KALAMU YANGU
S.L.P 2
JIPULIMEPASUKA
Mpedwa dada salam.
Hali yetu hapa nyumbani ni nzuri isipokuwa mama bado hana raha kwa sababu ya majibu ya barua niliyokutumia.
Matilaba ya barua yangu ni kutaka kukueleza kisa ambacho nahisi ukikikumbuka utajua kwa nini siachi kukusisitiza juu ya jambo nililokuambia juzi kwenye barua.
Kabla sijakusimulia hiki kisa ngoja nikupongeze kwa kuwa ' sharp' kujibu barua yangu kwani nilidhani isingekufikia,ama ungeipuuza kutokana na kuwa bize na kazi zako na pengine sijui MISTAGRAM nasikia unapiga tuu mapicha mara upo Iran ,Kenya hata Jamaica lakini umejibu haraka dada ,asante sana kwa kutujali.Asante pia kwa zawadi ya viatu uliyotutumia ila Merina havijamtosha nitavaa mimi dada.
Baada ya shukrani zangu naomba nikukumbushe kile kisa alichotusimulia mwalimu wa stadi za kazi siku ile alipopewa nafasi ya kumtunuku mshindi wa mtihani wa Ujirani mwema.
Alianza hivi;-
Hapo kale palitokea mwana mmoja ambaye alikuwa akijisifu kwa kuwa tajiri, daima alikuwa akijisifia kwa kuvaa vito vya thamani ikiwemo saa yake iliyokuwa imeundwa kwa dhahabu tupu.Si wakati wa masomo,ibada hata michezo lazima aonese saa yake ilivyomelemeta kito hicho cha thamani ilifika wakati hata wenzake walitamani wamuibie ile saa sema wangeificha wapi ile saa wakati alikuwa nayo peke yake?.
Basi baada ya siku za majigambo na manyanyaso ya huyo mwana juu ya dhahabu yake akaja mwana wa mjane mmoja ambaye licha ya kutokuwa tajiri alijaliwa kuwa na hekima ambazo zikamfanya apendwe na watu wengi sana , watembezi na wafalme wengi walitokea kumpenda yule mwana wake wa kiume ambaye waliamua kumtuza vito vingi ukiwemo mkufu na saa ya dhahabu.Yule mwana ni kama alirithi hekima za mama yake hakuwa mtu wa kujivuna na hata saa yake hakuwa akiivaa kila mara zaidi ya mkufu wake ambao daima ulikuwa shingoni lakini haukuonekana kuwani daima ulifichwa na shati lake.
Mwana huo naye alitokea kupendwa sana na watoto wenzake hata watu wazima wakiwemo walimu lakini kwa upande wa yule mwana majivuni alianza kumchukia yule mwana mpole na kuanza kumuonea.
Siku moja mwana majivuni alianza kujisifu darasani kuwa pesa ndo iila kitu hekima ni kwa ajili ya masikini na akawanunulia maandazi wanafunzi wakorofi na wakaanza kumpiga yule mwana mpole ambaye alijitahidi kujinasua kutoka kwao lakini walifanikiwa kung'oa vifungo vya shati lake na kuufanya mkufu wake wa dhahabu kuonekana.
''Ha mwana mfalme!" wanafunzi wote wakaguna baada ya kuiona dhahabu kwenye shingo ya yule mwana mpole na hapo hapo heshima ikaanza kwake.
Baadaye darasa liligawika kwenye makundi mawili ambapo wapo waliokuwa wakidai kuwa mwenye saa ndiye tajiri lakini wengine wakadai mkufu ni wa wasichana baadaye yule kijana mpole akaonekana kuwa na vyote saa na mkufu.
Hapo ndipo ubishi ukakua hadi kwa walimu , kwani yule mwana majivuno alimtuhumu mwenzake kumiliki dhahabu isiyo halisi jambo alilolipinga kwa nguvu zote.
Hatimaye walimu walikubaliana kumtafuta mwosha vito ili aoshe vito vyao na kujua ipi haikuwa dhahabu halisi, wakakubaliana japokuwa yule mwana mpole hakukubaliana na jambo hilo kwani aliona kama ni kuweka utajiri wao mbele ya hoe hae ni kama dharau kwao.
Siku moja kabla ya tukio la kuosha vito vyao mwana majivuno alifunga safari hadi kwa mwosha vito na kumkatia fungu la fedha ili akatoe majibu kinyume na ukweli jambo ambalo mwosha vito kwa kupenda pesa alikubaliana nalo na kuongeza shangwe kwa mwana majivuno.
Wakati wa kuosha vito ukafika na mwosha vito akatangaza kuwa vito vya mwana mpole vilikuwa halisi na yule mwana majivuno havikuwa halisi.
Mwalimu alirudia kutangaza majibu ya mwosha vito na kumalizia kwa kauli moja KIZURI KIKIKOSEKANA BASI KIBAYA NACHO KITAONEKANA KIZURI.
Unaikumbuka hii kauli ya mwalimu dada'ngu? Basi na mimi nakuambia KIZURI KIKIKOSEKANA BASI HATA KIBAYA KITAONEKANA KIZURI.
Wasalamu.
Mdogo wako Heri.

0 comments:
Post a Comment