ads

Friday 5 June 2015

KOLABO SABA NISIZOTAMANI ZITOKEE BONGO



Na.Moringe Jonasy
Kwa kawaida tumezoea kusikia wanamuziki mbalimbali wakishirikiana na kutoa wimbo wa pamoja wanaweza kuwa wawili ama zaidi wenyewe wanaita Kolabo.Kolabo zimekuwa zikitumika kuchanganya ladha na kuwaburudisha wapenzi wa muziki, kuwatambulisha wasanii chipukizi kwenye uwanja wa muziki  na hata kuongeza na kuunganisha mashabiki.
Hapa nchini tumeshuhudia ngoma kubwa sana ambazo kwa wasanii kushirikiana zimefanya kazi kubwa ya kuufanya muziki wetu kukua kila siku.Nyimbo kama Number One remix,Nai nai, Kerewa, Ukisikia Paah Remix ,Kumi na tatu,Vitamini muziki,Kidela , Nana , bila kukunja goti , Kidela na nyingine nyingi nikiana kuziorodhesha naweza jaza kurasa zaidi ya tano.
Licha ya kolabo kuwa na matokeo chanya kwenye muziki lakini kuna kolabo ambazo najikuta sitamani zitokee.

1.BELLE NINE & BEN PAUL
Wote naweza kuwaita ni chorus killers lakini kwa wimbo wao wa anaishi naye nikajikuta kutotamani kusikia wimbo wao tena labda wamwongee mtu mwingine.Si kwamba wanamuziki hawa ni wataalamu wa kuimba na kushirikishwa kwenye nyimbo nyingine lakini kwa wakali hawa kuimba wawili mhh Hapana.
Lakini wanaweza kufanya kitu kingine kikali.

2.ALIKIBA & OMMY DIMPOZ
Unaweza ukasonya baada ya kusoma majina ya hawa wanamuziki lakini ukweli ni kwamba wakali hawa wa Nai nai iliyowapa tunzo za muziki za Tanzania miaka michache iliyopita kinachonifanya nisitamani kusikia tena wimbo wao mwingine kutokana na mzimu wa wimbo huo mkubwa utatutesa masikioni na hata wakija kuimba wimbo mzuri utalinganishwa na Nai nai na kuonekana si kitu.Lakini wanaweza kutengeneza hit nyingine itakayoturudisha nyuma.

3.FID Q &AFANDE SELE
Unaweza kutukana na kutamani kuacha kusoma baada ya kusoma na hii , lakini kwa upande wangu naona wakali hawa wa muziki sijui wakija kuimba waimbe kitu gani.Na wakija kuimba kitu kikali kwao ila kwa mashabiki wanaweza kujikuta wakipenda sehemu fulani ya wimbo ama iliyoimbwa na Fid ama ile iliyoimbwa na Afande.Lakini wanamuziki hawa wanabebwa na tabia yao ya kupenda kujifunza na kutengeneza hit.

4.ALIKIBA & DIAMOND
Hii inaweza kuwa kali kibiashara kwani inaweza kutengeneza wimbo uatakao vunja rekodi nyingi za kupakuliwa ,kutazamwa na kuleta matamasha ya ndani na nje mwanzoni.Ubora wa wimbo hautapewa kipaumbele zai namna ya kutanganzwa na kuachiwa ndicho kitakuwa kitu cha msingi sana na kuvunja Aliences ambazo zimejijenga kwa makampuni ya simu hasa kwenye kipindi cha kupiga kura za tuzo  hayatanufaika kwani kasi na ushindani wa kuwapigia kura wanamuziki hawa itapungua.
Hivyo kolabo ya wakali hawa wa muziki haitakuwa na ladha tunayotarajia kutoka kwao hivyo kwa maoni yao wasanii hawa wakitaka kufanya kolabo wasifanye peke yao aongezeke mtu wa tatu kati na kuleta uji badala ya mafuta ya taa na maji.

5.FID Q & ROMA
Hakuna sababu ya kuzuia kolabo yao lakini kitu kinachonifanya nisite kutamani kolabo yao ni kujaribu kufikiria kitu na namna ya kuimba kwenye huo wimbo.Kwa aina ya uimbaji na utunzi wa wasanii hawa naona kabisa kutengenezwa kwa maji na mafuta ya taa na maji na kuifanya kolabo ya kawaida.Ila wana nafasi ya kutengeneza album ya pamoja ambayo itakuwa na nguvu kuliko kolabo ya wimbo.

6.DIAMOND & NEY WA MITEGO
Unaweza ukanicheka na kunitukana ila kwa upande wangu sitotamani kusikia kolabo yao tena licha ya kutengeneza hit kali kama muziki gani na ngoma inayofanya vizuri kwenye stesheni nyingi za redio kwa sasa Mapenzi au Pesa wanamuziki hawa wanaonekana kukosa namna nyingine ya kushirikiana zaidi ya kubishana.Nadhani legacy ya matokeo ya wimbo wao waliofanya kama utani wa muziki gani bado inawatafuna na kujikuta wakibaki kwenye njia ile ile ya mwanzo.
Lakini pia katika kolabo zao mara nyingi nimeona Diamond akifanya kazi kubwa ya kuchanganya uji huo ili usiwe mafuta na maji kwa hiyo siku akilega tutegemee wimbo maarufu lakini mbaya.

7. RACHEL & RAY C
Nayo inaweza kukuacha mdomo wazi kushangaa kwa nini siipendi na kuniona mtu wa ajabu, ila kwa upande wangu naona utakuwa wimbo ambao hatutaweza kujua nani kaimba wapi.Rachel ni Ray C mpya na huo wimbo utakuwa si uji tena bali utakuwa maji.Ila kolabo itafanywa kwa msukumo wa kibiashara  na itawafurahisha wengi kwa upande wangu natamani matamasha na album ya pamoja.

Kwa upande wangu nimejikuta sitamani kolabo hizo japokuwa sinaweza kuja kutokea kwa sababu ya misukumo ya mashabiki ama kibiashara ila kwa chemistry ya muziki wenyewe  hazitakuwa nzuri.Nitumie nafasi hii kuandika wasanii kolablo ambazi hazitowachosha wasikilizaji; SHETTA & DIAMOND, AY & FA, ALIKIBA & ABDUKIBA,STAMINA & JUX, WEUSI nanyingine nyingi.

Niambie mtazamo wako #mwanakalamu

0 comments:

Post a Comment