ads

Tuesday 2 June 2015

HUFANANI NA MELISSA? MHH HUYU MUNGU SASA MNAMPA KAZI

Na.Moringe Jonasy
We ni msichahana mrembo sawa ama ulikuwa mrembo sana zamani lakini muda huu kazi yako ni kumlalamikia Mungu na kutamka hicho unachokiita laana kwa huyo unayedhani mbaya wako.
Kila siku wewe unadai "Umesamehe na unamwachia Mungu'' lakini kila dakika unalaani kitendo ulichofanyiwa.
Unachekesha sana ama ndo ule msemo wa ''Nakusamehe ila sitokusahau?''
Labda nikupe mfano mmoja ambao kama hautokuwa ni picha halisi ya maisha yako basi utakuwa unashabihiana kabisa na maisha yako ya nyuma.
Natumia jina la Melissa kama mfano.
Melissa alizaliwa miaka ishirini na mbili iliyopita , Mungu alimjalia uzuri haswa si urembo maana urembo upo hata dukani ila uzuri kila mmoja anao na ni zawadi yetu kutoka kwa Mungu.
alipofikia umri ambao naweza kusema ni katikati ya mawio na machweo hakuna ambaye hakuuna uzuri wa Melissa.Wanaume wakatamani kuwa karibu yake wapate kuwa rafiki zake baadaye waitwe wapenzi wake na hatimaye wauone na kuutumia uzuri wake.
Mwanzoni Melissa aliwakwepa akifuata mafundisho ya wazazi wake,mafundisho ya msikitini na Kanisani.Lakini baadaye aliamua kutojinyima kwa kumchagua aliyemwita ''mtu wake'' na kumruihusu kuuona vizuri uzuri wake , we waligandana ,wakashibana kila mtu kajua hata yule ambaye hakutakiwa kujua walimfanya ajue.Shuleni walimu walianza kumpa karipio lakini wapi kwa walimu wa kike aliona kama wanamwonea wivu wale wakiume akaona wanamtamani na kumpa kiburi Juma wake ambaye alimwona kila kitu kwake.
''Hakuna marefu yasiyo na ncha'' na ''penye wengi pana mengi'' ndivyo ilivyokuwa Melissa alianza kutamani zaidi ya kile alichokipata kwa Juma baada ya kuambiwa alichokuwa akikipata hakikufika hata robo wa vingine vya kwingine.
Akakata shauri, lazima avifuate vingi moyo ukimkumbusha methali na misemo ya wenzake ''Chelewa chelewa utamkuta mwana si wako'' akamfuata Hussein ,Aman ,Moringe, Nyemo, na Charles huku akiwa amajipangia ratiba kali ambayo ilikuwa ni vigumu kwa Juma kujua kama alikuwa akiibiwa.
Juma kuja kushtuka mambo yameharibika na aliishia kumwambia kuwa ''Mtaka vingi kwa kupa hukosa vyote'' na ''pema usipopema ujapo pema si pema'' lakini Melissa alikuja na kashfa ''Wapi? maneno ya mkosaji hayo''.
basi siku zikapita akaijikuta anazama kwa Nyemo bila kujua kuwa nyemo alikuwa amefuata kizuri akione lakini alijifanya kama alikuwa na pendo kama la Juma.
Nyemo alishakuona na Hussein akajifanya hajaona siku ile na Moringe akavunga na Charles siku ya mahafari akajifanya kalewa ili uibe vyema ukajiona wewe ni bingwa zaidi ya Messi wa Barcelona sasa Nyemo kakupa mimba na kaikataa Melissa ukaishia kulia na kulaumu na kumwachia huyo unayemwita Mungu.
Nyemo ameamua kukuachia hilo tumbo kwa kuwa alijua huenda si muhusika maana Moringe, Charles na Hussein hata Aman umewaweka wapi huenda ndo wahusika ila wewe ndiye mwenye kujua ukweli na unauhakika ni Nyemo na unahisi kakuonea Melissa.
mwisho wa siku nakuambi huyo Mungu unayemwachia huenda si nimjuaye .
Niambie ‪#‎mwanakalamu‬ mwenzangu umewahi kuwaona akina Melisa wangapi?

0 comments:

Post a Comment