Friday, 12 June 2015

ALIKIBA NA KILE KINACHOITWA ''DIE HARD FANS''
Na.Moringe Jonasy
Nadhani we ni mmoja wa mamia ya watu wanaliojiuliza ama wanajiuliza swali hili.
Kwa nini Amefanikiwa kurudi kwenye muziki baada ya kimya na kuanzia alipoishia kitu ambacho ni nadra kutokea?
Ni wachache walioweza kufanya hivyo kabla yake alifanya mtu mmoja tuu, Lady Jay Dee ambaye baada ya kimya kiefu alirejea na wimbo aliotungiwa na kutayarishwa na Bob Junior akimshirikisha Mr Blue 'Wangu'.
Kuna mengi yamesema juu ya kurudi kwake kuna waliodai kuwa alitumia jina la mkali mwingine kwenye muziki 'Diamond' pale alipomtuhumu kumdharau baada ya kumfuta kwenye wimbo wa lala salama kisha kudanganya umma kuwa Ally Kiba ndiye aliyemfuta kwenye wimbo wa single boy lakini madai hayo yanakosa mashiko kwani ni wasanii wengi sana wadogo na wakubwa waliwahi kukorofishana ama kukorofishwa na Diamond lakini wakaishia kuzungumzwa na kuandikwa magazetini na mitandaoni kisha wakapotea ila kwa Ally amebaki kuwa msanii mkubwa.
Pia kuna waliowahi kudai kuwa Alikiba ni msanii mkali na kazi zake zinazoishi ndizo zilizomrahisishia kazi ya kufuta vumbi la kiti chake.
Zifuatazo ni sababu chache zilizomfanya Alikiba asihangaike sana kuurudia Ufalme aliokuwa nao :
1. WAFUASI ' DIE HARD FANS'
Haikuwa kazi rahisi kuwatengeneza hawa watu bali kwa kazi kubwa aliyoifanya kwenye Album zake mbili alijikuta akitengeneza kundi kubwa la watu ambao hawakuwa mashabiki tuu bali walipitiliza na kuwa wafuasi.Hao ndio waliokuwa wakimsumbua redioni na mitandaoni na kumtaka arejee kwenye muziki na kutaka kujua kilichomfanya apooze.
Wafuasi hao ndio waliozifanya nyimbo alizokuwa ameshirikishwa kuwa kubwa kwa kuziomba kwenye vipindi mbalimbali vya redio na Televisheni , zikiwaaminisha kuwa mwanamuziki wanayemfuata hakuwa 'underrated' kama ilivyodaiwa na wengine.
Kwa kujua kuwa alikuwa na kundi hilo la watu wala hakuhangaika kuupromote wimbo wake sana na hata alipouachia usiku ule wa tarehe 27 july mwaka jana ilikuwa kama mchana na mkito ikazidiwa na nguvu ya wafuasi hao waliokuwa wamemmis mfalme wao.
Wafuasi hao walimsukuma sana kutoa video mapema kwani walikuwa wakitamani kuona maendeleo ya mfalme wamfuataye kwenye video kwani alishawahi kukiri kuwa hakuwa serious sana kwenye video lakini ujio wake ulikuja na ahadi ya kufanya mambo mazuri zaidi aitumia kauli mbiu yake ya 'Bampa to bampa' ndivyo alivyofanya pale disemba 19 mwaka huo huku video yake ikivunja rekodi kadhaa za kutazamwa ndani ya masaa ishirini na nne.
Licha ya video hiyo kukosolewa na baadhi ya watu kutokana na wengi kujitengenezea script zao kichwani lakini video hiyo ilienda mbali hadi kupigwa kwenye vituo vikubwa vya TV duniani kama Trace urban.
Wafuasi walifanya mengi mwaka huu ikiwa ni pamoja na kumpendekeza kwa kumpigia kura kwenye tuzo za watu na tuzo za Muziki za Kilimanjaro na tayari wameshampa tuzo kwenye tuzo za watu na kumpa vipengele zaidi ya vitano kwenye tuzo za muziki kilimanjaro.
Na kwa nguvu ya wafuasi hao kumpigia kura si ajabu akifanikiwa kuchukua tuzo zaidi ya sita kwani wafuasi hao wanajituma haswa kupiga kura huku wakiapa kutorudia uzembe walioufanya miaka ya nyuma pake Mfalme wao aliposhiriki kwenye tuzo mbalimbali za ndani na nje zikiwemo KORA na BFTA.
2.UBORA WA KAZI ZAKE
Licha ya kuwa na nyimbo nyingi nzuri zilizompa Ufalme wa Bongo Ally ni miongoni mwa wasanii wachache wenye uwezo wa kutoa nyimbo kubwa zaidi ya zilizotangulia kitu ambacho Kwa Mwana FA imekuwa kawaida kwake.
Mwana na chekecha cheketua bila msaada wa video zilifanikiwa kuwasahaulisha watu Dushelele , Nakshi nakshi na nyingine nyingi.Hiki ndicho kilimfanya aongeze wafuasi wake ambao kwa muda waliamua kuwa mashabiki wa wasanii wengine na sasa wamerudi kwa mfalme wao na sitoshangaa akiwa mkubwa zaidi ya alivyo sasa.
3.ROCKSTAR 4000
Wengi wamekuwa wakiilaumu management hii kwa madai ya kutojua biashara ya Afrika , huenda hawaijui vizuri kampuni hii ambayo ipo chini ya Sony.Hawa ndio wanaommeneji Rose mhando, Redsun, Treysongz na wengine wengi akiwemo Fally Pupa wa Kongo.
Wanamuziki wengi wa Afrika wana ndoto ya kuwa chini ya usimamizi wa kampuni la ukubwa huo.
Leo hii Alikiba akitoa album wao ndio watakao husika kuisambaza na kusimamia uuzwaji wake na kwa uzoefu na teknolojia waliyonayo habari za kuwa Album hazilipi zinaweza kuwa hadithi na Mhindi hatolalamikiwa tena.
Hawa ndio waliomtuliza Ally kwani kwa hali ya kawaida ya kushindanishwa na kupambanishwa na mwanamuziki nguli kwa sasa Afrika (Diamond) angejikuta akikurupuka na hata kutoa nyimbo mbovu lengo likiwa ni kutaka kuwaridhisha mashabiki ambao wamekuja kumshabikia baada ya kuwa na chuki na mafanikio ya Diamond.
4.LIVE BAND
Kwa wasiojua muziki wanaweza wasijue thamani ya kufanya muziki live ila kwa wanaoujua muziki huu ni zaidi ya sanaa.
Kwa sababu hizo na nyingine nyingi zitaendelea kumpandisha Alikiba na kufika mbali zaidi ya alipofikia na kuwa miongoni mwa mwanamuziki halisi wa kizazi hiki nchini.Huku wafuasi wakiendelea kumsaidia kufika huko mapema.
Niambie chochote ‪#‎mwanakalamu‬ mwenzangu

0 comments:

Post a Comment