ads

Wednesday 3 June 2015

PNC YULE WIMBO NA VIDEO KALI ILA UMETUSHTUKIZA

Na.Moringe Jonasy
Unakumbuka wimbo wa mbona alioimba kwa kumshirikisha Mr Blue?
Bila shaka utakuwa unajua kuwa huyu jamaa ni mkali wa nyimbo za kulalamika.Mpe chorus yako lazima akufunike muulize dogo janja atakuambia nini namaanisha maana alichokifanya kwenye wimbo wa Yamoyoni anakijua yeye.
PNC ambaye wengi walimsahau baada ya zile kelele za kumpigia magoti Ustadh Juma kuisha.
Huyu mkali kaja na video yake kali na wimbo wake ambao kama bahati nimeukuta whatsap baaa ya kutumiwa na kaka yangu kipenzi Steven Mwakyusa nikajikuta nakubali kila mstari aliouimba huyu mkali.
Tatizo huyu mkali wa utunzi ameutoa wimbo bila kuweka cover zake mitandaoni na kuweka jingo redioni kuwa alikuwa akitambulisha video kali.
Pengine amepost kwenye account zake tuu na rafiki zake ambao hata hatuwafahamu angetuma kwa Idris sultan, Shetta ,shilole, Alikiba, Wema Ommy dimpoz na Diamond ambao wana wafuasi wao wangeipost na kuipeleka taarifa mbali ili tutege masikio.
Lakini video kali kama ile katushtukiza kama alivyofanya mwenzake Rich mavocal kwenye pacha wangu ambayo licha ya ukubwa wake tumeishia kuisifia tuu na kuiacha ipite.
Basi bhana badilika kaka mwisho wa siku uje ulalamike akina fulani wanapewa promo ni akili tuu.
Niambie ‪#‎mwanakalamu‬ mtazamo wako

0 comments:

Post a Comment