Na.Moringe Jonasy Mhagama
Uhakiki ni kitendo cha kutathmini ,kueleza
,kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi
Fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum.Kazi hiyo ya fasihi inaweza
kuwa; shairi,hadithi tamthilia na vipera vyake.
Kumekuwa na mjadala mkubwa sana juu ya dhana
ya uhakimki wa kazi hizo za fasihi na kutengeneza makundi makuu mawili kundi la
kwanza likidai kuwa mwandishi ama mtunzi
ndiye ajuaye dhima na muundo wa utunzi wake kwani hujua kilimchochea kutunga
hiyo kazi na kundi la pili likidai kuwa kuna haja ya watu wengine kueleza,
kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi hiyo kwa kuzingatia mambo mbalimbali kama
itikadi,historia ,tamaduni na hata imani ya mtunzi wa kazi hiyo.
Kundi la kwanza linaamini kuwa kuna uwezekano
wa kuchambua umbo la nje na ndani mwa
kazi hiyo ya kifasihi lakini kuna vitu ambavyo mtunzi anahitajika kutoa
alichokimaanisha na kundi lingine limeweka misingi mbalimbali ambayo itawaongoza
wachambuzi wa kazi hiyo.
Turudi kwenye mada yetu ya leo kuhusu video ya
chekecka cheketua ya mwanamuziki Alikiba ambayo haijamaliza wiki moja tangu
itambulishwe kwote duniani.Kama ilivyokuwa mwana wengi waliikosoa na kudai si
nzuri na bilinganya kibao ili mradi tuu kutoa kasoro.Bahati mbaya wengi walioikosoa
walishindwa kutoa sababu anata waliotoa sababu walikuwa na sababu nyepesi sana
hali iliyomfanya hata Alikiba mwenyewe awaone ni ‘’wenye chuki binafsi tuu’’.Kabla
sijaamini kuwa alikuwa ni watu wenye chuki pekee ndio waliikosoa ile video ngoja
niandike mambo yafuatayo juu ya nilichokiona kwenye wimbo ule.
1.WIMBO KUTOELEWEKA KWA WENGI MWANZO
Haujaimbwa kwa lugha ambayo haitumiki
Tanzania, mashairi yamebeba maneno ya Kiswahili na machache sana yalikuwa ya iingereza kama
siyo neno moja .Wengi waliposikia jina la wimbo hawakujua ni wimbo wa aina gani
na hata ulipotoa wengi walionekana kutouelewa hadi pale walipomwona akitumbuiza
jukwaani hapo ndipo walipoanza kujenga maana yao ya wimbo huo, walikiona
kiitikio kilichokuwa na maneno matatu yaliyojirudia rudia ndiyo dhana kuu ya
wimbo na kuhisi hata video yake itatawaliwana wasichana wenye kile AY anakiita
‘’zigo’’ wakishindana ‘’kucheketua’’ kitu amabacho si sahihi kwani wimbo
ulibeba dhana pana zaidi ya kucheketua.
Wengi walitegemea video ingewapa maana halisi
lakini walipokutana nayo walijikuta wakisema mbaya mara mpangilio wake mbaya
mara uchezaji mbovu na mambo mengi yenye uhai mfupi kuliko njiti ya mwisho ya
kiberiti.
2.UPEKEE WA ALIKIBA KATIKA UTUNZI
Alikiba ni miongoni mwa watunzi wa kipekee
ambao wanauandishi wakipekee sana hapa nchini, akiandika hadithi kwenye wimbo
basi maneno na misemo atakayoitumia basi itamfanya msikilizaji atake kusikia
tena na tena alichokiimba rejea Mac Muga ,Dushelele,Hadithi na hata mali yangu
ni simulizi zenye ufundi wa hali ya juu.Namana yake ya utunzi ndiyo
iliyowafanya wengi kutoa tafsiri ya ziada kweye wimbo wake wa ‘’Mwana’’ Kwani
walishazoea kuwa huyu mtu huandika kwa kutoa maana zaidi ya maana ya mwanzo.
Upekee huu wa kiuandishi ndiko kulikopelekea
wengi waachwe njia panda kwenye video ya chekecha cheketua ambayo imezingatia
tyuni , marimba na maana ya mashairi yake hili linaonekana kwenye madhari ya
video na hata mwonekano wa wahusika wa
kwenye video.
3.VIDEO KUWA NA ZAIDI YA KISA KIMOJA
Tofauti na kwenye video za nyimbo
zilizotangulia kama vile Hadithi,Karim, Mac Muga na hata mwana ambayo mwimbaji
huyu aliamua kutamba mashairi yake na kucheza sehemu ndogo ya wimbo wake akiheshimu
kile mwandaaji wake na mpiga gitaa kwenye chekecha cheketua Ally aliamua kuweka
viza zaidi ya kimoja kitu ambacho wengi hajaking’amua.Kuna kisa cha yeye (Kiba)
Yule mrembo ambaye yupo na mama yake na hata Yule kijana mwingine.Wengi
wamechanaganya visa na kuiona video haieleweki na wengine wakaenda mabli na
kudai haina maana.
