Na.Moringe Jonasy
Kwanza nikupongeze baada ya kupata tunzo za
muziki Tanzania kwa mara nyingine baada
ya mwaka jana kuweka rekodi ambayo ni vigumu sana kufikiwa na wasanii wengine
wa muziki nchini.Lakini pia nikupongeze kwa kuchaguliwa kugombea tunzo nyingine
za kimataifa kama za MTV na kwingineko ambako juhudi zako ukimtegmea Muumba
zimekufanya uonwe huko nje na kuwekwa huko.
Ni hatua kubwa sana kuwekwa kwenye vipengele
vitatu na hesabu kama ni ushindi maana kuna maelfu ya wanamuziki Afrika ambao
walitamani hata kutajwa walau mara moja tuu lakini kwako ni mara ya pili.
Kwa kura za watanzania na wapenzi wa muziki
wako nje ya Tanzania naamini una nafasi ya kushinda mbili ama moja kati ya
tunzo unazoshindania japokuwa kuna uwezekano wa kushinda zote lakini kuna
kipengele kimoja ambacho unashindana na
wanamuziki wakubwa zaidi yako Afrika hivyo ushindani utakuwa mkubwa sana ndiyo
maana nina uhakika kuwa mbili zaweza kuja Tanzania kwa mara ya kwanza.
Ushindi wako ni ushindi wa mtanzania yeyote
kwani kwa kushinda kwako utaifanyaTanzania kutazamwa kwa jicho la tatu kwa
upande wa muziki kwani kwa mtu mwenye
akili hawezi kuamini kirahisi kuwa Tanzania ina mwanamuziki mmoja ama
wawili tuu wenye sifa ya kutambuliwa Afrika
hivyo utakuwa umefungua milango ya mafanikio kwa wanamuziki wengine ambao wana
kipaji sawa ama hata zaidi yako na kufika mbali zaidi.Nimekuwa mmoja wa wapiga
kura hasa linapokuja suala la kitaifa kama hili wakati mwingine nimekuwa
nikipiga hata kiushabiki tuu ili mradi mtanzania ushinde.Hata awamu hii
nimekupa kura yangu na kumwacha Wizkid ambaye ukweli unanisuta kuwa bado kidogo
kumfikia lakini nitafanya nini utanzania tuu unanisukuma.
Tuachane na habari za tunzo unazishindania,
naomba tuongelee suala la wanamuziki hasa wa Tanzania kusita ama niseme kuogopa
kutoa Album badala yake wamekuwa wakitoa nyimbo kwa kudonoa donoa wakikwepa
kile wanachokiita wizi wa kazi zao.Ni kweli tumeshuhudia wamnamuziki wengi
wakilia na jambo hilo na wenzetu wa filamu ndo usiseme wamebaki kulia kilio cha
samaki na machozi kusombwa na maji , hakuna anaye wasikia na hata kama kilio
chao kinasikika basi wakisikiao bado wanahisi kilio chao kama wimbo Fulani wa
hisia ambao unawafanya wasinzie badala ya kuamuka na kuchukua hatua.
Wengi wanaogopa na wamejiapiaza kutotoa Album
lakini kwa watu wa filamu watafanya nini zaidi ya kukubaliana na hali maana
licha ya kazi zao kunakiliwa zimekuwa zikikodishwa.Lakini ninachojiuliza hakuna
wanachokipata hata kidogo?
Jibu ni hapana.
Hivyo kuna wanachokipata licha ya kuwa
hakilingani na walichotakiwa kupata ndiyo maana tunawaona ni miongoni mwa
mabingwa wa kuuza sura mitandaoni na kwenye kumbi za starehe japokuwa kuna
madai kuwa wana vyanzo vingine halali na haramu vya kujiingizia pesa.Vyanzo
halali ni kama mauzo ya kazi zao, malipo
matangazo mbalimbali na kazi nyingine rasmi kama biashara na nyinginezo.
Kwa wanamuziki kama wewe una cha ziada kwani
una matamasha ya ndani na nje ya nchi na kuuza kazi mtandaoni na hata nyimbo zenu kutumiwa kwenye kampeni Fulani
kama vile vita dhidi ya madawa ya
Kulevya,UKIMWI ukeketaji na hata kuhimiza kilimo japokuwa kwenye jambo la
mwisho mmekuwa waoga sana kuandika kuhusu masuala hayo.
Sasa nini kinachowafanya muogope kutoa Album
zaidi ya wizi wa kazi zenu kwenye zama za sayansi na teknolojia kama hizi?.Kama
kuiba hata hizo nyimbo mnazodonoa donoa zinaibiwa licha ya kuuza kwa njia za
kisasa maana pia kuna njia za kisasa za kuiba.Mfano ukitoa wimbo mpya
nitaununua kisha nitawarushia wenzangu zaidi ya kumi kupitia parua pepe ,Bluetooth
ama hata whatsap na hata ukiweka video youtube mwingine anaweza ipakua na
kuanza kuiangalia na kuwatumia wengine kupitia whatsap hivyo kupunguza idadi ya
watazamaji ambao wangekuwa kama kichocheo cha kulipwa na youtube ama hata
google.Nasema haya kwa kutaka kukuambia hata kwenye kudonoa donoa kuna wizi
hivyo naamini kama utatoa album utauza na kupata faida kubwa huku wizi nao
ukiwa mkubwa.
Najaribu kufikiri Album yenye nyimbo kali kama
my number one, number one remix, nana ,mdogo mdogo ,nasema nawe ,nimpende nani
na nyingine nyingi ambazo hazijatoka kamaulizowashirikisha wanamuziki wengine wa Afrika na nje ya Afrika
itakuwaje Afrika na duniani ikiuzwa kupitia mitandao na kwenye CDs.Hautakuwa
bilionea tuu kama siyo tirionea ama nusu tirionea.
