ads

Monday, 13 July 2015

ALIKIBA NA KILE TUNACHOKIITA ''UZALENDO''

Na.Moringe Jonasy
Habari wanakalamu mwenzangu, poleni na majukumu ya kila siku ,wengi wamekuwa wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea Dodoma najua sahizi mambo yanaendelea kama kawaida.Ni kitu kizuri sana kujua hata kinachoendelea kwenye siasa za nchi yetu na jambo la msingi sana ni  kwenda kujiandikisha ili kupata kitambulisho kitakachotusaidia kupiga kura kwani ni hai na wajibu wetu kama watanzania wenye sifa za kupiga kura.

Wakati mchakato ukiendelea Dodoma mjadala ulikuwa mkubwa sana na nilibahatika kukaa na wenzangu tukijadili hili na lile juu ya sifa ya kiongozi tunayemwitaji watanzania kwa sasa mojaya sifa ambayo ilikuwa kama imebeba mambo mengi kama siyo yote ni ''UZALENDO'' .
Je, tunajua maana ya uzalendo?
Nani anatakiwa kuwa mzalendo?
Kivipi unaweza kuwa mzalendo?
Unaweza kunufaika na uzalendo?
Je, kama hakuna uzalendo kuna nini kinachoweza kutokea?

Hayo ni baadhi ya maswali niliyokuwa nikijiuliza baada ya kutoka kwenye mjadala huo ambao uliisha kwa kila mtu kutoa lake analolijua.
Uzalendo umefasiliwa kwa ujumla kumaanisha ‘mtu kuwa na utiifu, upendo na kujitolea kwa taifa au nchi yake’. Hii inamaanisha kuwa, kila mwananchi wa nchi fulani anapaswa kuweka maslahi ya taifa lake mbele kwa kila akifanyacho kwa kuzingatia kuwa kila alitendalo linamwathiri kwa namna moja au nyingine mwananchi mwenzake, ambae ndie dada, kaka, mama na baba yake.
Uzalendo umejikita zaidi katika matendo na si maneno matupu tu. Matendo hapa yanahusu wakati wowote ule, iwe wakati taifa likiwa katika dhiki au furaha. Dhana ya uzalendo inajipambanua zaidi kuwa kwa mzalendo, kuitumikia nchi yake kwa uaminifu na kwa manufaa ni fahari kubwa kupita zote.
Wanapozungumzia uzalendo, Wamarekani hukumbuka zaidi msemo wa Patrick Henry alioutoa wakati wakipigania Uhuru wao dhidi ya wakoloni Waingereza kuwa ‘give me liberty or give me death’. Kwa tafsiri siyo rasmi, Henry alimaanisha kuwa katika kupigania nchi yake, mtu awaye yote hupaswa kuchagua moja tu kati ya mambo mawili ‘kupata ukombozi au kifo’. Tunayosimuliwa jinsi Chifu Mkwawa wa Wahehe alivyopinga ukoloni wa Wajerumani hata kumgharimu maisha yake yanaakisi kauli ya Henry.
Msamiati ama neno Uzalendo limekuwa likitumika kwenye nyanja mbalimbali Muziki ukiwemo hasa pale myuziki ama mwanamuziki anapovuka mpaka wa nchi.Haikuwa ajabu BASATA walipomwonya Shilole kwa madai ya picha yake kusambazwa mitandaoni akiwa kwenye mwonekano usio wa kimaadili.Na taasisi hiyo ilienda mbali na kudai kuwa kila mtanzania hususani wanamuziki wanapopata ziara ama matamasha nje ya nchi hupewa kibali na huwa wamebeba utambulisho wa Tanzania kama taifa hivyo kwa kufanya kitendo kilichokuwa kinyume na maadili yetu kilitafsiriwa kama udhalilishaji kwa taifa.
Uzalendo ulikosekana kwa mtu kuangalia hisia zake zaidi badala ya utaifa aliokuwa amevikwa ndiyo maana akapewa onyo lile.
Si hivyo tuu imetyokea pia wanamuziki ambapo wamekuwa wakiliwakilisha taifa si tuu kwa kushiriki kwenye tunzo za kimataifa bali hata kutumbuiza kwenye matamasha ya kimataifa na yasiyo yakimataifa nje ya nchi.Kufanya kwao vyema kunalipaisha taifa na letu.