4.KUHESHIMU NA KUSIKILIZA ALA ZA MUZIKI
Hapa marimba,gitaa , ngoma , zumari na
vinginevyo vinahusika.Alikiba ameendelea kuwa mtumwa wa gitaa si tuu awapo
jukwaani bali hata kwenye video zake ( rejea mwana ).Hiki pia amaekifanya
kwenye video ya chekecha cheketua Ally amesikiliza marimba kuandaa ‘’script’’ ambayo imekuwa ya kiasili
zaidi kuanzia usela ,uchezaji na hata madhari ya video angekuwa wa ajabu kama
asingezingatia hilo na kujaza meli ndege na maghorofa kwenye wimbo wa aina hii
japokuwa kwa wengi wanaoangalia muziki kwa juu juu wangemsifia na kumwona
amepiga hatua kumbe angerudi nyuma hatua nyingi sana maana hicho kitu tumekiona
kwenye nyimbo nyingi sana.
5.KULINGANISHA VIDEO HII NA ZA WENGINE
Hii ni kasumba kubwa ambayo wengi tunakosea na
kujipa uhuru wa kuona hiki kitu si sahihi ama kibaya.Kuna mahali kweli
panahitaji kulinganisha ambapo ni kwenye ubora wa video ambako kwa mwanamuziki
kazi yake ni kutoa pesa kwa mwongozaji
ambaye naye kufanya kazi.Lakini tumekuwa tofauti ubora twaukubali lakini visa hatujavielewa
basi tunaropoka tuu eti ‘’mbaya’’Japokuwa binadamu hana asilimia mia ya
utendaji ‘’efficient’’ lakini wengi wanataka visa viwe kama vya wanamuziki
Fulani ama wa Marekani ama hata ulaya ambao kwao wanaona kama wakuwaiga.Kweli kuiga tuige
vingine lakini si kwenye sanaa ambako mtunzi ndiye mmiliki wa kitu hicho.Mfano
kama Eric shigongo anaandika hadithi za namna Fulani akakubalia si lazima wote
tupite njia hizo ndipo tutafika alipofika Eric hicho ni kipaji ambacho ni kama
uumbaji mwingine mfano ng’ombe wanaweza kufanana rangi na hata urefu wa pembe
lakini unaweza kutofautisha mmoja na mwingine ndivyo vipaji vyetu.
KWA MASHABIKI NA WAPENZI WA MUZIKI
Mwisho niseme kuwa video ni nzuri kwa yule amabaye ataamua kuhakiki kwa kufuata nadaria yoyote ya uhakiki bila kutanguliza ushabiki. Si mbaya
kama wengi wanavyotaka kutuaminisha bali mambo niliyoeleza hapo juu yamechangia kuleta maneno hayo bahati mbaya wengine
wameangalia video mara moja halafu wanatoa hukumu bila kujua mwanamuziki huyu
amevumbua nini na kukiweka kwetu.Wengine wamefika mbali hata kuanza kumtusi na
kumwona mtu wa ‘’level’’ zao ,wengine wameenda kwenye ukurasa wa TRACE Nigeria
na kuanaza kutoa maneno ya shombo mara ehhee sijui video imesambaa sana whatsap
na aliyeisambaza ni yeye(Ally) hivyo haina ule upya kama walivyodai Trace.Huenda
kweli video ilisambaa ila wengi hawajua kuwa hawa wanamuziki huwapa watu wao wa
karibu , wanamuziki wenzao na hata waongozaji wa hapa ndai kutoa maoni yao
kabla ya kuitambulisha kwa hadhira hivyo watu hao wanaweza kuisambaza kwa watu
wengine wanaowaaamini kisha kusambaa sasa hayo maneno yana malengo gani kama
siyo chuki?.
Lakini video hii pia imewafanya wengine
waendeleeze kile wanachokiita ‘team’ amabazo kwa bahati mbaya hazina msaada
nchini bali kuiaibisha nchi kwa kutunana sisi kwa sisi na kuwatukana wazazi
wetu wengine wka bahati mbaya ni marehemu.Timu hizi hazina ile maana ya timu
halisi kwani hakuna timu popote duniani yenye kazi ya kumshusha Fulani na kumpaisha mwingine hata kama hastahili
kupaa.Timu hizi zinafanya kazi kinyume kabisa na maana halisi nijuavyo timu
huundwa ama hutokea kwa malengo chanya lakini kwetu ni shaghala baghala.
USHAURI WANGU KWA ALIKIBA.
Ni kutopishanisha wimbo na video yake kwa muda
mrefu sana kama ilivyofanyika kwa wimbo huu japokuwa kulikuwa na sababu maalum
zilizochelewesha zaidi video.Kama asingetoa wimbo hata matatizo yaliyokwamisha
yasingemuathiri hivyo naamini atakuwa amejifunza na kama atatoa wimbo pekee
basi iwe kama bonas tuu baada ya kutoa video na wimbo mpya na si kufanya
alichokifanya.Naamini wasimamizi wake wamelijua hili na sitegemei kama
litajirudia tena.
Pia kwa video hii ajaribu kuongea kwenye chombo chochote maana ya kazi hii ya chekecha cheketua ili awatoe gizani ambao hawajaielewa kwani wahakiki huru wamegoma kufikiri zaidi na kutuaibisha watanzania.
0 comments:
Post a Comment