Na.Moringe Jonasy
Nipo katikati ya shamba la mahindi nje tu na ninapoishi nanyosha nyosha viungo vyangu maana najihisi nina maumivu makali ya viungo.
Nasogea taratibu kuufuata Mwembe ambao upo katikati ya shamba ,lakini kabla sijaufikia mwembe huo ambao umebakiza maembe machache mabichi baada ya kukuru kakara za watoto wa mtaa wetu namwona mdudu mmoja akiwa amejificha katikati ya mahindi yaliyoangushwa na mchwa.Mdudu huyu sijawahi kumwona sehemu nyingine zaidi ya hapa Moshi ni kama nungunungu ila yeye ni mdogo sana wanamwita sijui Kirikuu sijui nini kwa kweli amejificha kweli kweli lakini namsumbua kwa kuyapiga majani ambayo yeye kachificha chini yake lakini anahangaika kujificha zaidi, namwacha na nazama kwenye lindi la mawazo.
Nikiwa nimeduwaa nashangaa mwili wangu unawasha kumbe unga wa mahindi maarufu kama poleni umetua mgongoni mwangu hapo napo nikapata wazo fulani ambalo linakatishwa ninapotazama mbele kidogo ya mwembe ambapo kuna makaburi kama matatu hivi.
Nikawaza maisha ya yule Kirikuu namna ya anavyoishi kwa shida maana anaweza kukutana na mtu mwingine akaanza kumpiga mateke na hata kumuua.
Mahindi nayo yanaonewa na mchwa lakini hata kufikia umri wakati wa kuliwa.
Nayafikiria mahindi na mimea mingine ikuzwayo ardhini lakini huishia kuwa vyakula vya viumbe wengine lakini nikifikiria juu ya uhai wa binadamu najikuta naiona ardhi hii hii ikuzayo mimea ndiyo huwala watu kwa kuwatunza kaburini.
Hapo wazo la kuwa nami nitaingia kaburini ama kutoingia humo ila uhai wangu huu najikuta nasisimkwa mwili kwa uoga.
Nami nitaachwa peke yangu kisha kuwa udogo?
Kama siamini si kama si kweli bali uoga unanifanya nisiamini.
Uoga huo huongezeka pale ninapogundua kuwa hata waliolala chini ya matuta hayo hawakujua siku ambayo walijikuta mle.
Tunatembea na kufanya mengi duniani bila kujua lini tutakuwa maiti.Siokushauri uogope kufa maana hukuogopa zaidi ulishukuru kuzaliwa bali nataka kukukumbusha wakati wowote kuanzia sasa utakuwa mfu.
Je, unakubaliana na madai kuwa kuna maisha baada ya kifo?
Kama unakubali umefanya nini ili uishi baada ya kifo chako ?
Maana si lelemama kufikia huko nadharia zinataka.
Najiangalia, nawaangalia ndugu, jamaa na marafiki zangu wengi nawaona wanahisi kuna siku wataambiwa kuwa kesho kutwa utakuwa maiti jipange leo.
Hakuna anayechukua hatua ndiyo maana licha ya uzinzi kuitwa dhambi lakini wanaweza kuzini na zaidi ya watu watatu ndani ya wiki moja.
Walipoambiwa wasiue mbona wanatoa ama wanasababisha kutoa mimba?
Mbona waliambiwa wasiseme uongo ila kwa sasa wanaongopa hata mbele ya vyombo vya habari?
Siku za bwana kwao zimekuwa siku ya kile wanachokiita bata?
Tamaa ndo usiseme wanafikia kuroga na hata kuua ?
Au wanataka kutuaminisha kuwa ni hekaya za mafunzo za kuleta amani na maadili tuu bali hakuna chochote?
Lakini kama hekaya ina maana Mungu alituumba tuishi miaka pungufu ya mia kisha tufe wazaliwe wengine ?, mchezo gani huo?
Lazima kuna kitu tumejiandaaje kwa maisha hayo?
Ujana ndo kabisaa hauna urafiki na maisha baada ya kifo maana kila amri tulizoambiwa zinavunjwa hapo.
#mwanakalamu unasemaje?

0 comments:
Post a Comment