Wanamuziki mbali mbali , wasanii mbalimbali na waigizaji hapa nchini wameliwakilisha taifa kupitia kazi zao miongoni mwao kwa kuwataja wachache ni AY,Juma Nature,Marehem,u Steven Kanumba, Wema sepetu, Jakate mwengelo,Vanesa Mdee, Lady Jay Dee, Diamond ,Fid Q, Saida Karoli, Aslay, shaa, Joh makini , Alikiba , Martin Kadinda, Sheria Ngowi, Peter Msechu na wengine wengi kufanya kwao vizuri kuliwafanya waliwakilishe taifa letu  vema na wameonesha uzalendo wao  kwa kujituma na kutofanya vitu vilivyopoteza ma kupunguza heshima na hadhi ya taifa letu.
Sasa wakati nafikiria nafasi ya kila mtu kuwa wazalendo kwa taifa lao wakiwemo wasanii na watru wengine maarufu nikakumbuka hili linaloendelea kwenye tasnia ya muziki nchini ambapo baadhi ya wanamuziki wakitajwa kama si wazalendo.
Alikiba ni mmoja wa wanamuziki amabo wamedaiwa kuwa si wazalendo kwa kuwapa nguvu wanamuziki wanaoshindania tunzo za uziki nje ya nchi kufikia hatua ya waandishi wa habari kumuuliza alipokuwa kwenye moja ya kituo cha redio nchini.Nilipenda majibu ya Akiliba kwani yalifichuo uozo na ujinga wetu juu ya dhana ya uzalendo.
Alijibu kuwa alikuwa ametoa matangazo  mbali mbali kupitia kwenye account yake ya Instagram kwa wanamuziki waliokuwa wamemwomba kufanya hivyo.Laki Ally alinda mbali kwa kugeuzia kipao upande mwingine kwa kuhoji kwa nini amekuwa akiulizwa yeye kuwafanyia wenzake kuonesha uzalendo wakati kuna aliokuwa ameomba wenzake kutangaza kazi zake za kapeni ya kutokomeza Ujangili ambayo yeye pamoja na watu wengine wamejitolea kufanya kazi hiyo ambayo si jambo dogo na linagusa utaifa zaidi si kwa faida yake pekee, na walioitikia wito huo walikuwa ni watu wachache tofauti na aliokuwa amewaomba.
Ilishangaza kwa jambo ambalo linagusa taifa kwa kiwango kikubwa likipuuzwa na kubezwa kwa kulazimishwa kumtangaza mtu amabaye hakuona hata umuhimu wa kumwomba amuwekee tangazo lake la kuomba kura kwenye tunzo za kimataifa kutumia neno Uzaledo hapo ndipo maswali yangu ya pale juu kuhusu uzalendo yanahitaji majibu.
Nani anapaswa kuwa mzalendo, Kwa nini  na  kwa wakati gani? Na maswali mengi amabayo najua wengi tunayajua bmajibu yetu lakini kwa kujifanya vipofu na viziwi tunaimba wimbo wa uzalendo kwa manufaa ya hisia zetu.
Sikatai kumekuwa na sintofahamu kwa wanamuziki hawa ambayo daima nimekuwa nikisisitiza kuwa inakuzwa na wanahabari na washabiki kwa kujua ama kutokujua lakini kwenye masuala yanayogusa maslahi na sifa ya taifa hili lilikuwa ni jambo la kuweka pembeni sifa binafsi.
Nilishangaa pale watu waliohoji Ally alipomwombea kura Mwanamuziki kutoka Nigeria na kumwacha mwanamuziki kutoka Kenya au Uganda bila kujua kuwa kipengele hicho kilikuwa cha video bora na ile video ulikuwa imeongozwa na mwongozaji aliyeongoza video yake mpya iliyotoka karibuni Chekecha cheketua.
Ingekuwa kwenyekipengele hicho kulikuwa na mwogozaji ama mwanamuziki wa Tanzania hapo ningemshangaa sana Ally kama nilivyoshangaa hao wanaoudai Uzalendo kwa Ally wakimwacha Diamond ambaye licha ya ukubwa wake Afrika hakuutumia uzalendo kutangaza ujio wa video mpya ya Alikiba na kumtangaza zaidi Alikiba kutokana na kuwa na washabiki wengi ndani na nje ya Afrika pengine kuliko mwanamuziki mwingine nchini.
Uzalendo unaongelewa wa kumtukana mwanamuki wa ndani kwenye ukurasa wa kituo kikubwa cha televisheni Afrika na duniani  ni uzalendo wa aina gani?
Inashangaza sana tunapotumia neno uzalendo kuwatuhumu wenzetu na kujisifia bila kujali  mantiki yenyewe ya neno uzalendo.
Kwa mantiki hiyo UZALENDO unakosa maana kutokana na matendo yetu na ubinafsi wetu kama wafanyavyo wanasiasa na watu wengine wengi wakifanya mambo  yanayopoteza maana ya neno uzalendo.
Niambie #mwanakalamu mwenzangu

0 comments:

Post a Comment