ads

Friday 5 June 2015

FEROUZ MFALME NA MWANZILISHI WA VINGI SANA.

Na.Moringe Jonasy
Unaukumbuka wimbo wa starehe alioimba na kumshirikisha Profesa Jay?
Basi utakuwa unakumbuka jinsi ule wimbo ulivyokuwa na nguvu nje na ndani ya nchi zilizokuwa zikitumia lugha ya kiswahili.Ulikuwa si wimbo tuu bali ulikkuwa ni kama filamu fulani hivi iliyoamsha na kuchochea mapambano dhidi ya UKIMWI maana ulikuwa ni moja ya mambo yaliyokuwa yanasumbua jamii tofauti na siku hii ambapo Ufisadi unaonekana kama tatizo kubwa kuliko yote>
Ilikuwa si ajabu kumkuta mwanafunzi ameandika mistari ya wimbo huo ama ametunza gazeti ama jarida lililokuwa na mistari ya wimbo huo na wengine wakiimba bila hofu wakla mashaka maana haukuwa na tusi ama neno baya la kusema litamfanya amuogope mzazi ama mkubwa wake.
Kwenye makongamano na matamasha mengi ulikuwa ni kama wimbo rasmi kwa shughuli.Utamwambia nini kijana wa zama zile juu ya wimbo huo?
Unaweza kumfanya akutukane maana kupitia wimbo huo ndipo kulipozuka wimbi kubwa la vijana walioanza kuimba nyimbo za UKIMWI na hadi leo hii wamejikuta kama si waimbaji basi watakuwa ni watu fulani waliokaribu na Muziki.
Kwa desturi zetu watanzania hata kama wengi walishawishiwa na huyu Mfalme kuimba na kuwa nyota wa Muziki hawawezi kumtja wataishia kuwataja akina Chris Brown japokuwa lugha anayoimbia huyo Chris amejifuza juzi juzi kwa Rasi Simba.
Ni wimbo uliomvutia hata aliyekuwa Rais wa Muungano wa Tanganyika na Zazibar aliyekuwa mbali kidogo na muziki kuusikiliza na kumzawadia Ferouz.
Ferouz ndiye aliyewafanya wengi wabadilike kwa kuanza kuona kazi ya ziada ya muziki zaidi ya kuburudisha na kujisifia.
Kwa albam yake iliyokuwa na wimbo huo watu wengi walipata sana fedha bila jasho huku wakimfanya Ferouz kuwa miongoni mwa wasanii ambao leo hii wanahangaika kuinuka na kurejea juu si tuu kisanii bali hata kiuchumi.
Album iliyokuwa na wimbo mkali kama mkasa wa bosi na hiti nyingine kali kwa tuliokuwa tunatumia Tape hatukuwa na kile tulichokiita Nenda side B ilikuwa ni hit baada ya Hit na aliwafanya wengi wapate raha ya kuwa na album.
Nikisikiliza nyimbo zake alizoimba na alizoshirikishwa nabaki najiuliza kama kuna atakayeweza kuvaa viatu vyake kimuziki.
ILA KWA NINAVYOIJUA TANZANIA AKIFARIKI NDIPO UTAKAPOKUJA KUJUA FEROUZ ALIKUWA NA KIPAJI KARIBA YA ALBERT MANGWAIR.
Niambie mtazamo wako ‪#‎mwanakalamu‬ mwenzangu.

0 comments:

Post a Comment