ads

Friday 5 June 2015

YA MO MUSIC NA "BASI NENDA", JE WIMBO ULIMZIDI UKUBWA?




Na.Steven Mwakyusa
Mara nyingi imetokea kwa wasanii wa muziki wa aina mbalimbali kuhit na wimbo mmoja na baadaye kupotea! Tukijaribu kuangalia kwa hapa nyumbani list ni ndefu sana, kuanzia kwa akina Adili(Peke yangu), Balozi (kwenye chatt),Chelea man (Usiniache), B.boy(Sina demu), JI (Kidato kimoja), Bablee (Kiziz), Buibui (Nimekusamehe) na Hmbizzo (Mchumba)!!
Hawa wote ni wasanii ambao uwezo wao haukutia shaka katika nyimbo zao, sitaki kuamini kama walibahatisha kama wengi ambavyo huwa wanasema, hapa nadhani yote ni matokeo ya kutengeneza wimbo mkubwa ambao baadaye hugeuka kuwa "benchmark", hivyo chochote msanii anachoimba baada ya hapo, kinachoitwa wimbo mkubwa kinakuwa kama "refference point" ya kuamua kama umeweza ama umevurunda, sasa inapotokea msanii akashindwa "kumeet customer's expectations" hapa kwa maana ya mashabiki ndipo kupuuzwa huanza na kadhalika!!
Haya yaliyowakuta wasanii wengi huko nyuma naanza kuyaona kwa kwa Momusic, huyu ni msanii aliyejitambulisha vyema na "hitsong" ya "Basi nenda", kwa kifupi ulikuwa wimbo mkubwa pengine tofauti na matarajio yake, wengi walifananisha uimbaji wake na Marlaw huku wengine na mimi nikiwemo sikuweza kumtofautisha na Becka hasa katika wimbo wa Narudi kazini!! Hatimaye siku zilienda na nikawa nina hamu ya kumsikia katika kazi nyingine!
Alipotoa "almasi" sikumuelewa kabisa hata alipotoa "Simama" sikumuelewa pia na hata huu wimbo wa siku za karibuni "Nitazoea" bado nilipata shida kumuelewa mpaka niliposhawishiwa kuusikiliza na mtu wangu wa karibu.
Nilichokuja kugundua ni kwamba, si kwamba Mo music hatoi nyimbo nzuri, hapana ila kinachomtafuna ni "Basi Nenda", mpaka sasa kashindwa kutengeneza kazi itakafika pale au kuizidi na mbaya zaidi anachoimba ni muendelezo wa Basi Nenda! Sasa huu muendelezo wa nyimbo unanipa shaka na mwendo wake, je wewe kama mfuatiliaji wa muziki wa hapa nyumbani unamuona huyu kijana akipiga hatua?

0 comments:

Post a Comment