Na.Moringe Jonasy
Unaufahamu wimbo wa Nai nai alioshirikishwa Alikiba na Ommy Dimpoz?
Kama huufahamu nenda kauzikilize , wimbo huu ndio uliotufanya tumfahamu na kumheshimu Ommy Dimpoz yule wa Top Band kisha tukampa tunzo na ziara za kutosha ndani na nje nchini.
Unajua kwa nini? Kwa sababu moja tu wimbo ulikuwa mkubwa kweli, wengi walidhani Ommy Dimpoz kabebwa na Ally lakini nyimbo nyingine baada ya Nai nai zikafuta fikra hizo na kuuaminisha umma kuwa Ommy alikuwa mwanamuziki haswaa.
Leo nakupa orodha ya wanamuziki ambao walipoimba na Alikiba tulitarajia mengi kama aliyoyafanya Ommy Dimpoz lakini wameshindwa kufanya hivyo;
1.JONSON NA JACKSON
Unaweza ukawa hujawahi hata kuwasikia ila uliwahi kusikia wimbo wao mzuri wa 'yote yale' ambao uliwafanya wengi tuwafahamu mapacha hawa.Nini kilifuata baada ya yote yale hakuna kikubwa kilichofuata.Hapo najikuta najisemea kuwa ile heshima waliyopata walishindwa kuitumia.
2.NUH WA DAR STAMINA
Wimbo wa niacheni alioshirikishwa Ally ukawaweka wengi makini kutaka kusikiliza nyimbo nyingine kutoka kwa huyu kijana lakini kilichofuata mhh anakijua mwenyewe.
Hapa napo naweza kusema ile heshima haikurudishwa kwa Ally.
3.BAUCHA
Wengi tulimfahamu kama moja ya watayarishaji wakongwe wa muziki nchini.Huyu ndiye aliyetengeneza Fid.com lakini alipotoka masomoni akajaribu muziki na akimshirikisha Ally mwenzake 'Kelele' ikapiga kelele mtaani lakini baada ya hapo sijui kama aliweza kurudi tena studio kama mwimbaji.
4.TOX STAR
Huy naye alijikuta kwenye chart za juu za muziki nchini baada ya kutoa wimbo aliomshirikisha Ally 'sexy girl' .Lakini baada ya sexy Girl sijui nini kilifuata sikuweza kumwona tena Tox Star aliyetegemewa na wengi , nikaamini hakurejesha heshima aliyopewa kimuziki.
5.TOP C
Wengi tuliamini kuwa alimba ule wimbo wa Ulofa peke yake lakini kwa mbali tukawa tukisikia harmonizing za Alikiba ambazo licha ya ubora wa mashairi ya wimbo ule ndiyo zilikuwa zikiufanya wimbo uvutie masikio ya watu wengi.
6.SESEME
Unaukumbuka wimbo wa Ayaya?
Naam kama huukumbuki utafute hata youtube uusikilize , ni wimbo uliowavutia wengi sana na kumpa ziara nyingi za kimuziki Seseme mwisho wa siku akazimika kama mshumaa sijiu tena kama alikuja kuimba tena.
7.DOCHI FLEVA
Huyu alitambulishwa na wimbo uliojaa mashairi kutu wa 'imani' watu wakamwelewa wakampokea lakini baada ya hapo sijui nini kilifuata hakuna kinachotokea kimuziki kwa huyu kijana.
Mwisho wa siku tunaamini kuwa hakuiheshimu heshima aliyopata ama huenda hakuwa na kipaji kabisa.
Lakini wanamuziki hao wanaweza kuwa na nafasi zaidi ya kung'aa kama kweli walikuwa na kipaji cha kuimba.
#mwanakalamu unasemaje?

0 comments:
Post a Comment