI WA KWANZA
Hapa kwa mwanaume anaweza akaendelea kudanganya ila mwenzangu na mimi wa upande wa pili huna cha kujitetea.Licha ya umri wako mkubwa anaweza akawa na mashaka na upya unaodai unao lakini sehemu nyingine ya akili yake inamwambia huenda kweli yeye ni miongoni mwa wenye bahati kupata mali kubwa mpya na akija kusikia kauli zako kuwa sijui baiskeli sijui ye wapili mara Juma alikulazimisha basi ujue anaweza kukuchukia kama siyo kukufanya wa kutuliza kichaa chake huku akiwa na mwingine ampendaye.

3.MATARAJIO
Wengine tukionekana tuu barabarani miili yetu huficha dhiiki zetu na kuwafanya waamini kuwa huna shida za mara kwa mara lakini anapokuwa nawe basi anaona una shida nyingi kuliko aliyemkimbia.
Lakini pia unadhifu wako wa nje basi anafikiri kuwa upo kila mahali lakini baada ya kusinda nawe ndani masaa mawili anaona kuwa wewe ni mbwa mwitu mchafu mwenye sura na umbo la tausi.
Hapo lazima utakimbiwa.

4. KUMKUMBUKA MKOLONI
Kama aliwahi kutawala ama kutawaliwa basi lazima atalinganisha uhuru na ukoloni kama uhuru hauna maana basi atakumbuka ukoloni kisha kukona si kitu.Hapa pia epuka stori za ; yule alinitenda sana , sitaki kumkumbuka alikuwa hivi na vile baadaye unajikuta unaweka udhaifu wako peupe ?
Anakukimbia maana huna zuri wewe.

 Zipo nyingi sana niambie kitu kuhusu hili #mwanakalamu mwenzangu

0 comments:

Post a Comment