BARAKA
Na.Moringe Jonasy Mhagama
Naam wengi tunamfahamu Baraka Da Prince mkali wa nyimbo za visa za mapenzi ambaye mwaka huu ameibuka na Tunzo ya mwanamziki bora Chipukizi kwenye Tuzo za Muziki za kilimanjaro.Wengi wanajiuliza kwa nini mwaka huu na si miaka kadhaa iliyopita kwani kabla ya Siachani na wewe ambayo imewafanya wengi wamwangalie kwa jicho la tatu mkili huyu ambaye kabla ya hapa alikuwa ameimba nyimbo kadhaa za kiwango cha juu kama Jichunge,Sio fine na Ndio maana.
Kwa nini hakuangaliwa sana kama anavyoangaliwa sahizi ?
Ni kitu kimoja tuu usimamamizi kama ilivyo kwa mkali mwenzake Belle nine ambaye licha ya ubora wa kazi zake amejikuta kisifiwa tuu kuwa ni mkali lakini hana mafanikio kama yale ambayo wanaolingana naye.
Hilo linajieleza kwani unaweza kuamini kuwa Ney wa Mitego amemzidi ubora Belle nine?
Hapana ni usimamizi tuu kama ilivyo kwa Baraka ambaye yupo chini ya Tetemesha iliyomfanya awe mwanamuziki anayepata kutokana na ubora wa kazi zake.
SAMIR
Ukiniambia nitaje watunzi kumi bora wa nyimbo za mapenzi siwezi kumsahau huyu mkaliwa nyimbo mbalimbali kama vile Ningejua Ukipenda,Mnyonge , kinyulinyuli na wimbo unaotamba kwa sasa 'Nakuombea'.Tangu nikiwa kidato cha tano nilikuwa nikimsikia mwanamuziki huyu lakini usishangae akipata usimamizi unaoeleweka zaidi akichukua tunzo ya mwanamziki Chipukizi kama ilivyotokea kwa Baraka ambaye huu mwaka haukuwa mwaka wake bali miaka mingi iliyopita.
Nakuombea kama ilivyokuwa mnyonge zinabaki kuwa nyimbo zinazodhihirisha ukali wake wa utunzi.
CHRISS WAMARYA
Kwa wale ambao si wakazi wa Morogoro na wanaofuatilia muziki kwenye redio za Dar es Saalam wanaweza wasimfahamu mkali huyu ambaye Stamina aliamua kumweka kwenye wimbo wa Mngekuwepo na kuonesha umahiri wake wa kupendezesha 'Chorus'.
Chriss Wamarya nilianza kumsikia alipoimba wimbo wake wa Sinyorita mwaka 2009 na kuniaminisha kuwa alikuwa na kazi ndogo ya kuifanya Tanzania nzima imfahamu na kumpokea kinyume chake hata baada ya kutoa nyimbo zake kali kama Kilomita sita,Tutoke,nakuwaza na wimbo wake ulionifanya nizidi kumhurumia mwanamuziki huyu kutopokelewa na watanzania na kupewa heshima yake kwenye 'bongo Fleva' wa 'Usinihukumu' bado hakupokelewa kwa heshima aliyostahili.
Kwangu sitashangaa pia siku akija kutwaa tuzo ya mwanamuziki Chipukizi baada ya kuwa chini ya usimamizi mzuri zaidi kama ilivyotokea kwa Baraka Da Prince.
Niandikie mtazamo wako #mwanakalamu wenzangu
0 comments:
Post a Comment