ads

Friday, 1 January 2016

KALAMU YANGU 'YAPATA MTOTO' MWAKA MPYA


Ni siku ya furaha kwa kila mwanadamu kuuona mwaka mpya, wengi walitamani kuuona huu mwaka lakini wameshindwa kuuona huku malengo yao mengi juu ya mwaka huu  yakizikwa bila kutimia hata kujaribiwa.
Naam ni mwaka mpya kila mtu anaupenda kama matatizo yatakuja basi tunajua ni kawaida kwa kiumbe yoyote kukutana na matatizo anapopambana na mazingira katika kupata mahitaji yaliyo muhimu na yale yasiyo ya muhimu.
Kalamu yangu inawapongeza wote walioufikia huu mwaka na tunawapa POLE wote waliowapoteza wapendwa wake mwaka uliopita.Pia tunampongeza mwanakamu Mwenzetu Steven Mwakyusa ambaye anatimiza miaka kadhaa tangu azaliwe kule kwetu mtoto huyu tungemwita 'Mwaka' ila wacha tumwite Steven Mwakyusa Mtu makini kama apendavyo kuitwa.

HONGERA   KAKA STEVEN MWAKYUSA MUNGU AKUONGEZEE HEKIMA NA BUSARA NA MIAKA MINGI YA KUISHI YENYE BARAKA ZAKE.

2 comments: