Tuesday, 26 May 2015

AT MKALI WA MUZIKI ASIYEDAIWA CHOCHOTE BONGO-FLEVANI

    AT(mwanamuziki)
Na.Moringe Jonasy
Unakumbuka wimbo wa 'Nipigie' alioimba kwa kumshirikisha Stara Thomas?
Labda hukumbuki labda nikurudishe nyuma zaidi kwa wimbo wake alioshirikiana na mkali mwingine wa sauti tamu Marlow 'wanimaliza' ama ule alioimba na mkali mwenzake wa sauti kwenye wimbo wa Usikomae naye Alikiba , unazikumbuka hizo?
Unaukumbua wimbo wa yamini?
Kama hukumbuki ngoja nikuulize juu ya huu wimbo wake ambao aliimba na wakali wenzake Ray C na Jerry rhymes, ' mama n'tilie' nadhani umenipata huyo si mwingine bali ni mkali anayestesa na video ya wimbo wa SIJAZOEA.
Mkali huyu ambaye ana historia mbaya ya kuteswa na ugonjwa wa ajabu wa kutoa usaha badala ya damu naweza kusema hadaiwi kabisa na Bongofleva.
Kwa nyimbo nilizokutajia hapo juu wimbo gani hakuutendea haki kwa mashairi na kuteka rika zote katika jamii?
Leo hii anaimba mduara ambao hakuna shaka nao anaudai badala ya kudaiwa kutokana na juhudi zake katika kila anachokifanya.
Mashairi yenye lugha yenye kumvutia msikilizaji, video zake zenye viwango na ujuzi wake wa hali ya juu kwenye muziki unamtofautisha na wasanii wengine na kumweka kwenye kundi la wanamuziki bora.
Lakini licha ya kudaiwa wapenzi wa bongofleva bado tuna hamu ya kumsikia tena kwenye wimbo mmoja ama zaidi za bongofleva.

Unaonaje ‪#‎mwanakalamu‬ mwenzangu? Niandikie hapa chini

0 comments:

Post a Comment