Si pesa tuu itakuweka kwenye daraja Fulani la
wanamuziki kwani licha ya kuwa na tunzo kubwa za muziki pia iadadi na mauzo ya
album ni moja ya kipimo cha ukubwa wa mwanamuziki.Na hata kwenye kusaini na
makampuni makubwa ya muziki kinachoangaliwa ni pamoja na idadi na ubora wa
album ndiyo maana licha ya uwepo wa wanamuziki wengi wazuri kipindi Airtel one
8 project Alikiba alikuwa chaguo la kwanza kutokana na kuwa ni mwanamuziki
aliyevunja rekodi za mauzo ya album Afrika mashariki.
Unaweza kuuliza kwanini Diamond , lakini
ukweli ni kwamba wewe ndiye mwanamuziki unayeangaliwa zaidi ndani na nje ya
Afrika hivyo wanamuziki wengi
wanakuangalia wewe kama mfano wao hivyo kama nawe utawatisha kama ulivyotishwa
na watangulizi wako basi tutaishia
kudonoa donoa tuu vinyimbo vizuri huku mkitunyima haki yetu ya kusikiliza
albuma ambazo amini usiamini zitakuongezea mashabiki kama siyo wafuasi ambao
wanapeda kusikia nyimbo za mwanamuziki Fulani zilizokusanywa wakisikia ubunifu
wako badala ya kusikia tuu nyimbo chache chache zitokazo kwa vipindi.
Lakini pia wewe ni mmoja wa wanamuziki wenye
mafanikio makubwa ndani na nje ya Afrika
hivyo suala la kuingia mikataba isiyo ya kibabaishaji na makampuni yatakayoweza
kukuibia ni gumu sana lakini pia una uzoefu na biashara ya muziki hivyo kuziba
mianya ya wizi ni jambo jepesi kuliko kwa mwanamuziki mchanga kama Mo music kwa
mfano.
Sababu nyingi ya kwa nini Diamond ni kwamba
wewe ni miongoni mwa wanamuziki wachache wenye matamasha na ziara nyingi iwe
nchini ama nje ya nchi hivyo ukiwa na album unakuwa na hazina kubwa ya nyimbo
za kuimba jukwaani badala ya ufanyavyo sasa kuimba nyimbo za ablum ya kwanza
nyimbo chache ulizozitoa karibuni.
Pia ablum hukutengenezea wafuasi wengi kuliko
mashabiki.Unaweza jiuliza ni kitu gani hiki ila kwa kifupi mashabiki ni wale
wanaokupigia kelele kukushangilia kwa si kwa sababu ya kupenda kazi zako bali
kwa sababu nyingine ama mwonekano wako ama chuki dhidi ya mtu mwingine yaani
akutumie wewe kupooa hasira zake juu ya huyo mtu anaweza akawa mwanamuziki,
mtayarishaji na hata muigizaji lakini mfuasi yupo na wewe kwenye raha na shida
zako.Mfano Alikiba ni mwanamuziki mwenye wafuasi wengi tangu kale kutokana na
album zake alizozitoa awali, Juma nature naye hivyo hivyo kama ilivyo kwa Lady
Jay Dee ,mwana FA ,Marlow ,Pro.Jay na wengine wengi hii yote kutokana na album ambazo si tuu
zinawapa nafasi ya kuburudika na kazi zako bali kuzieleewa zadi kwani kwa
utafiti wangu usio rasmi ni kwamba ukisikiliza album Fulani hutoisikiliza mara
moja bali utaisikiliza zaidi na zaidi na kuelewa hata kile ambacho kilicjificha
kwenye talata yako tofauti na kusikiliza nyimbo kwa misimu kutokana na upya
wake.Ulifanikiwa kulifanya hili ulipotoa Album ya kwanza lakini ghafla
ukasikiliza ya wakongwe badala yake unashabikiwa kwa msimu kutokana na upya wa
kazi jambo ambalo si zuri sana kwa mwanamuziki mkubwa kama wewe ni wakati wa
kutengeneza wafuasi sasa ufaidi matunda ya kazi zako.
Na sababu ya mwisho ambayo si ya kiuchumi sana
bali ya kisanaa zaidi ni kwamba Album ni
kama kipimo cha kipaji chako.Nikupe mfano mmoja wapi alipo Sam wa Ukweli? Unaweza
usijue kilichompoteza ama unaweza nipa
sababu nyingine za kawaida kufikiria.Ila ukweli ni kwamba Sam mmoja wa
wanamuziki ambao niliwatabiria makubwa kama nilivyofanya kwako amemezwa na
mafanikio ya album yake ambayo kiukweli ilikuwa ni bora.Yupo kama amemaliza
kipaji chake kwenye ile Album yaani alifikia mwisho wa kufikiri na kwa kutoa
ile album hivyo hata akija kuimba anaweza kurudia idea za kwenye ile album kama
alivyofanya kwenye kurudia namna ya uimbaji kwenye ile album yake.Hivyo ukitoa
album zaidi na zaidi kipaji chako kinapimwa haswa na kukubalika zaidi.Au
unafanya ulisema kwenye spora show, kuwa
haiwezekani mwaka mzima ushindwe kutunga wimbo mmoja mzuri? Kwa hiyo
itakuchukua mika zaidi ya kumi kuandaa album nzuri?.
Naomba niishie hapa nikikusisitiza kuwa huu ni
wakati wa Diamond kutoa album ya pili.
Naomba kuwasilisha #mwanakalamu.
0 comments:
Post a Comment